Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,796
- 3,362
Kwa wale wafugaji wa kuku wa kienyeji na wasio na uwezo wa kupata artificial incubators, fuata njia hii kutotolesha vifaranga vingi katika kipindi kifupi.
- Uwe na majike kadhaa wanaotaga (mfano 40)
- kusanya mayai yatakayotagwa ndani ya wiki 2 (yatunze vizuri yasiharibike)
- Kawaida kuku wa kienyeji hutaga mayai 12-14 kabla ya kupumzika kutaga (kutaka kuatamia)
- Kuku atakaenyesha dalili za kutaka kuatamia katika kundi,mwekee yai moja aatamie
- Endelea vivyohivyo kwa kuku watakaoonyesha kuatamia hadi watakapofikia idadi kuku 10
- Andaa chumba kizuri chenye mwanga,kisafi na nafasi ya kutosha kukaa kuku 10 bila kubanana
- Katika chuma hicho,weka viota (nests) 10- unaweza kutumia boksi ndogo,tia mchanga laini,na tandaza majani laini au pamba juu ya mchanga.
- Chukua mayai,yapange ndani ya viota hivyo (mayai 12 kila kiota)
- Chukua kuku wale 10,wapange katika viota hivyo. Yai moja kila kuku waliokuwa nayo,yatupe.
- Kwenye chumba hicho,weka vyombo vya maji na maji,vyombo vya chakula (chenye mchangayiko mzuri),pia usisahau kuweka dawa ya kuzuia wadudu (viroboto,utitiri nk)
- Baada ya siku 21, mayai yataanguliwa (90%-98%). Wanyanganye kuku vifaranga vyote,na vihamishie kwenye artificial brooder (sehemu ya joto ya kukuzia vifaranga). Wakati unaondoa vifaranga,rudishia mayai mengine kwa idadi ile ile na kuku walewale.
- Nashauri ufanye mizunguko ya aina hiyo 3,ndo uwapumzishe kuku au kubadilisha wengine.
- Kwa hesabu rahisi, kuku 10 @ vifaranga 12 = vifaranga 120 (siku 21), na ukirudia ni vifaranga 240 (siku 42) sawa na vifaranga 362 (siku 63=miezi 2). Hii ina maana kama utatumia kuku 20 kuatamisha, utakuwa na vifaranga 724 ndani ya miezi 2.
- Kama vifaranga hivi vitatunzwa vizuri (mada itakuja wiki ijayo) baada ya miezi 2 ya kukua, kwa bei ya soko ni Tsh 3,000/= kwa kifaranga kimoja x 724 (endapo hakuna vifo) = 2,172,000/=
- Kwa kuku wa kienyeji ambao kwa sehemu kubwa hawahitaji gharama kubwa ya chakula na madawa 25-30% ni gharama za madawa na chakula cha ziada.
- Ukifanya tahmini utagundua kuna faida kubwa. Karibuni tupunguze au kuondoa kabisa umasikini wa kipato