Njia salama ya kutunza vyeti vyako

Kwenye Drive nimeweka Contacts za sim yangu na my current Memory card data. So i can access them from anywhere, also Hata nikibadili sim or ikipotea 4 instance all i do is download them and sync them up with the new 4ne then its like it never happened. Karibu everything important of mine is in the drive, very helpful indeed at times.
 
Habari zenu wana JF, Leo nakuja na njia mbadala ya kutunza vyeti vyetu tumekuwa tukisikia kila siku kwenye radio au kusoma magazetini watu wamepoteza vyeti vyao na ni vyeti muhimu sana katika maisha haya ya kuajiriwa, na kujiajiri.
Wengi wetu njia tunayotumia kuhifadhi nakala halisi ya vyeti vyetu ni makabatini wengine kwenye mabegi na baadhi kwenye safe lock. Ila tunasahau haya ni makaratasi tu lolote linaweza tokea yawe maji, moto, kuibiwiwa au hata kupoteza. Sasa Nawashauri wale wote mnaotaka usalama wa vyeti vyenu mfanye mpango muwe softcopy backup ya vyeti vyenu.
Scan vyeti vyako vyote muhimu na hifadhi online hii itakusaidia hata vile original vikipotea au kuharibiwa na pia unaweza pata access ya nakala ya vyeti vyako popote pale uendapo.

Sehemu za kuhifadhi:
Kuna online storage nyingi sana unazoweza tumia kuhifadhi nakala zako hizi ni baadhi tu:

4shared- hapa wanatoa 15GB free (unafungua account)
Drop box- Nayo free
Google Drive- free
Icloud- wale wa apple products hii nayo safi
Sky drive- wale wa microsoft.

Hizo ni baadhi tu ila zipo nyingi. natumaini wengi mtahamasika.
Akhsanteni.

Sawa inasaidia lakini je softcopy ya original inatosha? Maana interviews chache nilizowahi ku-attend huwa wanataka original certificate tena upeleke hardcopy.

Anyway thanks kwa idea hii pia, binafsi nimejitumia vyeti vyangu kwenye email yangu.

Unachosema ni kweli isipokuwa umesahau kwamba unapo poteza vyeti vyako unajikuta hujui unaanzia wapi kuvipata.
Ila ukisha kuwa na soft copy kazi utakayo kuwa nayo ni kuvi certify tu kwamba ni nakala halisi za vyeti vyako hata ukienda kuomba vingine ni rahisi wao kukusaidia tofauti na ukiwa huna kitu.

anayepaswa ku-certify lazima aone original ndo agonge mhuri na ku-sign

Nadhani jambo la kwanza kabisa ni kuvipeleka vyeti halisi (Original) kuwa certified kisha unazitunza hizo soft copy za certified copies kwenye hizo cloud na mengineyo au simply kujitumia kwenye email. Ni wazo zuri kwakweli.

Kama mtu unafaham kitu na mtu mwingine anakuja na ushauri unaodhani kwako sio muhimu au umepitwa na wakati, sio lazima ubeze, kuna watu itawasaidia.

Kisha ukiweza sio mbaya ukinnunua ka safe kadogo ukaweka document zako muhimu huko huku certified soft copies zikiwa zimehifadhiwa ki digitali.
 
Kwenye Drive nimeweka Contacts za sim yangu na my current Memory card data. So i can access them from anywhere, also Hata nikibadili sim or ikipotea 4 instance all i do is download them and sync them up with the new 4ne then its like it never happened. Karibu everything important of mine is in the drive, very helpful indeed at times.

We kijana hiyo lugha yako tuu!.mimi hoi utadhani nasoma comment ya Wema Sepetu vile, maana yeye ndo mtaalamu wa hicho kilugha cha "it's like, you know wora i min", na vitu kama hivo, hatari sana.
 
We kijana hiyo lugha yako tuu!.mimi hoi utadhani nasoma comment ya Wema Sepetu vile, maana yeye ndo mtaalamu wa hicho kilugha cha "it's like, you know wora i min", na vitu kama hivo, hatari sana.

Dah we mheshimiwa mbona una majungu sana!!!!!!!!!!
 
Ahsante, binafsi nilianza kuitumia google-drive kitambo. Huko nimetunza documents kibao, picha za familia, video na nyimbo. Pia hata coresponding docs kati yangu na office mbali mbali nimezitunza huko..
 
Kwani vyeti navyo ni siri? Kama unaogopa basi weka files zako ndani ya Encrypted ZIP file kabla ya kuupload au tengenza TrueCrypt container, weka files zako kisha upload.

Hii hiko deep kidogo ebu funguka in a layman's language utatusaidia hata kwny mengine
 
Akusaidia kufanya nini'? Mbona rahisi hata wewe mwenyewe unaweza. Scan vyetu weka kwenye e mail yako

Kujitumia kama email nisingependa kumshauri mtu maana kwa mtazamo wangu it's not safe kwa asilimia nyingi otherwise uwe makini sana.
Nalisema hili kwa sababu kuna kipindi inbox yako inakua na mails nyingi na unataka kuzifuta kwa sababu majority ni notifications au matangazo ya biashara wengi wetu uona ni kazi kuchagua moja moja na kuanza kuifuta matokeo yake anaamua kuempty inbox yake kwa kuclick select all hapo impact yake ni kuifuta hata ile email yako uliyojitumia..
Ushauli wangu Google drive ndio habari ya mujini ni safe almost 99% other ways mtumiaji haikosee
 
We kijana hiyo lugha yako tuu!.mimi hoi utadhani nasoma comment ya Wema Sepetu vile, maana yeye ndo mtaalamu wa hicho kilugha cha "it's like, you know wora i min", na vitu kama hivo, hatari sana.

comparing Good Guy to Wema! Apologise immediately then we'll talk
 
thanx ngoja nimtafute mtu wa computer science anisaidie
Mtafute mtu wa stationery au kule kwenye vyuo vya kompyuta mitaani. Mtu wa computer science ana kazi muhimu sana za kufanya kuliko kupandisha vyeti google drive.
 
Ahsante, binafsi nilianza kuitumia google-drive kitambo. Huko nimetunza documents kibao, picha za familia, video na nyimbo. Pia hata coresponding docs kati yangu na office mbali mbali nimezitunza huko..
Aisee umetunza corresponding docs huko??!!!!! Dah si mchezo kazi ipo.
 
Hii hiko deep kidogo ebu funguka in a layman's language utatusaidia hata kwny mengine
Unapotengeneza zip file au rar file kuna option ya kuifanyia file hiyo encryption na kuweka password, kama password yako ni secure enough hizi file ni practically impossible kusomwa na mtu asiye na password. So kama unaogopa usalama fanya hivyo kabla ya kuupload file zako. Mfano hapa natumia 7zip kuwekea zip file password.
picha.png

TrueCrypt nayo ni program ya Encryption ambayo unaweza kutengeneza Encrypted containers ambazo unaweza kuweka files ndani yake, na yasisomeke na mtu mwingine. Pia unaweza kuencrypt HD nzima ukitaka.
 
Sawa mkuu. Ila navyojua mimi huwa wahusika hawa certify original document bali huwa wana certify true COPY of the original in presence of the original document.
Document zenye shaka na ambazo huwa zinatakiwa kuwa certified,ni zile Copies. Ndio maana askari traffic akikuuliza kadi ya gari,ukimpa original hana tatizo,lakini ukimpa copy na ikiwa haiko certified ataikataa!
Nadhani jambo la kwanza kabisa ni kuvipeleka vyeti halisi (Original) kuwa certified kisha unazitunza hizo soft copy za certified copies kwenye hizo cloud na mengineyo au simply kujitumia kwenye email. Ni wazo zuri kwakweli.

Kama mtu unafaham kitu na mtu mwingine anakuja na ushauri unaodhani kwako sio muhimu au umepitwa na wakati, sio lazima ubeze, kuna watu itawasaidia.

Kisha ukiweza sio mbaya ukinnunua ka safe kadogo ukaweka document zako muhimu huko huku certified soft copies zikiwa zimehifadhiwa ki digitali.
 
Sawa mkuu. Ila navyojua mimi huwa wahusika hawa certify original document bali huwa wana certify true COPY of the original in presence of the original document.
Document zenye shaka na ambazo huwa zinatakiwa kuwa certified,ni zile Copies. Ndio maana askari traffic akikuuliza kadi ya gari,ukimpa original hana tatizo,lakini ukimpa copy na ikiwa haiko certified ataikataa!

Nimekupata mkuu, ndio maana nikasema jambo la kwanza nikuchukua original documente zako, unazitoa copy, kisha una zicertify kwa vyombo husika vinavyotambulia (wanasheria) n.k Sasa hapo ndio unascan hizo certified copies na kuzihifadhi ki elektroniki. Tuko pamoja.
 
Kama unaogopa originals kupotea ni bora kutoa copy kisha kucertify halafu kuhifadhi copy hizo kwa ndugu au rafiki, na yeye anaweza kufanya vice versa, maana balaa la moto au wizi sio rahisi kuwakumba wote wawili kwa mpigo. Hii tunaita off-site backup kitaaalamu!:amen:
 
Google Drive is My peace of Mind. Nmehifahdi picha za Mwanangu from Day One hadi hii leo 4yrs. Almost picha zake kama 3200. My Wedding Video and Still Picture and so forth. Google keep it up Innovating.
 
Back
Top Bottom