Niwasaidiaje kaka zangu?

Kwahiyo Dada Jesca kuniomba msaada wa kukuunga JF sikuile ndio nia yako hii kuja kutusema na bora ungebadili User name nisiikujue, haya yote situngeyaongea kifamilia kumbuka sisi kakazako huwezi kutuweka hadharani hivi mtaji kweli ulinipa ila mdogo sana.
 

Duh kiswahili ni lugha yako ya ngapi?
 
Pole sana mdogo wangu. Mungu awatie nguvu
 
Mwalimu wetu wa physics form two sijui alikua anafundisha topic gani akatuambia ili rocket ipae inahitaji ukinzani wa hali ya juu sana kisha akaendelea akili ya binadamu ni kama rocket ili ifanye kazi inatakiwa ibanwe kisawasawa na kuanzia hapo alitupeleka mchakamchaka mpaka wengine walikimbia somo lake

Sasa nachotaka kusema hapa ni kwamba hao kaka zako acha kuwadekeza we wakatie mirija kabisa ikiwezekana hata wakikupigia simu usipokee badili namba kabisa kisha fanya mambo yako ya msingi haiwezekani dume zima at age of 30 unalilipia kodi na hela ya nauli unalipa litajiongeza saa ngapi sasa

We kata misaada fanya mambo yako wangekua wa kike kidogo inge make sense
 
Sikia dada,hutaweza kuwaondoa kaka zako kwenye mduara wa umaskini hata kidogo,chakufanya wewe jenga msingi wa maisha yako,na wape msaada mkubwa wazazi wako kwa kadri ya uwezo wako,hao kala zako,hebu waache kwanza wapambane na hali yao,usiwalipie kodi,unawaharibu,hawatatafuta kwakuwa wanajua wewe upo
 
USHAURI WA BURE
Jenga kwanza alafu katk kujenga kwako kama unawez weka mabanda ya mifugo na fremu za biashara
Ukimalza Jenga ita Hao kaka zako wafuge na wafungue biashara wazisimamie kabla hujaolewa
Ukiwa na bwana usimpelekw apo kwako waheshimu kaka zako.
Kwa maelezo zaid njoo INBOX
 
Hapo tumia Elimination Method.​
Let X = Nyumba​
y = Kaka zako​
Halafu ondoa Kaka zako solve for X then malizia kusolve y.​
Application ya symliteneous equation kwenye real life ndo inatumika hapa.​
​
 
Mkuu,hongera sana kwa kuwa na hekima.Kaka zako hawahitaji msaada wa kifedha,wala mtaji.Wanahitaji kuwa challenged-JENGA KABISA MJENGO uliokamilika wa maana.KOPA FUNGUA BIASHARA YAKO USIMAMIE IKUE,TAFUTE MUME MWENYE BUSARA ALETE POSA ANATAKA KUKUOA.

Fanya mambo makubwa mpaka wao waje kwako watake ushauri,msaada.USIWAPE NAULI WALE ELA YA KULA ISPOKUWA KAMA WANAUMWA.Kama ni njaa wacha wajifunze kuishi kwa bajeti yao.

Huo ni mtazamo wangu na ushauri wangu kwako.Kama unahitaji ushauri zaidi wa namna ya kwasaidia basi karibu PM
 
Mtoto wa kiume ashiki mimba...

Mtoto wa kiume mwache mwenyewe ajitume...

Mtoto wa kiume maisha yanavyomchapa ndo na akili hufunguka...

Concentrate na wazazi, hao ndugu zako uzuri ni wakiume ipo sku akili zitawakaa sawaa tuu na watazishika kuliko wewe na kuwasahau wazazi...
 
Kwakuwa Unapambana Upate Nyumba Iwe Msaada
Naona Ungetia Juhudi Kwenye Nyumba Ikamilike
Kwakuwa Uwezo Wako Ni Mdogo, Ukiwa Hutaweza Kumaliza Hiyo Nyumba

Halafu Maisha Yanakwenda Kasi Hakabadilika Wakati Wowote
Yanaweza Kuwa Mazuri/Mabaya. Jenga Nyumba
 
Kama sijakuelewa kaka! Kwamba nimejivuna au? Hali yoyote niliyoielezea hapo ni ili tu mpate picha halisi ilivyo ningeficha vingine cdhani kama ningeeleweka! Na wala sina majivuno kabisa! Km nimekukwaza pole
We achana naye huyo wamezoea kuiba ng'ombe, majangiri kwa kifupi uelewa wa ni mrefu kwenda chini.
 
Je wazazi wako hai? Huna obligation ya kuwabeba kaka zako. Unachoweza ni kusaidia kuwapatia uwezo wakujitegemea. Ask them what they need for them to stand on their own feet. Do not impose. If possible involve your parents. Karibu utakuwa na mji wako ie your own family na utashindwa ku sustain kusaidia kaka zako.
 
Jibu zuri sana
 
Yaani Jesca sikujua kama una tabia ya kuwasimanga ndugu zako hadi JF. Kwani Geoffrey alikosea kukuelekeza namna ya kujiunga JF hadi uje umsimange namna hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…