Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,429
Hapo kunakuwa na checks and bbalance nyingi sana mkuu ambapo mtu hawezi akaruka stage zote hizo ispokuwa ndie mtu sahihi na smart kuliko wenzake.Mleta mada una mapendekezo ya msingi, lakini hapo namba 4 wao kwenda kuthibitishwa bungeni. Waende kudhibitishwa kwenye bunge hili hili ambalo zaidi ya 50% wameingia kwa maagizo ya rais kwenye uchaguzi ulionajisiwa? Hakuna uwezekano wa kupata viongozi stahiki nchi hii, huku viongozi wakubwa kabisa wanapatikana kwa wizi wa kura.
Unakusudia nini mkuu?MCC unafikiri watakubali?
Uko sahihi kabisa mkuu, na hii pia itapunguza 'populism politics' uchochezi, unafiki, kujipendekeza, watu kulia lia na.k.Ni wazo jema, na linaweza kuboreshwa zaidi ili ku-fit uhitaji wake na ngazi tofati za uongozi zitakazohusika kwenye mchakato wa aina hii...
Kumbuka majina yatakayoenda bungeni chini ya utaratibu huo, ni yake tu ambayo tayari yana sifa tu, na walioyachuja ni wataalam kwa kutumia vigezo vitakavyowekwa.Ushauri mzuri ila hapo kwenye kupelekwa huko bungeni sio sawa maana mzunguko umeurudisha tena kisiasa.
Na mbaya zaidi kwa bunge letu ambapo alieishia la nne B anaweza kuwa mbunge sasa hawa wanaweza wakawa ndio wengi halafu wakampigia kura ya hapanaaa mtalaamu wa Nuclear bila sababu ya maana.
Ukitumia recruiting agencies zinaweza kuhongwa au kununuliwa. Ukitumia za kimataifa zinaweza kupenyeza interest za magenge ya nchi nyingine, kwa hiyo ni hatari.Wala hakuna haja ya majina kwenda kupigiwa kura sioni nadharia yake yapo makampuni ya recruitment ya kimataifa yafanye vyote kuanzia interview na process zote ila wapeleke majina matatu then ndo Rais ateue mmoja bhasi ukisema mambo ya Bungeni tena itakuwa ni kupoteza Muda na Bunge lenyewe wakijua huyu ni kada wa CCM si watampigia kura yeye?
Uongozi ni kipaji + utashi + ujuzi + elimu + busara + uadilifu.Uongozi ni utashi wala si cheti cha kisomo.
Uongozi ni kipaji.
Uongozi ni utendaji na usimamizi.
Ukiweka wasomi wote kwenye uongozi jua hapo utendaji utakuwa 50%
Hapo kwenye uwiano wa kijinsia ndio umeharibu.1. Nafasi za kazi za kitaalam zitangazwe, sifa zinazoendana na aina ya kazi husika ziainishwe, na kila anayedhani ana sifa aombe.
2. Mchujo ufanywe na jopo maalum lenye mchanganyiko wa wataalam mbalimbali. Wenye sifa wote waende hatua inayofuata...
Hata kama ni majina 3 yamepelekwa huko bungeni lakini kuna mmoja ni bora zaidi. Lakini kwa tabia za wanasiasa wanaweza kumkataa bora zaidi sababu za interest zao tu na ukakosa kiongozi bora na mwenye uwezo wa ajabu kama ulivyosema.Kumbuka majina yatakayoenda bungeni chini ya utaratibu huo, ni yake tu ambayo tayari yana sifa tu, na walioyachuja ni wataalam kwa kutumia vigezo vitakavyowekwa...