Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 287
- 601
KanKanuni ya Kwanza
Kutojihurumia
Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
— 1 Wakorintho 9:27
Watu wengi ambao wamekuwa na tabia za kujirudiarudia au uraibu wa kitu fulani, wamekuwa na tabia ya kujionea huruma.
Kuna mtu anasema hawezi kulala bila kunywa kidogo, au mwingine anasema hawezi kujizuia kutokuwa na mwanamke, na vitu kama hivyo.
Tukumbuke kwamba nia ya mwili siku zote ni kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu.
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu; kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
— Warumi 8:7
Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
— Warumi 8:8
Siku zote, tukiishi kwa kutii mapenzi ya mwili, mara zote tutakuwa chini ya kifungo cha uasi au kifungo cha dhambi.
Ili Mungu aweze kutusaidia, lazima tujionyeshe kuwa tunauhitaji msaada wa Mungu kwa kujutia kile tunachokifanya na kuonyesha tunautaka msaada.
Kutojionea huruma ni kukataa mazingira yoyote ambayo yanaweza kukuzamisha katika uraibu wa aina yoyote.
Mtume Paulo anasema yeye mwenyewe alikuwa anautiisha mwili wake, kama vile wanamichezo wanavyofanya mazoezi ya mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha mwili unakuwa timamu kwa ajili ya michezo. Kadhalika na sisi pia.
Ni kweli una uraibu wa pombe — kwanini unakwenda baa? Ukiwa na udhaifu katika pombe, badilisha ratiba zako. Badala ya kutembelea maeneo ya klabu, unaweza kujiunga na vikundi mbalimbali kama vile kwaya, maeneo ya mazoezi, ukafanya jogging n.k.
Una udhaifu kwa wanawake/wanaume? Jiweke malengo ya kufanya au kutekeleza ili kuuweka mwili wako busy. Unaweza kuwa na malengo ya kuwa mzazi bora kwa kuhakikisha kuwa haumsaliti mwenzako.
Unasumbuliwa na masterbation? Jifanyishe mazoezi. Kama ukiwa kwenye basi na umebanwa na haja kubwa, hauwezi kujisaidia popote tu hadi ufike sehemu salama. Kwanini usitumie mbinu hiyo ya kujizuia?
Badilisha fikra zako. Ondoa msamiati wa "haiwezekani", weka "inawezekana". Badilisha ratiba zako. Hakikisha unautumia vizuri muda wako wa mapumziko.
Kama umekuwa ukitumia simu kutazama vitu vinavyoweza kukuingiza katika uraibu wa aina yoyote, badilisha matumizi. Badala ya kutazama video zenye vichocheo vya uraibu wa kingono n.k., unaweza kuingia kwenye video za Neno la Mungu, za kwaya, au video zenye mafundisho ambazo zitakujenga.