Njaa kali mjini nimelazimika kuulizia mashamba ya marehemu babu

whitehorse

JF-Expert Member
Aug 29, 2009
2,565
4,432
Zamani wazazi wangu walikuwa waajiriwa Kwa sasa wameshatangulia mbele za haki (RIP Mama na Baba) walikuwa na mashamba kijijini huko mkoani walikotoka. Walilima kwa kutuma pesa ili kuweka vibarua na Hata kwenda wenyewe wakati wa likizo
Tulikuwa tunasafiri kwenda huko kulima au kufanya chochote kule shambani kufuatana na Msimu tutaofikia

Hatukukosa chakula nyumbani mwetu. Mavuno yalipatikana Sio haba tulishiba mno na kugawa hadi Kwa majirani ule Msimu wa mavuno. Walipofariki wazazi wetu utaratibu ukaishia hapo. hatukukumbuka mashamba wala Msimu wa kilimo tena. Babu na bibi wakafa pia Ndio kabisaa hat sababu za kwenda kijijini kule tukakosa. Sasa huku mjini joto limeanza kushika kasi JPM amebana Hata semina kunduchi beach hamna Leo Mwaka unapiga kati (june) siamini Kama nimekuwa kiumbe wa kutegemea mshahara tu . Wafanyakazi wa umma jasho linatutoka Jamani kha!

Nimewaza weee Leo Kwenye foleni nimenyanyua simu yangu natafuta angalau ndugu mmoja wa kijijini kuulizia mashamba kiaina Jamani majibu yamenipa majonzi matupu
"baba yenu Mdogo ameuza mashamba mengi kuna mengine amekodisha, Yale mengine ya kule karibu bondeni watu wanalima bure tu tena Kama lile shamba la baba yako nimelima Mimi Kwa kweli nashukuru nimepata Sana Mwaka huu"
Alinijibu ndugu huyo wa kijijini ambaye angalau huwa namrushia hela ya chumvi

Hadi nakata simu nimebaki kufikiria kwenda kuomba angalau ekari mbili za marehemu wazazi wangu Kwa baba Mdogo sijui atanipa

Turudi kulima tu sasa mashamba ya marehemu babu zetu yanalimwa na majirani turudi kuyapokonya tulime tupate chakula mjini hapa tutaadhirika hali ngumu Sana kweli kabisa wanaofaidi Ni wenye hospitali binafsi tu watu wanaumwa wanaenda kutibiwa kila siku biashara zingine hovyo kabisa nasikia Hata guest houses watu hawaendi hawana hela ila
 
Ada ya watoto huko shule za English medium tuliwapeleka sasa kina eleweka. Mikopo kila kona mpaka hatukopesheki tena. Hakuna rangi tunaachana kuona. Watu wanauza mashamba , viwanja, nyumba hadi magari.....afanaleki.
 
bado haujachelewa msim wa kulima karbu utaanza kwani sasa wana vuna.....
 
TUNAISOMA NAMBA KIKAMILIFU. NA JUZI NDO His Excellence anamesema tukipelekwa KIKWATAKWATA TUTAFIKA.
 
Sawa unalima
Swali utamuuzia nani kama uchumi umeporomoka?
Watu twasubiri fadhira za mahindi ya msaada na hayo mahindi yatanunuliwa kwenu kwa bei ndogo
 
Sawa unalima
Swali utamuuzia nani kama uchumi umeporomoka?
Watu twasubiri fadhira za mahindi ya msaada na hayo mahindi yatanunuliwa kwenu kwa bei ndogo

Sifikirii Sana kulima Kama biashara nalima ili kupunguza makali ya kununua maharage 2400 Kwa kilo Mwaka mzima na Dona kilo 1500-1600 Mwaka mzima it's not a joke kusafirisha kiroba cha kg 20 kutoka bush Ni sh 5000 ndugu yangu bora nikashike jembe nile vyangu na ndugu zangu niwagawie Kama walivyofanya wazazi wetu walisave Sana tu life ya jiji hili .
 
Haya maisha haya dah kuna mwingine kaja Leo na ushuhuda Wa kufungua bar Yake Hali imekuwa ngumu watu awajuhi hii nchi inapoelekea alafu tunaambiwa makusanyo ya kodi yameongezeka
 
Sawa unalima
Swali utamuuzia nani kama uchumi umeporomoka?
Watu twasubiri fadhira za mahindi ya msaada na hayo mahindi yatanunuliwa kwenu kwa bei ndogo
Ni bora hata akila mwenyewe ili ambayo ungenunulia chakula ifanye jambo jingine ..hili ni darasa guru kweli JPM anatoa somo bila chaki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom