Njia 7 rahisi za kulinda afya yako ya akili unapotumia mitandao ya kijamii

amai_martha

Member
Jul 27, 2021
8
25
Je, huwa unajisikia kuchoka? Wivu? Kama vile haufai au maisha yako sio bora kama ya wale unaowaangalia kwenye mitandao ya kijamii? Hauko peke yako. Hayo ni madhara machache kati ya mengi ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye afya ya akili. Mitandao ya kijamii tunaipenda, inatusaidia kupoteza muda kwenye daladala na foleni, inatupa kampani tunaposubiria watu, hutusaidia kusema vitu vyovyote hadharani na kukutana na watu wanaofikiria sawa nasi, hutupa madili mbalimbali lakini pia hutuhabarisha na hutuchosha ili tulale, lakini je ushawahi kuwaza madhara yake kwa muda mrefu ni yapi?

Tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii huchangia kwenye watumiaji kupata sonona, wasiwasi, kutolala vizuri, kushindwa kujithamini na kujikubali miili yao na hali zao za maisha kwa vile wanajilinganisha na kuhisi kuwa maisha yao yanabidi yafanane na yale ya mtandaoni na pia kuwa mateja kwa kutaka kuitumia mara kwa mara mitandao hii. Utafiti wa mwaka 2015, ulionyesha kuwa wanawake wanapata sana msongo wa mawazo kupitia mtandao wa Twitter kuliko wanaume, kwa vile wanaona na kufahamu shida za watu wengine na vitu vinavyowasababishia msongo wa mawazo watu wengine kupitia mtandao huo.

Kama ungependa kuendelea kutumia mitandao hii huku ukiilinda afya yako ya akili dhidi ya athari hizi zinazoathiri afya ya akili, vile unavyoiona dunia na unavyojiona, hizi hapa ni njia zitakazokusaidia kufanya hivyo:

1- 'Unfollow' mada au watu wanaokufanya ujisikie vibaya, unapofungua mitandao ya kijamii, yale unayoyaona ni matokeo ya mada ulizozifuatilia au watu unaowafuata. Kama haupendezwi na mada, watu au kuna namna posti unazoziona zinakufanya ujisikie kila ukiingia mtandaoni basi 'unfollow' watu wanaoongelea mambo yanayoendana na vitu unavyoviona vinavyokufanya ujisikie namna fulani.

2- Chukua mapumziko ya mitandao ya kijamii, utafuti unaonyesha kuwa binadamu anapata habari zenye ukubwa wa GB 34 kwa siku kupitia televisheni, redio, magazeti, matangazo na mitandao ya kijamii. GB 34 ni kubwa sana, ubongo pia unahitaji kupumzika. Chagua wiki, mwezi au hata mwaka ambao unaweza kupumzika, ukweli ni kuwa hauwezi kupitwa na vitu kama unavyodhani utapitwa, na marafiki zako wa kweli watatafuta namna ya kukupata zaidi ya mitandao ya kijamii. Wewe sio mashine hivyo ni muhimu kupumzisha mwili na akili, mapumziko ya mitandao ya kijamii yanasaidia akili yako kupumzika, na hivyo kukusaidia kwenye afya yako ya akili. Kwa wale ambao wanaona pia mitandao ya kijamii haina kazi kwao sana na inawapa madhara mengi kuliko faida, pia unaweza kuifuta, sio kila mtu yupo mtandaoni au sio kuwa utakuwa kitu cha ajabu ukiwa hauna akaunti mtandaoni. Ishi maisha yako kwa namna inayokuletea furaha zaidi.

3- Kuwa na mambo mengine ya kufanya zaidi ya kupata furaha yako kwenye mitandao ya kijamii. Kama mitandao ya kijamii ndiyo kazi yako, ni rahisi kutumia muda mrefu hapo maana ndio ofisi, ila kwa sisi tunayoitumia kutaka ile furaha ya muda inayotoa au kwa kukosa cha kufanya na kutaka kupoteza muda, inakuwa vyema zaidi kama utakuwa na vitu vingine vya kufanya maana mwisho wa siku baada ya kumaliza muda wako wote kwenye mitandao ya kijamii unaanza kujisikia kama haujafanya cha maana kwenye siku yako zaidi ya kupoteza muda. Hivyo wekeza huo muda unaotumia kwenye mitandao kwenye kufanya au kujifunza vitu vingine, au pia kukutana na watu uso kwa uso zaidi ya mahusiano yako kuwa mtandaoni tu. Kwa dunia ilivyo sasa ukifuatilia kila habari ya mtandaoni na ukakaa huko tu, unaweza kudhani dunia inaungua na hakuna tumaini, ila ukija mtaani ndio unaona maisha yanandelea tu vizuri na ukweli wa mtaani muda mwingine ni tofauti au mpana zaidi ya maneno machache unayoyaona kwenye Twitter. Na maisha ya Wema au Diamond kwa siku anapitia hisia nyingi zaidi tu ya posti moja ya furaha au kujisifu aliyoiweka asubuhi ambao inakufanya umchukie au ujisikie vibaya kuhusu maisha yako.

4- Usijilinganishe na watu wa mtandaoni, mbali na kuwa picha nyingi nizaku-edit, watu wengi pia huwa hawaposti ukweli wote wa maisha yao au yale wanayoyapitia kwenye mitandao. Unaona sehemu ndogo sana ya maisha ya mtu ukimuona mtandaoni, kwahiyo ile aliyokuonesha sio maisha yake yote na mara nyingine sio maisha yake ya kweli. Usijiliganishe na watu wa mtandaoni.

5- Zima arifa, arifa inaingia kuwa fulani kaposti, unaenda kuangalia alichoposti mara unajikuta nusu saa imepita, na unajisikia wivu kwa jinsi maisha yake yalivyo mazuri na sasa muda umekwenda kazi uliyotakiwa kufanya haujafanya. Zima arifa ili uwe unahabarika mtandaoni pale unapoamua wewe kuingia mtandaoni. Arifa ziliwekwa ili zikuvuruge, kila zikiingia, zikupe shauku ya kuangalia nini kinaendelea mtandaoni na kwa vile mitandao imetetengenzwa kukupendezesha wewe ili uwe teja kwayo basi unajikuta unatumia muda mwingi zaidi kuliko uliotarajia utatumia.

6- Jipangie muda wa kuitumia kwa siku, ni vizuri kujitambua na kuona namna mitandao ya kijamii inavyokuathiri, na kama kwako ni muhimu sana kuitumia basi jiwekee mipaka ya muda kwa siku. Kila kitu ni kizuri ukikitumia kwa mipaka fulani, linda afya yako ya akili na macho kwa kujiwekea mipaka ya habari na posti unazozifuatilia kwa siku.

7- 'Follow' vitu vinavyokupa habari njema zaidi kuliko mbaya, mitandao ya kijamii huleta msongo wa mawazo zaidi hasa ukiona mabaya kwenye eneo unalolipenda. Sisemi usihabarike ila habari nyingi hasi hushusha moyo chini. Jaribu kufuatilia vitu vizuri pia, dunia sio ina mabaya tu, ina mazuri pia. Mazuri yanaweza kuamsha hisia nzuri ndani yako jambo ambalo ni zuri kwako. Katika hili pia kumbuka sio kia mada mtandaoni inahitaji mchango wako, mada nyingine jiepushe nazo.

La mwisho kwenye hili ni vizuri kujichunguza na kuona vile mitandao ya kijamii inavyokubadilisha, watu wengi hupata kujiamini mitandaoni au kujibu vibaya mitandaoni wakati hadharani ni watu wema. Jaribu kuwa mtandaoni, yule ambaye wewe upo hadharani, hii inabadilisha mitandao ya kijamii lakini pia inakubadilisha vile unavyoishi au unayozungumza na wengine mtandaoni. Jua muda wa kupumzika na kutoitumia kama unaona inakuletea madhara kwenye afya yako ya akili. Mara nyingi watu ni wepesi kulalamika kutaka kubadilisha mitnadao ya kijamii ilivyo, wakati njia rahisi ni kubadilisha au kuacha matumizi ya mitandao hiyo.

Na hizo ndio njia saba unazoweza kuzitumia kulinda na kupunguza athari za mitandao ya kijamii kwenye afya yako ya akili. Je ni athari gani umezipata katika matumizi yako ya mitandao ya kijamii?

- M
 
KONGOLE KWA UZI MZURI SANA
 
Back
Top Bottom