Hebu jaribu kufafanua kama njaa nayo ni kigezo bana!
Kweli mkuu njaa ndio kila kitu ndio kigezo kikuu na ndio mpango mzima wa kuingia huko
Mkuu njaa si huwa inafikia mwisho?
nakuwaje sasa hapo?
Baba paroko ndoa inajengwa na vitu vingi.ukisema akishiba ataacha bhasi kila siku watu wangekuwa wanaoa huyu lengo la njaa...huyu upendo...huyu anataka watoto..nk
Ila ndoa ni muunganiko wa mengi
Na kama kimojawapo kikikosekana bhasi haitokamilika
Maagano ya ndoa lazima chakula kiwepo tna chako mwenyewe upate kwa muda muafaka ili usitaman chakula cha mwingine pind upatwapo na njaa.
Ndo mana kama utamnyima mwenzio chakula pind akiwa na njaa utashtakiwa
Huwez kusema akishiba ataacha sio kweli kwa maana njaa ipo siku zote na mlaji atafurahia kama anapata "chakula chenye quality "
Labda kwasababu "moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote" ...lol!
njaa haina mwisho....unakula inatulia baada ya masaa fulani inarudi tena....kuna siku unapigwa njaa kila ukitafuta 'chakula' hupati unaweza kula 'jalalani'....na hapo ndio wazo linakuja hivi ningekuwa na wife ningehangaika hivi...!
Mkuu hili nalipinga kabisa
Njaa ni mengineyo tu
Njaa nasema sio sababu kwakuwa njaa ina time frame,yaani kuna wakati inakuwa haipo kabisa na huu wakati ni mkubwa au mrefu sana kwenye maisha ya ndoa
Ukiongozwa na njaa ndoa inafikia ukomo mapema sana!
Na kwa pointi yako hii basi ni kuwa njaa sio kigezo cha kuingia ndoani bali kuna sababu nyingine ambazo zinatakiwa zikufanye uingie ndoani!Mkuu Sawa nakubaliana na wewe njaa ni ya wakati na kipindi na sio ya kila saa na muda wote
Ila kwa hao wanaooa kjwa sababu ya kusema wanatuliza njaa hawafikirii hilo
Wanawaza tulizo la njaa tuu basi
Na ndo maana watu kama hao chakula cha nyumbani kikiwa kibaya ni wepesi sana kukimbilia magengeni na mtaani kutafuta chakula kitamu
Na ndio hao ambao wakiona chakula kipya kimetengenezwa mtaani hawaishi kutokwa udenda wa hamu
Ni kweli unayosema lakini ninachosema hapa ni kuwa,kama sababu ya kuingia kwenye ndoa ni njaa,unadhani ukishiba sababu ya kuendelea kuwemo ndoa ni itatoka wapi?
Njaa sio sababu pekee na hat ikitokea huna njaa unaweza kuishi kwa Yale mengine ya muunganiko .
Ingekuwa ikiisha na ndoa inaisha ingekuwa shida
Kwa mfano MTU alioa kwa lengo LA kupata mtoto je akishapata mtoto ataachana na ndoa?
Njaa ina mda wake na mengine yana mda wake
Na kwa pointi yako hii basi ni kuwa njaa sio kigezo cha kuingia ndoani bali kuna sababu nyingine ambazo zinatakiwa zikufanye uingie ndoani!
Ndo maana mkuu tunasema kabla ya kuingia huko jifikirie kwanza unajua ni kwa nini unaoa au unakimbilia kwa sababu ya kutuliza njaa tuu
Au kwa sababu fulani kaoa anapata chakula chake kila siku na wewe unaamua kuingia huko
Unatakiwa ufikirie zaidi ya hapo na zaidi ya hilo
Sio Njaa kuoa ni kutafuta heshima baada ya umri kufika Njaa inawezwa kutulizwa na MTU yoyoye utakayemuamulia kumfatilia siku hizi ni kubip tu kuwa Leo una njaa unapigiwa nikuletee wapi?
Kwako au guest, ukitaka ni pesa yako tu au msingi kiuno.
Mkuu Sawa nakubaliana na wewe njaa ni ya wakati na kipindi na sio ya kila saa na muda wote
Ila kwa hao wanaooa kjwa sababu ya kusema wanatuliza njaa hawafikirii hilo
Wanawaza tulizo la njaa tuu basi
Na ndo maana watu kama hao chakula cha nyumbani kikiwa kibaya ni wepesi sana kukimbilia magengeni na mtaani kutafuta chakula kitamu
Na ndio hao ambao wakiona chakula kipya kimetengenezwa mtaani hawaishi kutokwa udenda wa hamu
Nikweli mkuu
Mtu unaingia ndoani kwasababu tu umefurahishwa na post za mtu hapa jamvini kumbe kwenye uhalisia ni kinyume
Sijui kama utavunja ndoa au laa
Njaa inaweza kukufanya ukakitamani chakula fulani lakini ukishahsiba unaanza kukiona chakula hakifai kabisa!