Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
1. Nafasi za kazi za kitaalam zitangazwe, sifa zinazoendana na aina ya kazi husika ziainishwe, na kila anayedhani ana sifa aombe.
2. Mchujo ufanywe na jopo maalum lenye mchanganyiko wa wataalam mbalimbali. Wenye sifa wote waende hatua inayofuata.
3. Ufanyike usaili wa kujieleza ambao utarushwa live kwenye media mbalimbali ambapo wasailiwa watatakiwa waeleze namna wanavyoweza kutatua changamoto fulani zinazohusiana na nafasi wanayoomba huku wakiulizwa maswali magumu na jopo la wataalam. Watakaopata zaidi ya alama flani zitakazowekwa wanaenda hatua inayofuata.
4. Majina ya waliofuzu hatua ya 3 hapo juu yapelekwe bungeni na wapigiwe kura za ndio na hapana na wabunge, na watakaopata zaidi ya 70℅ ya kura za wabunge, majina yao yanaenda kwenye hatua ya uteuzi sasa
5. Mamlaka ya uteuzi inateua majina kulingana na idadi ya nafasi zilizopo kwa mujibu wa mamlaka itakavyoona inafaa kutoka kwenye majina yaliyofuzu hatua ya (4) hapo juu.
Kwa kufanya hivyo tutapata viongozi wenye competence isiyo ya kawaida, wanaopatikana kwa sifa, cream & very smart, randomly na hivyo kukidhi standards kama vile kuwa na uwiano wa kijinsia na.k
======
Huu ni ushauri tu kama ukionekana unafaa na unaweza kuwa na manufaa kwa ustawi wa nchi yetu.
==========