Njia gani naweza kutumia kuhifadhi mafuta ya alizeti?

Jun 5, 2022
78
115
Je, mafuta ya alizeti nikinunua na kuyahifadhi kwenye madumu Yale ya Lita 20 ndani ya mwaka mmoja, mafuta yanaweza kukaa bila kupoteza ubora wake?

Pia njia zipi nyingine ambazo naweza kuzitumia kuhifadhi mafuta ya alizeti ndani ya mwaka mmoja bila kuharibika?

Naombeni ushauri wenu wazoefu na wataalamu wa mafuta ya alizeti .

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu waungwana asanteni Sana
 
Je, mafuta ya alizeti nikinunua na kuyahifadhi kwenye madumu Yale ya Lita 20 ndani ya mwaka mmoja , mafuta yanaweza kukaa bila kupoteza ubora wake?

Pia njia zipi zingine ambazo naweza kuzitumia kuhifadhi mafuta ya alizeti ndani ya mwaka mmoja bila kuharibika?

Naombeni ushauri wenu wazoefu na wataalamu wa mafuta ya alizeti .

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu waungwana asanteni Sana
Noted.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Je, mafuta ya alizeti nikinunua na kuyahifadhi kwenye madumu Yale ya Lita 20 ndani ya mwaka mmoja , mafuta yanaweza kukaa bila kupoteza ubora wake?

Pia njia zipi zingine ambazo naweza kuzitumia kuhifadhi mafuta ya alizeti ndani ya mwaka mmoja bila kuharibika?

Naombeni ushauri wenu wazoefu na wataalamu wa mafuta ya alizeti .

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu waungwana asanteni Sana
Hayaharibiki lakini hakikisha dumu la kihifadhia limekauka vzr...ni vzr kuweka mafuta kuliko alizeti kuepuka changamoto za wadudu na kunywea kwa alizeti.
 
Tunapotoa ushauri ni bora tukawa na uhakika na utaalamu wa tunachoshauri, kuna mtu anasema hayatoharibika, ni upotoshaji mkubwa sana. Ukweli ni kuwa ni lazima yatapoteza ubora wake na kutengeneza harufu, inatakiwa uondoe hewa yote ya oksijeni kwenye mafuta kabla ya kuyahifadhi kuzuia oxidation reaction.

Ili kufanikisha hilo inabidi uyachemshe kwa usahihi kabisa kwa kuongeza maji kiasi na chumvi kidogo. Chumvi ina lower boiling point ya mafuta ili yachemke kwa wepesi na maji yanapogeuka mvuke uondoka na hewa yote ya oksijeni iliyoko kwenye mafuta. Fanya hivyo kisha yahifadhi na yatakuwa salama. Nikipata muda nitakupa details zaidi ila hii ndiyo njia sahihi
 
Tunapotoa ushauri ni bora tukawa na uhakika na utaalamu wa tunachoshauri, kuna mtu anasema hayatoharibika, ni upotoshaji mkubwa sana. Ukweli ni kuwa ni lazima yatapoteza ubora wake na kutengeneza harufu, inatakiwa uondoe hewa yote ya oksijeni kwenye mafuta kabla ya kuyahifadhi kuzuia oxidation reaction. Ili kufanikisha hilo inabidi uyachemshe kwa usahihi kabisa kwa kuongeza maji kiasi na chumvi kidogo. Chumvi ina lower boiling point ya mafuta ili yachemke kwa wepesi na maji yanapogeuka mvuke uondoka na hewa yote ya oksijeni iliyoko kwenye mafuta. Fanya hivyo kisha yahifadhi na yatakuwa salama. Nikipata muda nitakupa details zaidi ila hii ndiyo njia sahihi
Mfano mafuta lita 20 unatakiwa uweka chumvu na maji kiasi gani?
 
Sasa hapa sijui tushike lipi tuache lipi
Mkuu waweza shika lolote, ila pia waweza jisomea zaidi. Mafuta yakutoka viwandani yaliyochakatwa vyema yaweza kukaa hadi miaka miwili kama yatakuwa hayajafunguliwa. Haya tunayochakata mitaani ni muhimu kufanya kama nilivyoshauri kama utayatunza kwa zaidi ya miezi sita, vinginevyo ubora utapotea na yatatengeneza kaarufu (rancid. Tumezoea kuwa ili chakula kiharibike ni lazima usikie harufu kali, au rangi ibadilike au uone fangasi wameota n.k. Ila ukweli hayatokuwa salama kwa chakula. Adui wengine wa mafuta ni mwanga wa jua na unyevunyevu (moisture), mwanga wa jua upelekea mafuta kupoteza vitamin E kwa wepesi sana.
 
Mfano mafuta lita 20 unatakiwa uweka chumvu na maji kiasi gani?
Mkuu nitaomba baadaye nikupe jibu la uhakika, ila nakumbuka kwa kila lita mia tulikuwa tunaweka kilo moja ya chumvi na maji lita 5. Kumbuka mwisho wa mchakato maji yote yatakuwa yameisha kwani yanachemka kabla ya mafuta na kupotea kama mvuke, lengo ni kuondoa hewa ya oksijeni tu. Nina miaka 21 tangu nimeacha kufanya shughuli hii, nitakupatia formula halisi. Kama unayatumia ndani ya miezi sita hayana shida sana, zaidi ya hapo ni vyema kuyachakata vizuri.
 
Tupe madini
 
Kumbe kunautofauti Kati ya mafuta haya ya kukamuliwa mashineni na mafuta yanayo kamuliwa viwandani
Mafuta yakiwa processed viwandani yanapitia hatua zote muhimu kuyafanya salama na kuweza kuhifadhika kwa hadi miaka miwili. Kinachofanyika kwenye mashine zetu za mitaani ni kukamua, kuchuja na kuweka kwenye madumu, biashara inakuwa imekwisha. Hakuna process nyingine yoyote kuhakikishayanakuwa salama kwa muda mrefu (zaidi ya miezi sita). Na ndio maana nikatoa njia rahisi inayotumika kwa wakamuaji wadogo na wakati kuhakikisha usalama wa chakula (food safety).
 
Nimependa mada hii ngoja na Mimi niweke neno hapo mim ni mfanya kazi katika kiwanda kidogo Cha mafuta ya alizeti kipo kahama mjini sas sisi tuna kamua mafuta na kuchuja kisha tuna weke kwenye madumu makubwa na mdogo kwa kuuzwa sas nimjibu mtoa mada alizet ikiwa Ina kamuliwa kwenye mashine pale Kuna joto kilo pale ndomana mafuta machafu Yana Toka yamoto Kisha tunayachukiwa mafuta machafu tuna weka kwenye chujio pale na napo Kuna presha inayoivisha mafuta ambayo inauwa vijidudu vyote yakita apo miaka kumi hakuna alafu Wala kuganda angalizo chombo unachoweka mafuta kiwe kisafi
 
Back
Top Bottom