Njia rahisi ya kutotolesha vifaranga vingi bila kutumia mashine (incubators)

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Kwa wale wafugaji wa kuku wa kienyeji na wasio na uwezo wa kupata artificial incubators, fuata njia hii kutotolesha vifaranga vingi katika kipindi kifupi.
  1. Uwe na majike kadhaa wanaotaga (mfano 40)
  2. kusanya mayai yatakayotagwa ndani ya wiki 2 (yatunze vizuri yasiharibike)
  3. Kawaida kuku wa kienyeji hutaga mayai 12-14 kabla ya kupumzika kutaga (kutaka kuatamia)
  4. Kuku atakaenyesha dalili za kutaka kuatamia katika kundi,mwekee yai moja aatamie
  5. Endelea vivyohivyo kwa kuku watakaoonyesha kuatamia hadi watakapofikia idadi kuku 10
  6. Andaa chumba kizuri chenye mwanga,kisafi na nafasi ya kutosha kukaa kuku 10 bila kubanana
  7. Katika chuma hicho,weka viota (nests) 10- unaweza kutumia boksi ndogo,tia mchanga laini,na tandaza majani laini au pamba juu ya mchanga.
  8. Chukua mayai,yapange ndani ya viota hivyo (mayai 12 kila kiota)
  9. Chukua kuku wale 10,wapange katika viota hivyo. Yai moja kila kuku waliokuwa nayo,yatupe.
  10. Kwenye chumba hicho,weka vyombo vya maji na maji,vyombo vya chakula (chenye mchangayiko mzuri),pia usisahau kuweka dawa ya kuzuia wadudu (viroboto,utitiri nk)
  11. Baada ya siku 21, mayai yataanguliwa (90%-98%). Wanyanganye kuku vifaranga vyote,na vihamishie kwenye artificial brooder (sehemu ya joto ya kukuzia vifaranga). Wakati unaondoa vifaranga,rudishia mayai mengine kwa idadi ile ile na kuku walewale.
  12. Nashauri ufanye mizunguko ya aina hiyo 3,ndo uwapumzishe kuku au kubadilisha wengine.
  13. Kwa hesabu rahisi, kuku 10 @ vifaranga 12 = vifaranga 120 (siku 21), na ukirudia ni vifaranga 240 (siku 42) sawa na vifaranga 362 (siku 63=miezi 2). Hii ina maana kama utatumia kuku 20 kuatamisha, utakuwa na vifaranga 724 ndani ya miezi 2.
  14. Kama vifaranga hivi vitatunzwa vizuri (mada itakuja wiki ijayo) baada ya miezi 2 ya kukua, kwa bei ya soko ni Tsh 3,000/= kwa kifaranga kimoja x 724 (endapo hakuna vifo) = 2,172,000/=
  15. Kwa kuku wa kienyeji ambao kwa sehemu kubwa hawahitaji gharama kubwa ya chakula na madawa 25-30% ni gharama za madawa na chakula cha ziada.
  16. Ukifanya tahmini utagundua kuna faida kubwa. Karibuni tupunguze au kuondoa kabisa umasikini wa kipato
 
Sijaelewa kitu hapo.. Ina maana KUKU baada ya siku 21 anaendelea kuatamia mayai mengine bila kuchoka??? Duh mm nilijuwa akimaliza kutotoa nimpaka atage tena na ndy atamie tena .Hebu nielimishe hapo
Ndiyo,ataendelea kuatamia!
Hawatachoka kwa vile wanapata chakula bora na maji. Pia usisahau kunyunyizia dawa za kuuwa wadudu kama viroboto na utitiri ambao ni visumbufu vikubwa vya kuku wanapoatamia.
 
Mkuu bandiko lako ni zuri ila naomba niongeze nyama kidogo tu...
Hakikisha mayai yako yote unayaandika tarehe. Kumbuka mayai ya kuangua/ kutotolewa hayapaswi kukaa zaidi ya wiki mbili bila kuatamiwa.
Halafu kingine kwanini haya mayai 10 yaliyolaliwa na wale kuku kumi yote uyatupe?! Utaratibu mzuri ni kuwawekea mayai visa wakati wa kusubili idadi kamili itimie.
Halafu kumbuka sio kuku wote hawana uwezo wa kutambua yai viza au watakubali kuatamia yai moja tu.
Jitahidi uchague kuku wanaoendana na huu utaratibu.
Kiujumla mbinu yako ni nzuri.
 
Kwa wale wafugaji wa kuku wa kienyeji na wasio na uwezo wa kupata artificial incubators,fuata njia hii kutotolesha vifaranga vingi katika kipindi kifupi.
  1. Uwe na majike kadhaa wanaotaga (mfano 40)
  2. kusanya mayai yatakayotagwa ndani ya wiki 2 (yatunze vizuri yasiharibike)
  3. Kawaida kuku wa kienyeji hutaga mayai 12-14 kabla ya kupumzika kutaga (kutaka kuatamia)
  4. Kuku atakaenyesha dalili za kutaka kuatamia katika kundi,mwekee yai moja aatamie
  5. Endelea vivyohivyo kwa kuku watakaoonyesha kuatamia hadi watakapofikia idadi kuku 10
  6. Andaa chumba kizuri chenye mwanga,kisafi na nafasi ya kutosha kukaa kuku 10 bila kubanana
  7. Katika chuma hicho,weka viota (nests) 10- unaweza kutumia boksi ndogo,tia mchanga laini,na tandaza majani laini au pamba juu ya mchanga.
  8. Chukua mayai,yapange ndani ya viota hivyo (mayai 12 kila kiota)
  9. Chukua kuku wale 10,wapange katika viota hivyo. Yai moja kila kuku waliokuwa nayo,yatupe.
  10. Kwenye chumba hicho,weka vyombo vya maji na maji,vyombo vya chakula (chenye mchangayiko mzuri),pia usisahau kuweka dawa ya kuzuia wadudu (viroboto,utitiri nk)
  11. Baada ya siku 21,mayai yataanguliwa (90%-98%). Wanyanganye kuku vifaranga vyote,na vihamishie kwenye artificial brooder (sehemu ya joto ya kukuzia vifaranga). Wakati unaondoa vifaranga,rudishia mayai mengine kwa idadi ile ile,na kuku walewale.
  12. Nashauri ufanye mizunguko ya aina hiyo 3,ndo uwapumzishe kuku au kubadilisha wengine.
  13. Kwa hesabu rahisi,kuku 10 @ vifaranga 12 = vifaranga 120 (siku 21), na ukirudia ni vifaranga 240 (siku 42) sawa na vifaranga 362 (siku 63=miezi 2). Hii ina maana kama utatumia kuku 20 kuatamisha,utakuwa na vifaranga 724 ndani ya miezi 2.
  14. Kama vifaranga hivi vitatunzwa vizuri (mada itakuja wiki ijayo) baada ya miezi 2 ya kukua,kwa bei ya soko ni Tsh 3,000/= kwa kifaranga kimoja x 724 (endapo hakuna vifo) = 2,172,000/=.
  15. Kwa kuku wa kienyeji ambao kwa sehemu kubwa hawahitaji gharama kubwa ya chakula na madawa 25-30% ni gharama za madawa na chakula cha ziada. Ukifanya tahmini utagundua kuna faida kubwa. Karibuni tupunguze au kuondoa kabisa umasikini wa kipato
Mkuu asante kwa mada nzuri ya ujasiria mali
 
Nimependa mada yko ni nzuri.samahani ninafuga kuku wa kienyeji lakini si kwa ajili ya biashara ni kwa ajili ya kitoweo hapa nyumbani.nimeazimwa jogoo hii mbegu kubwa ya malawi.sasa mwenye jogoo analihitaji jogoo lake .nimekaa nalo siku nane je nitakuwa nimepata mbegu?
 
Mkuu bandiko lako ni zuri ila naomba niongeze nyama kidogo tu...
Hakikisha mayai yako yote unayaandika tarehe. Kumbuka mayai ya kuangua/ kutotolewa hayapaswi kukaa zaidi ya wiki mbili bila kuatamiwa.
Halafu kingine kwanini haya mayai 10 yaliyolaliwa na wale kuku kumi yote uyatupe?! Utaratibu mzuri ni kuwawekea mayai visa wakati wa kusubili idadi kamili itimie.
Halafu kumbuka sio kuku wote hawana uwezo wa kutambua yai viza au watakubali kuatamia yai moja tu.
Jitahidi uchague kuku wanaoendana na huu utaratibu.
Kiujumla mbinu yako ni nzuri.
Asante,yai viza nisawa,kwa maana nyingine hilo yai moja unaweza kulihifadhi kupunguza costs kwa next session .
 
Nimependa mada yko ni nzuri.samahani ninafuga kuku wa kienyeji lakini si kwa ajili ya biashara ni kwa ajili ya kitoweo hapa nyumbani.nimeazimwa jogoo hii mbegu kubwa ya malawi.sasa mwenye jogoo analihitaji jogoo lake .nimekaa nalo siku nane je nitakuwa nimepata mbegu?
Nimependa mada yko ni nzuri.samahani ninafuga kuku wa kienyeji lakini si kwa ajili ya biashara ni kwa ajili ya kitoweo hapa nyumbani.nimeazimwa jogoo hii mbegu kubwa ya malawi.sasa mwenye jogoo analihitaji jogoo lake .nimekaa nalo siku nane je nitakuwa nimepata mbegu?
Itategemea uliliweka kwenye majike mangapi,kama ni chini ya 20,kuna uwezekano ukapata mbegu(mayai yenye uwezo wa kuangulia). Kumbuka kuku anaweza kutaga bila kupandwa na jogoo! Hivyo kama kundi la majike lilikuwa kubwa zaidi ya 20 au 25,kuna uwezekano mayai mengine yakawa hayakuchavushwa(fertilized)
 
Usiseme hivyo mkuu wengine hayo maeneo ya kufugia hawana wamepanga vyumba
Mkuu wapo ambao wako kwao hasa vijijini wana maeneo. Shida kubwa wametekwa na mataputapu na viroba. MTU umelewa toka asubuhi utafuga kuku? Au madawa mjini utafuga? Tuombe Rehema kwa Mungu.
 
Itategemea uliliweka kwenye majike mangapi,kama ni chini ya 20,kuna uwezekano ukapata mbegu(mayai yenye uwezo wa kuangulia). Kumbuka kuku anaweza kutaga bila kupandwa na jogoo! Hivyo kama kundi la majike lilikuwa kubwa zaidi ya 20 au 25,kuna uwezekano mayai mengine yakawa hayakuchavushwa(fertilized)

Asante mkuu.mitetea ni sita tu.
 
Sawa kabisa mkuu. Kifaranga wa miezi 2 anauzwa 5000 huku Sengerema. Kama unao 100 ni sawa na 500,000. Aisee kuku wa kienyeji wanalipaaa ishu iko kwenye chakula tu. Ukiwamudu unajikwamua kabisaaa

Hali ya soko ikoje,kuna wateja wengi huko?
 
Hio njia yako mkuu ni nzuri sana ila nasikia inakondesha na kumdhoofisha sana kuku.
 
Sio kweli na nikutoe wasiwasi,nimeitumia sana. Kitakachofanya akonde ni pale atakapokosa chakula bora (chenye viini lishe vyote muhimu) na maji. Hivi ni vitu vya msingi sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom