Njia Ambayo Serikali inaitumia Njia hizi Kuelezea Vitu vingi.

fortuneless

Member
Jun 8, 2016
95
49
Matumizi ya Asilimia ambapo utasikia Uchumi umepanda kwa 7.2% Budget imeongezeka kwa 32% umasikini Umepungua kwa 13% tumetoa mikopo kwa 78% wanaopata maji safi ni 27% sijui wenye kutumia choo ni 21% Makahaba wamepungua kwa 34% Watoto waliobakwa ni 4.3% watu wanaopata huduma za ARV's ni 7.3% Dar ina waathirika wa UKIMWI 31% ooooohhhhh!!

Mimi hizi namba naona huwa zinatumika kumficha mwananchi wa kawaida too much %%%%%% usage.
 
Hahahaa, umenikumbusha babaangu baada ya kustaafu shirika la reli, akarudi kijijini, akakuta rafiki yake wa enzi za utoto ana biashara ya ng'ombe za minadani, basi yule mzee akamwambia ili aweze kumudu maisha ya kijijini aingie kwenye hiyo biashara yaani unanunua ng'ombe mnada huu leo kesho kutwa mnapeleka mnada mwingine.
Basi baba akashawishika, inaonyesha baada kuingia kwenye hii biashara ya uchuuzi wa ng'ombe akaona upungufu kwenye matumizi ya huyu mzee mwenzake ingawa alikuta ina faida.
Siku moja wakiwa nyumbani baba akaanza kumuuliza mswali ambayo huyo mzee hakuyapenda.
Swali: katika mtaji wako huwa unatumia % ngapi? Ukiwa, kwenye eneo la mnada?
Jibu: kwanza lazima nipate busia kopo moja na supu ya mbuzi ndipo naendelea na mengine.
Baba akamwambia waunganishe mtaji uwe moja,akakubali, siku ya mnada wakanunua ng'ombe, wakauza, waliporudi nyumbani wakaanza kupiga mahesabu ya mapato na matumizi.
Baba: figure yetu ni 100%.
Mzee: mambo ya wanawake tena ya nini? Tuongee mambo ya muhimu,mambo ya mafiga kwani tulienda kupika?
Baba: siyo hivyo ni hesabu hiyo we tulia utanielewa.
Mzee: sawa endelea.
Babarofit ni 19%.
Mzee: ehe!
Baba: matumizi.
Mzee: ndiyo.
Baba: ushuru 0.01%
Mzee: ndiyo nini?
Baba: kiwango cha profit kilichotumika.
Mzee: we bwana ... Hii biashara kila mtu achukue chake tutaharibu uhsiano wetu na hizo % zako.
 
Back
Top Bottom