Njia rahisi kurudisha mafaili yaliyofichwa na virusi kwenye flash au External hard disk

Joeli

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
4,941
3,402
ishawahi kukutokea umeweka flash au external hard disk kwenye kompyuta na pale pale mafaili na mafolda yote yakageuka shortcut au yakapotea kabisa,

kuna njia rahisi (kwa watumiaji wa windows 7 na kuendelea) ambayo itasaidia kurudisha mafaili yako pamoja na mafolda yaliyokuwemo ndani ya flash au hard disk yako.

1. chomeka flash/external hd yako kwenye pc yenye antivirus iliyo uptodate kisha scan flash yako ili kuondoa virusi

2. nenda kwenye Control Panel > Folder Options > chagua VIEW tab, chagua “Show hidden files, folders and drives” pia uncheck “Hide protected operating system files (recommended)” ukimaliza bofya APPLY
winext-vista.gif



3. Fungua command prompt ( au bofya kitufe chenye alama ya window na R kwa pamoja, kisha andika CMD halafu enter)
labda tuseme flash au external yako inasomeka kama drive J:
sasa pale kwenye cmd andika maneno yafuatayo
Code:
attrib -h -r -s /s /d J:\*.*
kama yalivyo, usisahau iyo F ni herufi ya drive yako
attrib+command.jpg

ukimaliza bofya enter kisha tulia, baada ya muda mchache utaona kila kitu kimeonekana.


NB: izo alama zinamaana zifuatazo
"-"= ondoa attribute/permition,
h=hidden
s=system
r=read-only
a=archive
/s=sub directory
/d=directory,
drive_letter= herufi ya drive inavyoonekana kwenye windows explorer (mfano. j:,h: or D:) na
*.* inaitwa wild card.
 
Back
Top Bottom