Njia salama ya kuendesha boda boda mijini

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kama ilivyo taratibu waendesha boda boda wanatakiwa kufuata taratibu zile zile zinanoelekezwa na Usalama barabarani lakini hii imekuwa kinyume kabisa. Baadhi ya makosa yanayofanywa na waendesha boda boda ni haya yafuatayo:-
  • Boda Boda kuendesha kushoto mwa magari badala ya kuwa nyuma ya gari kama taratibu zinavyoelekeza.
  • Boda boda kupita (overtake) gari au piki piki upande wa kushoto badala ya upande wa kulia.
  • Waendesha boda boda (baadhi) kutovaa kofia za kinga (Helmet) pindi wanapoendesha vyombo vyao.
  • Waendesha boda boda kupita kwenye mataa hata pale taa inapoonyesha nyekundu.
  • Waendesha boda boda kuwa na kiburi na kuendesha bila nidhamu.
Haya yote yanafanyika wakati Maaskari wa Usalama wapo na wanawaona kila mara. Mfano hai ni kwenye mataa pale Buzuruga (Mwanza) ambapo Maaskari wapo kila wakati na bado wanawafumbia macho boda boda. Afande Mpinga tunakupa taarifa ili kuwepo na marekebisho.
 
Kama kuna watu wanajifanyaga hawana akili basi ni waendesha bodaboda.... wanatia hasira sana
 
Back
Top Bottom