Wakusolve
JF-Expert Member
- Jul 30, 2020
- 561
- 996
Njia rahisi ya kushinda uraibu(addiction) katika maisha yako.
Vijana wengi wanapoteza ndoto zao kwa kuingia kwenye uraibu wa vitu ambavyo sio sahihi kwenye maisha yao.
Uraibu kama wa picha au video za ngono, ulevi, matumizi ya sigara bangi, punyeto, ngono n.k
Uraibu huu unaweza kuua ndoto zako pia muda mwengine unaweza kusababisha matatizo ya kiafya, kupoteza fedha, mahusiano.
Mwili wako ni hekalu la Mungu hivyo matumizi yoyote ya uraibu utakuweka mbali na Mungu.
Njia za kutatua uraibu huu
Kwanza ni lazima uwe na nia ya kweli ya kutataka kuachana na uraibu wowote unao kusumbua.
Uraibu huu kuachana nao inaweza chukua muda lakini mikakati na nia thabiti itakufanya kushinda.
Anza kuacha kwa udogo, mfano unaweza kuacha matumizi ya uraibu huu mfano kuangalia video za ngono/picha , punyeto au bangi kwa wiki.
Ukifanikiwa wiki, unaenda tena bila matumizi wiki 2, unakuja mwezi, miezi 3 bila kuangalia picha hizo za ngono pia hii ni kwa aina yoyote kwa uraibu unaokusumbua iwe ulevi, pombe au bangi n.k
Unakuja miezi 6 na mwisho mwaka ukiweza hii akili yako itakuwa tayari imeachana na mawazo yanayokupelekea kwenye uraibu unaokusumbua na kufanikiwa kushinda.
Mambo ya msingi katika yote
Omba Mungu sana na kuwa na nia ya dhati, Mungu atakusaidia kushinda na utakuwa mtu mpya.
Pili achana na Mazingira au watu wanao kushawishi kuingia kwenye uraibu, ukiwa karibu na mazingira yenye ushawishi utapelekea akili yako kuona hilo jambo ni la kawaida
Mfano epuka group zinazo shawishi kufanya huo uraibu , nyimbo , picha au kitu chochote kinacho chaingia wewe upate hisia ya kufanya uraibu
Pia achana na watu au makundi, kuachana na watu sio dhambi watu wana asilimia kubwa ya kujenga au kuharibu tabia yako
Tatu, anza kufikilia kesho yako, jifunze vitu vipya, unapokuwa bize kujifunza vitu sahihi kama ujuzi, waza kuhusu uwekezaji hii itakusaidia kuepuka pesa kupotea kwenye ulevi.
Unapokuwa na kitu cha kufanya basi itakuepusha na huo uraibu kama ngono, picha za ngono, punyeto, bangi n.k
Kama kijana tambua umri wako ndio umri sahihi wa kujenga kesho yako epuka uraibu wowote maana unapoteza nguvu zako na muda pia.
Kijana ukitaka kujua uwezo wako achana na uraibu, Mungu kakuumba kuwa mtu mkuu, unashindwa kutambua uwezo wako sababu ya uraibu, utakapo jitambua ndipo utakapoona uwezo wako.
Kwa kijana ambaye hatumii uraibu wowote katika maisha yake anakuwa na nguvu kubwa na akili yake inakuwa na utulivu hivyo inapelekea ata vitu anavyofanya vinakuwa vina mafanikio sababu akili tulivu ina zalisha ubunifu mkubwa.