Njia zinazotumika kufanya utapeli na wizi kwenye M-pesa,Tigo-pesa na Airtel money

Mkali_01

Senior Member
May 13, 2015
166
116
Habari zenu ndugu zangu. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo, tujadiliane mbinu tofauti tofauti wanazotumia matapeli ili kuibia mawakala wa M-Pesa, tigo pesa na Airtel money. Hii itasaidia kufichua mbinu zao tofauti tofauti ili mawakala wawe kwenye safe side. Majanga ya kutapeliwa siku hizi yamekua mengi na ukiangalia faida inayopatikana na biashara hiyo ni ndogo. Karibuni
 
Kuna tecniq ambayo mtu anakuja kutoa hela, badala ya kutoa kwa kutumia namba ya wakala kwa mfano tuseme voda 406020 yeye anatoa kwa kutumia namba ya kawaida ya simu 0754563433. Kinachofanyika hapo ni kwamba anafoward sms ya kwamba ametoa pesa kwako kumbe hajatoa. Kugundua hilo inabidi sms yoyote utakayoipata jina la mtumaji lazima liwe M pesa vinginevyo utakua ni wizi
 
Back
Top Bottom