Njia Kuu 4 za kutengeneza Pesa

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,381
1,414
Kuna njia kuu nne za kutengeneza pesa, kutoa muda wako kwa ajili ya pesa, kutoa taarifa ili kupata pesa, kutoa bidhaa au huduma kwa ajili ya pesa na kuweka kitu au mtu kufanya kazi kwa niaba yako na ukapata pesa.

Njia ya kutoa muda wako ili kupata pesa ni njia inayotumika unapoajiriwa, utakuwa unalipwa kulingana na muda wako. Changamoto kwenye njia hii ni muda, mapato yako yanategemeana na muda wako hivyo inakuwa ngumu kutajirika kwa njia hii au kuwa na kipato kikubwa kuliko mwajiri wako. Hakuna tatizo na ajira, ni afadhali kuwa kwenye ajira kuliko kutokufanya chochote.

Njia nyingine ni kutoa taarifa ili kupata pesa. Kila mtu anafahamu kitu ambacho hakuna mwingine anakifahamu, hivyo tuseme unafahamu martial art (mchezo wa ngumi) au chochote kile, unaweza ukafundisha watu kwa njia ya video, kuandika kitabu na ukauza na ukapiga pesa. Uzuri wa njia hii, muda wako hauhusiki, ukishaandika kitabu mara moja au ukitengeneza video mara moja huna haja ya kutengeneza tena wewe utakuwa unauza tu mpaka unaingia kaburini, na njia hii ni moja wapo ya njia itakayo kuwezesha kupiga pesa nyingi sana. Hivyo tafuta kitu unachokifahamu kisha kitoe kwa watu.

Njia nyingine ni kutoa bidhaa au huduma ili kupata pesa. Kwa mfano unatoa huduma ya matengenezo ya magari, badala ya wewe kuniuzia taarifa ili nijifunze mwenyewe kufanya marekebisho kwenye gari langu, wewe unanitengenezea halafu mimi nakulipa, hivyo njia hii haina utofauti sana na njia ya kwanza ya muda.

Njia ya nne ni kufanya kitu au mtu au watu kukufanyia kazi, watatoa muda wao nawe utawalipa mshahara, njia hii inakuhitaji uwe na kipato kikubwa na utahitaji kuwasimamia ila utapata muda wa kuwa huru kufanya mambo yako mengine.

Let's grow together!
 
Back
Top Bottom