Njia 8 za kutengeneza pesa Facebook, Whatsapp na Instagram

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Inawezekana kabisa siku ambayo ulifungua akaunti yako ya Facebook, Instagram au hata WhatsApp ulikuwa na lengo na kuchati na washikaji, ndugu na watu wengine wengi. Hukufikiria kuhusu kutengeneza pesa, ulichokiona ni kwamba utakapokuwa na uhitaji wa kuwasiliana na washikaji, basi uwasiliane nao na hata wakati mwingine kuwatumia picha ukiwa viwanja ukila bata.

Rafiki yangu! Muda unakimbia sana, dakika zinasonga kwa haraka, inawezekana zaidi ya siku nyingine za nyuma, mambo yamebadilika na kwa sasa watu wana akaunti kwa ajili ya kutengeneza pesa, wewe bado unafikiria kuchati tu halafu akaunti yako isikuingizie pesa? Hakika unakosea.

Leo ningependa nikupe njia nane za kutumia akaunti yako kutengeneza pesa, si kwamba uwe nayo kwa ajili ya kuchati tu, hapana, unatakiwa kuwe na watu wanaokupa pesa za kununulia bando, pia kuwe na watu wanaokupa hela ya chakula kila siku. Ukitumia njia hizi hapa, hakika utapiga pesa kama watu wengine.

2. TAFUTA MARAFIKI WENGI AU FOLLOWERS
Kwa Facebook ningesema kwamba utafute marafiki wengi, usiogope kumtumia mtu ujumbe wa urafiki wa kutaka kuwa swahiba wake. Unatakiwa upate marafiki wengi ili pale utakapoanza kutangaza biashara zako basi watu wengi wazione.
Kwa upande wa Instagram utatakiwa kupata follwers wengi kwa ajili ya kuwatangazia biashara zako. Ngoja nikwambie namna ya kupata followers wengi Instagram. Kitu cha kwanza kabisa ni lazima posti zako ziwe kama za mtu mwenye kiu ya mafanikio. Unapoweka posti zenye akili kila siku basi hata watu utakaowapata wengi watakuwa wale wenye akili.

Hebu chukulia unaweka picha ya utupu, jua kwamba utakayempata ni yule ambaye naye atakuwa mtu wa utupuutupu tu. Ifanye akaunti yako ivutie kwa kuweka pichaau posti ambazo mtu akiziona ajue kabisa kwamba ameingia katika akaunti ya mtu mwenye kiu ya mafanikio.

Endelea kusoma posti zinazofuata ujue njia zote nane.

2. TENGENEZA UKARIBU NA WATU SAHIHI

Ukishatengeneza marafiki wengi, utakachotakiwa ni kutengeneza ukaribu mkubwa na watu wenye mawazo chanya katika maisha. Si kila mtu aliye katika mitandao ya kijamii ni wa kuwa naye karibu, wengine wabaki marafiki wa kawaida lakini kuna wengine wanatakiwa kuwa maswahiba.

Ukiwapata watu wanaojielewa, wasiokuwa na ujinga wa kuweka posti za matusi au ujinga mwingine, itakusaidia pia kutengeneza ukaribu na watu wengine kama wao ambao nao watakuwa wakiona kile unachokiweka katika akaunti yako.
Kutana nao, zungumza nao, panga nao mikakati ni jinsi gani kutafuta pesa, ukipewa njia sahihi, rudi kwenye akaunti yako, weka bidhaa zako ili marafiki zako waone na kukuunga mkono.

3. TANGAZA BIDHAA ZAKO MARA KWA MARA
Hapa ni lazima ufahamu kwamba si kila unapoweka badhaa yako mtandaoni basi watu wote watakuwa wanaiona. Wakati unaweka asubuhi, kumbuka kwamba kuna watu wapo makazini, hawaingii kwenye mitandao ya kijamii na wakiingia jioni au usiku kuna watu wengi watakuwa wameposti mambo yao.
Ili nao waweze kuiona bidhaa yako basi ni lazima uwe unaweka mara kwa mara, ili mtu akiingia mchana, aone iliyowekwa mchana na akiingia usiku basi aone iliyowekwa usiku. Usichoke, utatakiwa kuposti mara kwa mara na ninakuhakikishia kwamba kuna watu wengi wataona bidhaa yako.

4.JIUNGE NA MAKUNDI MBALIMBALI
Kwenye Facebook na WhatsApp kuna makundi mengi tu, yapo makundi ya kijinga na makundi ya watu wenye akili. Kwa kuwa upo kibiashara zaidi, usisite kujiunga hata kwenye makundi ya kijinga.
Utatakiwa kufahamu kwamba mara nyingi watu wanapenda ujinga, wanapenda makundi ya ngono, utakachotakiwa kufanya ni kuwafuata hukohuko na kuwa katika kundi lao. Utakapokuwa na bidhaa zako, tangaza humo. Kwenye watu elfu hamsini waliokuwa humo, huwezi kukosa hata watu ishirini wa kununua bidhaa zako kama tu utakuwa ukitangaza mara kwa mara.

Inaendelea katika posti inayofuata.
5. TAFUTA VIDEO MBALIMBALI NA KUJIFUNZA MENGI
Kumbuka kwamba mitandao haikuanzishwa ili watu wachati tu. Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg alikwishawahi kusema kwamba yeye ametengeneza meza na kiti kwa ajili yako, yaani ukae na uagize kitu chochote katika meza hiyo. Kwa wenye akili, kwenye meza wataagiza vitu vingi ila kwa wale ambao hawana akili nzuri ya kutengeneza biashara wataiacha meza kuwa tupu kila siku.

Kuna video nyingi zinazofundisha namna ya kufanikiwa, zitafute, tazama, zipo kwenye mitandao ya kijamii, zipo Facebook, tembelea katika kurasa za watu wengine, angalia wameposti nini kwa siku hiyo. Kuna watu wengi wanafundisha kuhusu mafanikio, kile ambacho hukijui, kuna mwingine anakijua, nenda katazame wenzako wanafanya nini.

6. WAWEKE WATEJA WAKO KUWA KARIBU NAWE
Kuna watu watakuunga mkono! Ndugu yangu hao si watu wa kuwapuuzia, utakachotakiwa kufanya ni kuwa nao karibu mara kwa mara. Kama umewauzia mafuta, uwe unawauliza wanayaonaje. Utakapofanya hivyo, mtu huyo ataona kujaliwa sana, hivyo hata utakapokuja na bidhaa nyingine inakuwa rahisi kwake kukuunga mkono kwa kuwa wewe ni mtu unayejali.

7. TUMIA PESA UNAPOTAKIWA KUTUMIA
Wengi wanajisahau, wanapoamua kutafuta pesa hawataki kutoa pesa.Rafiki yangu, ili upate pesa ni lazima utumie pesa, ndivyo biashara ilivyo. Kama ukiona huna watu wengi na ungehitaji kutangaziwa biashara yako basi wasiliana na watu wenye marafiki wengi, au followers wengi na kuwaomba wakutangazie.
Hata kama mtu atajitolea kukutangazia bure, wewe tamani kumlipa, unajua kwa nini? Hii itamfanya kukutangazia kwa nguvu kwa kuwa tu umemlipa pesa. Unapomwambia mtu akutangazie bure, hatotangaza kwa nguvu kama ambavyo utamlipa pesa. Jitahidi kutumia pesa pale ambapo unaamini kwamba utaingiza pesa.

8. USIFICHE GHARAMA
Wengi wanakosea hapa! Kuna watu wanaweka bidhaa zao kwenye mitandao ya kijamii bila kuweka gharama ya kitu hicho. Hiyo itakuwa inawatisha wateja wako. Mwingine ataona mkoba mzuri, hujaweka bei, kutokana na uzuri wake atahisi ni wa gharama kubwa kumbe ni ndogo.

Wengi hawana muda wa kukufuata inbox au kukupigia simu kukuuliza gharama za bidhaa zako bali utatakiwa kuwarahisishia kwa kuwawekea gharama ili mtu akija inbox anakuja kibiashara na si kuulizia bei. Ukifanya hivyo itakusaidia sana.

Cha kumalizia ni kwamba lazima ujue kuwa kuna watu milioni mia moja wanatengeneza pesa kila siku kwenye mitandao ya kijamii! Kwa nini wewe ushindwe? Kama unatumia mitandao ya kijamii kwa kuchati tu, ndugu yangu, unapoteza muda wako!
Chukua hatua.
 
Back
Top Bottom