Njia ambazo dunia huenda ikafika mwisho wake

Njia ambazo dunia huenda ikafika mwisho wake

vivaforever

Senior Member
Joined
May 30, 2016
Posts
113
Reaction score
170
1) Vita ya Nyuklia (Nuclear Armagedon)

Bomu moja la Nyuklia lina uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 80 hadi 95 kutoka eneo lililoripuliwa kuelekea umbali wa kipenyo cha Km 4 ingawa uharibifu mkubwa unaweza fika mbali zaidi.

Ingawa watu wanahofia sana kifo kutokana na mlipuko wa mabomu haya lakini tunachotakiwa kuhofia zaidi ni Msimu wa Baridi wa Nyuklia ( Nuclear winter ). Hii ni pale wingu la vumbi zito na moshi unaotokana na hii milipuko kufunika anga la Dunia hivyo kuzuia miale ya jua kufika Duniani. Mimea itakufa, wanyama watakufa... baridi litakuwa kali sana maana joto litadondoka chini ya 0°C, vurugu zitasambaa kwa wale wachache watakaobakia wakigombania mahitaji machache yatakayokuwa yamebakia. Wengine watakufa kutokana na kudhuriwa (watapata Kansa za ajabu) na mionzi yenye sumu ya Nyuklia kutoka kwenye hayo mabomu au vinu vya Nyuklia vitakavyo ripuka.

Marekani na Urusi pekee wana zaidi ya vichwa 7000 vya nyuklia.. ikitokea vichwa 4000 tuu vimetumika kwenye hii vita basi Dunia ndo kwisha habari yake. Nchi nyinginezo zenye mabomu ya nyuklia ni kama vile India, Pakistan, Korea Kaskazini, Uingereza, Ufaransa n.k.



2) Silaha za Kibaiolojia & Kikemikali ( Biological and chemical warfare ).

Tofauti na siraha za Nyuklia ambazo ni ghali sana na ngumu kuzitengeneza pia huaribu majengo, kuua mimea, wanyama kiufupi huaribu chochote kilicho mbele yake... siraha za kibaiolojia & kikemikali huweza kutengenezwa kwa gharama ndogo sana ndani ya Maabara kwa kutumia malighafi ambazo ni rahisi sana kuzipata.

Ndani ya miongo michache tumeshuhudia matumizi ya vimelea hatari kama vile Kimeta vikitumiwa kufanya mashambulizi ya kibaiolojia pia gesi na kemikali zenye sumu kama vile Sarin ambazo hutumika sana vitani.

Jee! Hatari iko wapi..??
Ukitaka kujua hatari ilipo basi fikiria kuhusu Virusi vya Corona vya mwaka 2019 (SARS - nCOV - 2019) ambavyo vimeitesa na Dunia kwa mwaka mmoja uliopita. Kama virusi hatari vikibadirishwa maabara kuvifanya viwe hatari zaidi (Mfano: Ebola Virus, Measles Virus) halafu visambae kama vya Corona... vifo vingekuwa vingi sana na Dunia ingesimama kwa miongo kadhaa.
Kuhusu hizi gesi za Sumu & Kemikali kama zikiwa zimeachiwa kwenye Vyanzo vya maji (Mfano; Bahari) au Hewa... basi ingesambaa haraka sana mwishowe Dunia isingekalika na viumbe hai vingekufa ovyo.



3) Mabadiriko ya Tabia ya Nchi. (Climate change)

Mnalionaje jua la Bongo huko..?? [emoji23][emoji23] liendelee kuteremka au tupunzike kidogo..??

Umoja wa mataifa kupitia Jopo la wanasayansi wake wametoa tahadhari kuwa tuna miaka 12 tuu ili kurudisha Joto la Dunia katika kiwango sahihi (Optimum levels).

Mwendelezo wa mabadiriko ya tabia ya Nchi hutegemeana na jinsi Dunia inavyozidi kuchemka (warming) kutokana na kuongezeka kwa Joto.

Jee! Hatari iko wapi..?
○ Vimbunga vya Kitropiki vinavyoangamiza. Hivi mara nyingi hutokana na mabadiriko ya mgandamizo wa hewa na joto huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mvurugiko huo.
○ Kuzama kwa Majiji makuu. Mfano; Florida, Bangladesh, Dar-Es-Salaam hii ni kutokana na kuongezeka kwa Maji ndani ya Bahari (kumbuka: Kama bara lote la Antarctica ambalo limefunikwa na theluji tupu likiyeyuka basi sehemu kubwa sana ya Ardhi ya Dunia itazama chini ya Maji).
○ Kutanuka kwa Majangwa.

Hali hii itasababisha uhaba mkubwa wa chakula, watu kukosa makazi na magonjwa ya mlipuko yasiyoelezeka.




4) Kuanguka kwa mfumo wa Ikolojia (Ecological collapse).

Mfumo wa ikolojia ni mwepesi sana na hujumuisha jamii ya viumbe hai mbalimbali wanaoingiliana na mazingira yao ya asili (yasiyo hai) kama vile Maji, Hewa na Ardhi. Mfumo wa ikolojia huweza kupona kutoka kwenye uharibifu unaofanywa na Binadamu kama vile kuongezeka kwa Joto, uharibifu wa makazi ya viumbe hai n.k (angalia jinsi misitu inavyochipuka tena baada ya kukatwa) lakini kuna hatua flani ikifika haiwezi kupona tena na kutokana na ripoti mbalimbali za kisayansi ni kuwa tumefikia hatua hiyo.

Mfano mzuri ni Ziwa Chad lililopo Afrika Magharibi. Miaka 60 ya ukame na matumizi holela ya maji ya ziwa hilo imesababisha ziwa lipungue maji yake kwa Lake Chad in West Africa is an 90% kiasi kwamba viumbe hai na watu takribani milioni 40 kutoka Nchi za Chad, Nigeria, Niger na Cameroom wanaotegemea hilo ziwa wakiwa hatarini.

Wanasayansi wanaamini kwamba hiki kipindi katika Historia kinaunda wakati maalumu unaojulikana kama Anthropocene Era (Zama za Anthropocene). Katika zama hizi, Binadamu ndio waharibifu wakuu huku wakiwa wanaharibu kile kinachoifabya hii sayari iwe ya kukalika.

Jee! Hatari iko wapi..??
○Mimea na Wanyama mbalimbali wataendelea kuadimika na mwishowe kutoweka (from Endangered to Extinct). Lakini miongoni mwa viumbe hao ndio tunawategemea sana ili tuweze kuishi, Mfano: Nyuki, kama wakitoweka basi Dunia itaanza kufa taratibu.



5) Magonjwa ya kusambaa Dunia nzima. (Pandemics).

Wakati tukiwa tunalia na Corona, hebu tujikumbushe kuhusu Tauni (Plague), mara mbili katika Historia tauni ilienea Duniani huku ikiua kadirio la 15% ya watu wote Duniani miongo michache iliyopita. Ilitokea katika karne ya 14 na 15.

Kwa bahati sana ni kuwa haya magonjwa yenye uwezo wa kusambaa Dunia nzima ni adimu sana, lakini yanatokea. Karne moja iliyopita Mafua ya Uhispania (Spanish Flu) yaliua zaidi ya watu milioni 50 huku mlipuko wa Ebola na mafua ya SARS hivi karibuni ikiwa kama ukumbusho kwetu.

Jee! Hatari iko wapi..??
○ Usugu wa vimelea. Vimelea vingi vimekuwa sugu kiasi zile dawa zinazotumiwaga kuwaangamiza (Mfano; Antibiotics) hazina uwezo wa kufanya hivyo tena.
○ Kukosekana kwa Kinga na tiba dhidi ya Vimelea sugu. Baadhi ya magonjwa hayana tiba wala kinga, mfano; Ebola. Kama yatasambaa Dunia nzima basi vifo vitakuwa vingi sana.



6) Dunia kupigwa na Kimondo (Asteroid impact).

Vimondo ni mawe makubwa yanayoelea angani huku yakiwa yanalizunguka Jua. Ni mara chache sana haya mawe hugongana na Dunia kama vile ilivyotokea miaka mingi iliyopita na kusababisha kutoweka kwa viumbe aina ya Dinosaurs. Kama kimondo chenye ukubwa wa 1/10 ya ukubwa wa kimondo kilichoipiga Dunia na kusababisha kuangamia kwa Dinosaurs kikiipiga Dunia leo hii basi matokeo yake yatakuwa ni ya kuogofya.

Inaaminika kuwa kitatoa shock kubwa sana kiasi majengo yote yataporomoka, milipuko itaikumba Dunia nzima na Moshi mzito utatanda anga la Dunia kuzuia miale ya Jua kufika ardhini., Dunia itakuwa kama imepigwa na Vita ya Nyuklia.



7) (Mlipuko wa Volkano kuu) Supervolcanic eruption

Volkano kuu iliyoripuka miaka 74,000 iliyopita ilitoa kifusi kikubwa kilichoifunika Dunia kiasi kwamba wanasayansi wanaamini kilisababisha Dunia ipoe na kuwa na baridi kali kutokana na kukosa miale ya Jua. Hali hii ilipelekea kupotea kwa mimea na wanyama wa aina mbalimbali (great Mass extinction).

Jee! Hilo linaweza kutokea leo..?? Ni ngumu sana kusema kwa sababu hatuna data za kutosha lakini kwa kiasi flani zinaonyesha kuwa hii hali hutokea kila baada ya miaka 17,000... na kama ni hivyo basi tumepitiliza maana mara ya mwisho Volkano kuu kuripuka ni miaka 26,500 iliyopita huko New Zealand.

Hatuna njia za kugundua kuwa mripuko unakuja isipokuwa baada ya wiki au miezi kadhaa, na pia hatuna njia yoyote ya kuzuia hilo lisitokee, wanasayansi wanayachunguza kwa ukaribu maeneo machache ambayo ni hatarishi na huwenda Volkano kuu ikaanza kuripukia hapo.. mfano: eneo la Yellowstone huko Marekani.



8) Solar geoengineering

Kuna njia nyingi za kuzuia joto la Dunia lisipande lakini huja na hatari zake.

Solar geoengineering hii njia huakisi mwanga na joto la jua lisifikie Duniani na lipotelee kwenye Anga, hii hufanyika kwa kuweka "Aerosols" katika Stratosphere (tabaka la Pili la angahewa kutoka Ardhini). Kwa sasa hii Teknolojia ipo kwenye Models tuu (bado haijafanyika) lakini Wanasayansi wa Havard wana mpango wa kuanza kuifanyia majaribio.

Jee! Hatari yake ni ipi..??
Solar geoengineering ni moja kati ya Teknolojia mbili zinazochipuka ambazo zinaweza rekebisha anga hewa na kupunguza wingi wa hewa ya Ukaa (Carbondioxide), Teknolojia nyingine ni ile ya kuondoa hewa ya Ukaa moja kwa moja kutoka kwenye angahewa ingawa hii Teknolojia haiwezi ondoa hiyo hewa kwa uwingi. Sasa hii teknolojia ya Solar Geoengineering hatujui madhara yake yatakuwa ni yapi, huenda itavuruga mfumo wa ikolojia katika eneo maalumu au Dunia nzima na hapo ndipo tatizo lilipo... hii itaathiri Binadamu kwa kiwango kikubwa kwa kuanguka kwa mfumo wa Ikolojia.



9) Akili ya kubuni (Artificial intelligence).

Akili ya kubuni "Artificial intelligence (AI)" inaendelea kukua kwa haraka kila uchwao ambapo tunaona maroboti yenye uwezo wa kutenda kazi na kubuni vitu kwa ufanisi mkubwa kuliko Binadamu yakivumbuliwa kila siku. Wanasayansi wanakadiria kuwa ifikapo 2050 hawa Maroboti (au A.I) watakuwa na uwezo wa kutenda kwa ufanisi kwa 50% kuliko Binadamu wa kawaida... na miaka michache mbeleni watakuwa wamewapita Binadamu katika ufanisi wa kutenda kazi.

Tatizo liko wapi...??
Shida ni kuwa Wanasayansi wanaamini uwezo huo mkubwa wa kutenda kazi na kubuni vitu vipya kwa hawa Maroboti utamuweka Binadamu katika hatari ya kutawaliwa na hawa viumbe (Cheki movie ya I - ROBOT kama mfano) kwani wanaweza buni siraha hatarishi (A.I Weapons), kutenda kwa kufuata matakwa yao (kujiamulia) au kama wakiwa chini ya mtu mwenye malengo maovu wanaweza tenda kinyume na malengo ya kuundwa kwao (Cheki movie ya CHAPPIE kama mfano).



10) Hatari ambazo hatuzijui. (Unknown risks)

Ingawa miongo na karne kadhaa zilizopita stori za kuogofya kuhusu mwisho wa Dunia zilikuwa ni kuhusu Vita kuu ya Tatu ya Dunia na sababu nyinginezo ila hadi sasa kuna hatari nyingi sana zilizotuzunguka na hatujui itakuwaje hadi zitaleta Maangmizi Duniani.

SABABU ZA ZIADA:

01. Majaribio ya Kisayansi hatarishi.
MFANO;
● CERN's Large Hadron Collider.
● SETI experiments.
● Kola Superdeep Borehole.
● Nuclear Detonation Test (Majaribio ya mabomu ya Nyuklia).

02. Vitu hatarishi vya Angani.
MFANO;
● Mashimo meusi (Black holes) haya humeza chochote kilichopo ndani ya njia yake na kukifinyanga kuwa kama Tambi.. yana nguvu kiasi kwamba hata Mwanga hauwezi kuyahepuka. Galaxy letu lina mashimo meusi mengi sana na ni vigumu kujua pale linapokaribia.
● Gamma Rays Burst.
● Solar Flares.
● Supernovae.

03. Tabiri za Dini
MFANO;
● Kiama.
● Vita kuu za Kidini (Armageddon & Jihhads).

K A R I B U N I
IMG_20211113_091855_235.jpg
IMG_20211113_091859_221.jpg
IMG_20211113_091954_506.jpg
IMG_20211113_092114_440.jpg
IMG_20211113_092227_080.jpg
IMG_20211113_092615_697.jpg
IMG_20211113_092623_695.jpg
IMG_20211113_092829_781.jpg
IMG_20211113_092935_084.jpg
IMG_20211113_093055_352.jpg
IMG_20211113_093149_517.jpg
 
Katika sababu zote ulizotaja
Hakuna hata moja itakayofanya dunia itikisike achilia mbali kupotea kabisa isipokua namba 6

Labda kama una maanisha Human extinction
Na hatuwezi kuwa wajinga kiasi hiko kuruhusu hilo litokee

Nchi kubwa zina miliki silaha za Nuclear for defense purpose na sio kushambulia

Sisi na uchumi wetu mbovu, tukiwa na silaha za Nuclear na tukazitegesha kuelekea Miji mikubwa Marekani

Marekani wataishia tu kututisha tu kwa maneno, hawato thubutu kutupiga
See? Defense.

Hakuna nchi itakayo tumia tena silaha za Nuclear vitani, tumejifunza

Na hii ni nadra mno kutokea

Pia namba 9 sidhani kama inafaa kuwa ndani ya orodha.
A.I ni over hyped concept kwa sasa

Strong A.I yenye uwezo wa kuleta madhara kwa binadamu ni bado mno

Kwa sasa tuna weak A.I...ambazo ni Programs tu za computer zinazotumia statistics na probability ku predict na classify vitu

Ni math tu, sio nafsi
 
Dunia kama sayari itafikia mwisho wake pia pale itakapomezwa na Jua.

Inaelezwa kuwa, kuna wakati hapo baadaye Jua litapoteza thamani ama litamaliza muda wake wa 'kuishi' (expire) kisha litatanuka kupita kiasi na kuzimeza sayari za karibu yake [dunia ikiwemo].

Ila ni baadaye sana, hivyo haina haja ya kuhofia sana!

Katika suala la vita ya nyuklia, teknolojia ya kujikinga na silaha hizo nayo inazidi kufanyiwa kazi. Hapo zamani tulikuwa tukizungumzia sana kuhusu Mutual Assured Destruction (MAD) ila hivi sasa hii hoja inazidi kupoteza thamani.

Mfano: nuclear bunkers zinazotengenezwa hivi sasa kupitia mifumo ya kisasa ya tunneling zina uwezo wa kuhimili shambulio lolote lile la nyuklia wakati wowote. Bila kusahau mifumo inayoambatana na hiyo ikiwemo ABM defense systems.

Kutokana na hilo, msingi wa MAD unaweza kukosa nguvu kabisa hivyo kuiacha dunia ikiendelea ku-survive wakati huo mkiwa mmekwisha tumia silaha zenu zote kushambuliana.
 
Katika sababu zote ulizotaja
Hakuna hata moja itakayofanya dunia itikisike achilia mbali kupotea kabisa isipokua namba 6

Labda kama una maanisha Human extinction
Na hatuwezi kuwa wajinga kiasi hiko kuruhusu hilo litokee

Nchi kubwa zina miliki silaha za Nuclear for defense purpose na sio kushambulia

Sisi na uchumi wetu mbovu, tukiwa na silaha za Nuclear na tukazitegesha kuelekea Miji mikubwa Marekani

Marekani wataishia tu kututisha tu kwa maneno, hawato thubutu kutupiga
See? Defense.

Hakuna nchi itakayo tumia tena silaha za Nuclear vitani, tumejifunza

Na hii ni nadra mno kutokea

Pia namba 9 sidhani kama inafaa kuwa ndani ya orodha.
A.I ni over hyped concept kwa sasa

Strong A.I yenye uwezo wa kuleta madhara kwa binadamu ni bado mno

Kwa sasa tuna weak A.I...ambazo ni Programs tu za computer zinazotumia statistics na probability ku predict na classify vitu

Ni math tu, sio nafsi
Hiyo namba 01 usii-underestimate kabisa. Kumbuka Dunia ilitaka kuingia kwenye Vita ya Nyuklia si chini ya mara 3 kutokana na makosa ya kibinadamu tuu
Hii ilikuwa miaka ya 90 huko yaani ni bahati tuu ndio iliyotufanya tuwepo hadi hapa tulipo leo.
Never underestimate Human stupidity

Pia kuna hii nyingine ya Supervolcano erruption, kama itatokea basi ukae ukijua Dunia haitokalika na janga litakuwa Worldwide. Supervolcano sio kama hizi Volcano ndogondogo (Mf: Krakatoa, Mt Fuji etc), Supervolcano ikiripuka basi inatifua eneo kubwa sana kwa kufuata lines of weakness za tabaka la juu la Dunia. Kwahiyo itaenea Kms nyingi sana na yale Majivu, gesi za Sumu + Uji wa volcano utakaotoka utaenda mbali zaidi.

Lastly kuhusu A.I... bro, hii A.I tunayoiona leo ya Softwares ni ya kawaida sana maana kama ingekuwa tishio basi isingeachiwa kwa public. Sasa ku a hizi A.I ambazo hatuzijui (behind the scene) na hatujui zina uwezo gani usizi-underestimate. Haya mashirika makubwa ya kijeshi (Mf: DARPA) yanaaminika kuwa yamejikita sana kwenye Advanced Robotics ambazo hatujui uwezo wake. Lakini kama Binadamu ameweza kutengeneza Roboti dhaifu linaloweza kukujibu na kufanya maongezi ya kawaida kabisa kama Binadamu (Robot Sofia) hatujui nyuma ya pazia wanatengeneza Robots za aina gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia kama sayari itafikia mwisho wake pia pale itakapomezwa na Jua.

Inaelezwa kuwa, kuna wakati hapo baadaye Jua litapoteza thamani ama litamaliza muda wake wa 'kuishi' (expire) kisha litatanuka kupita kiasi na kuzimeza sayari za karibu yake [dunia ikiwemo].

Ila ni baadaye sana, hivyo haina haja ya kuhofia sana!

Katika suala la vita ya nyuklia, teknolojia ya kujikinga na silaha hizo nayo inazidi kufanyiwa kazi. Hapo zamani tulikuwa tukizungumzia sana kuhusu Mutual Assured Destruction (MAD) ila hivi sasa hii hoja inazidi kupoteza thamani.

Mfano: nuclear bunkers zinazotengenezwa hivi sasa kupitia mifumo ya kisasa ya tunneling zina uwezo wa kuhimili shambulio lolote lile la nyuklia wakati wowote. Bila kusahau mifumo inayoambatana na hiyo ikiwemo ABM defense systems.

Kutokana na hilo, msingi wa MAD unaweza kukosa nguvu kabisa hivyo kuiacha dunia ikiendelea ku-survive wakati huo mkiwa mmekwisha tumia silaha zenu zote kushambuliana.
Sasa bro.... issue sio kujikinga, issue ni kuwa aftermath za hizi Nuclear War zikoje..?? Na zitachukua miaka mingapi kuji-clear...??

Pia survival ni ngumu sana kwenye hii vita maana vifo kwenye Population nzima ya Dunia vitakuwa 90% kwenda juu na wale watakaobahatika kubaki hai hawatokaa miaka mingi kwenye Sayari ambayo ishakuwa poisoned na mionzi ya Nyuklia.

Pia hizi Defense Systems zitawalinda dhidi ya Mabomu ya Nyuklia ni kweli, lakini kumbuka hazilindi kwa kuyafanya haya mabomu yasiripuke.. huwa zinayatungua. Na ukitungua tuu basi linaripuka.. wote tunajua likiripuka juu ya eneo flani madhara yatakayojitokeza chini ya hilo eneo ni yapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuundwa robot sawa ila kuzidiwa na robot ni big no yaani never!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23] Why big no...??

Maana nijuavyo mie tukifikia stages za Advanced robotics basi Roboti zitakazoundwa hapo zitakuwa na uwezo wa kutenda kwa matakwa yao... labda tuwawekee mipaka tuu ya utendaji wao (Programming).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakae nazo hao hao! Wazungu!! ila tu wakifanya kosa kubwa!! waka waonyesha Wakuryaaaa walee wa. Maji matitu, Tarime!!!! Kibumaye, Kiribho, kebhanchabhncha!!!! Maweee! sijui kulee wapi srori simba!! Dunia itakuwa Historia!!

watabaki wao tu! nakwambia! tena hata hao wao wasiwe na mifugo!! Mleta mada umeweka hapa htare ya bila kufunika wala kufikiria na haya majamaa haya!! hayakawii kwenda huko, Somalia!! na huko yatazifuata tech.hata kwa bei mbaya!

hivi mreta mada unajua kure jeshi la al shaabab!! yamejaa makurya kure!! hayo hayo ndiyo yanakuja kuiba ng'ombe Mugumu na Tarime yanarudi kure kufanya biashara!!! km mie muongo Nenda Somalia anza kuimba wimbo huu ''MUraa tata nyarusare weee! hyurenge! mluzi!
unakaribishwa faster ghetoni kwa al shaabab! unakuwa mshirika na kure yanaongea kikurya tu km yako tarime! wanapanda kupitia Isbania palee mpakani!! na...... Isbania wasomali ni wengi kuliko Namanga ajili ya kusajili makuruta toka Tarime na Mugumu!

Ajabu sasa wale wasomali wa mpakani wanajua kikurya kuliko kiswahili
 
Wakae nazo hao hao! Wazungu!! ila tu wakifanya kosa kubwa!! waka waonyesha Wakuryaaaa walee wa. Maji matitu, Tarime!!!! Kibumaye, Kiribho, kebhanchabhncha!!!! Maweee! sijui kulee wapi srori simba!! Dunia itakuwa Historia!!

watabaki wao tu! nakwambia! tena hata hao wao wasiwe na mifugo!! Mleta mada umeweka hapa htare ya bila kufunika wala kufikiria na haya majamaa haya!! hayakawii kwenda huko, Somalia!! na huko yatazifuata tech.hata kwa bei mbaya!

hivi mreta mada unajua kure jeshi la al shaabab!! yamejaa makurya kure!! hayo hayo ndiyo yanakuja kuiba ng'ombe Mugumu na Tarime yanarudi kure kufanya biashara!!! km mie muongo Nenda Somalia anza kuimba wimbo huu ''MUraa tata nyarusare weee! hyurenge! mluzi!
unakaribishwa faster ghetoni kwa al shaabab! unakuwa mshirika na kure yanaongea kikurya tu km yako tarime! wanapanda kupitia Isbania palee mpakani!! na...... Isbania wasomali ni wengi kuliko Namanga ajili ya kusajili makuruta toka Tarime na Mugumu!

Ajabu sasa wale wasomali wa mpakani wanajua kikurya kuliko kiswahili
[emoji23][emoji23][emoji23] Brother.... hawafiki huku hao, kwanza wanathamani sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Funguka kaka
Ni mionzi fulani ya nishati kutoka nyota zinazopasuka supernovae inayoweza kuachia nishati kama inayoachiwa na jua ketu kwa miqka bilioni 10 katika s3kunde chache tu.

Fikiria mtu akusanye nguvu zote za jua za miaka bilioni kumi, halafu atengeneze bomu, ailenge dunia na kuilipua dunia kwa bomu hilo.

Ni kitu fulani kikitokea hata kujikinga ni vigumu. Ila uzuri mpaka sasa hatujaona gamma ray bursts kubwa zikitokea kwenye galaxy yetu au ya karibuna probability kutokea ni mara moja katika miaka milioni tano.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom