Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 275
- 262
Mawazo yako ndio yanaongoza ndoto zako usiyaache yakapeperuka na kubadilika kila siku andika utapata msingi wa kuanzia ili kuifikia ndoto yako.
Unaweza kuwa na ndoto moja ila namna ya kuifikia kunakuwa na njia nyingi zinakuja kichwani mwako bila kuandika utajichanganya mwenyewe,weka ama tengeneza tabia ya kuandika mawazo yako sio lazima utembee na daftari maisha yamebadilika utandawazi unarahisisha mambo hata simu yako inasehemu ya kutunza kumbukumbu kama hizo (notes).
Andika kisha pitia na fanya tathmini,ukiyaandika mawazo yako kwenye maandishi ndio unaongeza uwezo wa kulifanya hilo wazo kwa uhakika zaidi.
Usidharau aina ya wazo ama kujiona umewaza pafupi,ukitaka kujitathmini wewe kama wazo lako sio dogo angalia kuna kiwanda cha kutengeneza pipi ambayo hiyo pipi inauzwa Tshs. 50/= yaani hadi kimejengwa kiwanda lakini kwa kutengeneza bidhaa ya Tshs.50 zamani tsh 10/,wazo lako ni kubwa na hakuna biashara isiyolipa ni mtazamo wako tu.Andika ndio mwanzo wa kufanya vitu kwa uhakika.
Jumapili njema.
Elisha Chuma.
Mshauri wa Branding,Biashara na Ujasiriamali.
@elishachuma