Wakuu heshima kwenu,
Jana mida ya jioni nilienda kumpokea mgeni Ubungo, kama vile mjuavyo ukiwa na gari binafsi ni vigumu kuingia Ubungo ukiwa unatokea Posta, ikanilazimu nipite Shekilango yaani nizunguke lego alafu nije kutokea barabara ya Sam nujoma.
Nikaanza safari ya Ubungo, bahati nzuri nikiwa nakaribia ukuta wa Ubungo termninal nikaona geti kubwa pembeni mpiga debe kaniambia bro unaweza ingia kwa huku nyuma pia.
Kitu ambacho nilikuwa nakiomba mara kwa mara kiweze kutokea. Yaani kuwepo na geti la pili la kuingia na kutoka magari madogo kuondoa msongamano usio na tija.
Asante kwa mamlaka husika, ingawa bado uboreshaji unahitajika. Kumalizia naomba ile barabara irekebishwe kidogo jamani mamlaka husika tafadhali hebu lifanyieni kazi hili maana usawa wa ule mto kuelekea kwenye lile daraja kuna siku gari itatumbukia mtoni kwa ule mmomonyoko wa udongo.
Asanteni.