Njia inayoweza kutupatia viongozi bora na wenye uwezo wa ajabu

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
1. Nafasi za kazi za kitaalam zitangazwe, sifa zinazoendana na aina ya kazi husika ziainishwe, na kila anayedhani ana sifa aombe.

2. Mchujo ufanywe na jopo maalum lenye mchanganyiko wa wataalam mbalimbali. Wenye sifa wote waende hatua inayofuata.

3. Ufanyike usaili wa kujieleza ambao utarushwa live kwenye media mbalimbali ambapo wasailiwa watatakiwa waeleze namna wanavyoweza kutatua changamoto fulani zinazohusiana na nafasi wanayoomba huku wakiulizwa maswali magumu na jopo la wataalam. Watakaopata zaidi ya alama flani zitakazowekwa wanaenda hatua inayofuata.

4. Majina ya waliofuzu hatua ya 3 hapo juu yapelekwe bungeni na wapigiwe kura za ndio na hapana na wabunge, na watakaopata zaidi ya 70℅ ya kura za wabunge, majina yao yanaenda kwenye hatua ya uteuzi sasa

5. Mamlaka ya uteuzi inateua majina kulingana na idadi ya nafasi zilizopo kwa mujibu wa mamlaka itakavyoona inafaa kutoka kwenye majina yaliyofuzu hatua ya (4) hapo juu.

Kwa kufanya hivyo tutapata viongozi wenye competence isiyo ya kawaida, wanaopatikana kwa sifa, cream & very smart, randomly na hivyo kukidhi standards kama vile kuwa na uwiano wa kijinsia na.k

======
Huu ni ushauri tu kama ukionekana unafaa na unaweza kuwa na manufaa kwa ustawi wa nchi yetu.
==========
 
Ni wazo jema, na linaweza kuboreshwa zaidi ili ku-fit uhitaji wake na ngazi tofati za uongozi zitakazohusika kwenye mchakato wa aina hii.

Nadhani kabla ya hapo, kuna suala la kubadili sheria/policy zilivyo kwa sasa ili ziendane na mktadha uliouelezea.

Kwa wanaoitakia mema nchi na wazalendo wa kweli, wataona mantiki. Wachumia tumbo na wanaopenda uongozi na madaraka kufuata mnyororo wa uko huu ni mwiba mkali.

Hapa ndo huwa nawaza watu walioko kwenye think tank section. Kwa nini wasitoe nafasi ya wataalamu mbalimbali kuwapa maoni yao unbiased then wao bila bias pia kuyafanyia kazi na kuons jinsi gani mawazo hayo yanaweza kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo y nchi yetu. Kama mtu ana mawazo kuhusu sekta ya afya, sheria, miundombinu , uwekezaji nk. Waweke link ili wapate mawazo kisekta.
 
Mleta mada una mapendekezo ya msingi, lakini hapo namba 4 wao kwenda kuthibitishwa bungeni. Waende kudhibitishwa kwenye bunge hili hili ambalo zaidi ya 50% wameingia kwa maagizo ya rais kwenye uchaguzi ulionajisiwa?

Hakuna uwezekano wa kupata viongozi stahiki nchi hii, huku viongozi wakubwa kabisa wanapatikana kwa wizi wa kura.
 
Kwa checks & balance ya level hiyo, kweli tutapata viongozi very inteligent & effective na kila mtu atafurahi kitakachotokea
 
Mleta mada una mapendekezo ya msingi, lakini hapo namba 4 wao kwenda kuthibitishwa bungeni. Waende kudhibitishwa kwenye bunge hili hili ambalo zaidi ya 50% wameingia kwa maagizo ya rais kwenye uchaguzi ulionajisiwa? Hakuna uwezekano wa kupata viongozi stahiki nchi hii, huku viongozi wakubwa kabisa wanapatikana kwa wizi wa kura.
Hapo kunakuwa na checks and bbalance nyingi sana mkuu ambapo mtu hawezi akaruka stage zote hizo ispokuwa ndie mtu sahihi na smart kuliko wenzake.

Hapo kama mtu ana makandokando, lazima kwenye stage flani atatemwa tu.
 
Ni wazo jema, na linaweza kuboreshwa zaidi ili ku-fit uhitaji wake na ngazi tofati za uongozi zitakazohusika kwenye mchakato wa aina hii...
Uko sahihi kabisa mkuu, na hii pia itapunguza 'populism politics' uchochezi, unafiki, kujipendekeza, watu kulia lia na.k.

Kwa lugha nyingine sio tu kwamba watapatikana viongozi smart bali pia haki itakuwa imetendeka mchana kweupeee na kila mtu ataona kwa jicho lake inavyotendeka.

Hali hii itajenga mshikamano na kuaminiana kwa hali ya juu ambapo katika hatua yake ya juu kabisa, tutajenga taifa ambalo watu wake wana uzalendo wa ajabu na morali wa kufanya kazi kwa kujituma isivyo kawaida badala ya kutegemea kufanikiwa kibahati nasibu.
 
Ushauri mzuri ila hapo kwenye kupelekwa huko bungeni sio sawa maana mzunguko umeurudisha tena kisiasa.

Na mbaya zaidi kwa bunge letu ambapo alieishia la nne B anaweza kuwa mbunge sasa hawa wanaweza wakawa ndio wengi halafu wakampigia kura ya hapanaaa mtalaamu wa Nuclear bila sababu ya maana.
 
Ushauri mzuri ila hapo kwenye kupelekwa huko bungeni sio sawa maana mzunguko umeurudisha tena kisiasa.

Na mbaya zaidi kwa bunge letu ambapo alieishia la nne B anaweza kuwa mbunge sasa hawa wanaweza wakawa ndio wengi halafu wakampigia kura ya hapanaaa mtalaamu wa Nuclear bila sababu ya maana.
Kumbuka majina yatakayoenda bungeni chini ya utaratibu huo, ni yake tu ambayo tayari yana sifa tu, na walioyachuja ni wataalam kwa kutumia vigezo vitakavyowekwa.

Huwezi kuwakwepa wanasiasa kwa sababu mwisho wa siku wao ndio viongozi wa juu. Kwa hiyo la muhimu ni checks and balance.
 
Wala hakuna haja ya majina kwenda kupigiwa kura sioni nadharia yake yapo makampuni ya recruitment ya kimataifa yafanye vyote kuanzia interview na process zote ila wapeleke majina matatu then ndo Rais ateue mmoja bhasi ukisema mambo ya Bungeni tena itakuwa ni kupoteza Muda na Bunge lenyewe wakijua huyu ni kada wa CCM si watampigia kura yeye?
 
Wala hakuna haja ya majina kwenda kupigiwa kura sioni nadharia yake yapo makampuni ya recruitment ya kimataifa yafanye vyote kuanzia interview na process zote ila wapeleke majina matatu then ndo Rais ateue mmoja bhasi ukisema mambo ya Bungeni tena itakuwa ni kupoteza Muda na Bunge lenyewe wakijua huyu ni kada wa CCM si watampigia kura yeye?
Ukitumia recruiting agencies zinaweza kuhongwa au kununuliwa. Ukitumia za kimataifa zinaweza kupenyeza interest za magenge ya nchi nyingine, kwa hiyo ni hatari.

Kumbuka suala senstive kama hilo likifanywa na kampuni au watu wacheche bila checks and balance, hiyo source inaweza ama kwa bahati mbaya au kwa malengo maalum ( ya msingi au yasiyo ya msingi) ikafanya kitu kisicho cha kawaida.

Ndio maana checks nyingi nyingi ni muhimu.
 
Uongozi ni utashi wala si cheti cha kisomo.

Uongozi ni kipaji.

Uongozi ni utendaji na usimamizi.

Ukiweka wasomi wote kwenye uongozi jua hapo utendaji utakuwa 50%
 
Uongozi ni utashi wala si cheti cha kisomo.

Uongozi ni kipaji.

Uongozi ni utendaji na usimamizi.

Ukiweka wasomi wote kwenye uongozi jua hapo utendaji utakuwa 50%
Uongozi ni kipaji + utashi + ujuzi + elimu + busara + uadilifu.

Kupitia hatua za kwenye uzi wa msingi, vyote hivyo vinaweza kupimwa kikamilifu.
 
1. Nafasi za kazi za kitaalam zitangazwe, sifa zinazoendana na aina ya kazi husika ziainishwe, na kila anayedhani ana sifa aombe.

2. Mchujo ufanywe na jopo maalum lenye mchanganyiko wa wataalam mbalimbali. Wenye sifa wote waende hatua inayofuata...
Hapo kwenye uwiano wa kijinsia ndio umeharibu.

Sasa kati ya hao watatu wakiwa wanaume wote itabidi umuache mmoja ili umchomeke mwanamke mmoja?
 
Kumbuka majina yatakayoenda bungeni chini ya utaratibu huo, ni yake tu ambayo tayari yana sifa tu, na walioyachuja ni wataalam kwa kutumia vigezo vitakavyowekwa...
Hata kama ni majina 3 yamepelekwa huko bungeni lakini kuna mmoja ni bora zaidi. Lakini kwa tabia za wanasiasa wanaweza kumkataa bora zaidi sababu za interest zao tu na ukakosa kiongozi bora na mwenye uwezo wa ajabu kama ulivyosema.

Wanasiasa wapelekewe jina tu kuwa ndio huyu mtalaamu na Mtalaamu awahutubie tu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom