Niwaeleze yanayotokea ofisini

Niwaeleze yanayotokea ofisini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Kule ofisini ni sehemu yetu ya kumalizia stress. Tukipata muda hasa lunch time tunawasema waume zetu na kumaliza hasira. Kama uliamka ukakutana na taulo chini sakafuni, na bafuni jamaa alisahau kuflash basi yote yale ukiyatoa pale mashost wanacheka unapata ahueni.

Sasa ukutane na na aunt wakuzodoe, wakwambie hukufundwa wewe. Mimi niko kwenye ndoa mwaka wa 35 huu na wajukuu tumepata lakini ulishanisikia nikimsema uncle wenu hapa! Mmh auntie ni kwakuwa huna age mate hapa.

Jioni mkija kutupitia ukichekewa sana shemeji shemeji usifikiri kuwa wewe ni mzuri sana. Ni kuwa wanakumbuka ile stori yako ya kutapika kitandani siku ile ulipo changanya red wine 🍷 🍺 na🥃 brandy.

Mkittuachisha kazi haya tuyaongee na dada wa kazi au na mama Pili mtaa wa pili?
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kuna kipind wife alisema nimeambiwa na shoga agu appetite yako inapotea kwasabab huli mapish yangu sikuiz unakula ya dada wa kaz..ndo mana hata kiwango cha unywaji kimeongezeka..moyon nikajua nishachomwa kwa shoga yake job mana shem zilizid
 
Mi nimekodoa macho ili nione vizur sehemu ya iliyoandikwa paaaa puuuu chiiiiii zinavyozinduliwa vizur na baadhi ya wajanja wa ofsini kumbe hakuna, ngoja ninawe nikalale zangu tu.
 
Hehehe ofisi yenu tofauti. Sie ofisi yetu kila mtu mjanja, anapendwa, ni malkia, anapelekwa dubai holidays na analetewa maua kwenye besdei na keki kuubwa.

Siku yakaletwa maua mazuriii. Nikasema mazuri haya, mirabel huyu? Heh alieletewa akataja alieyaandaa na bei. Nikachekea tumboni nikajua kajinunulia huyu. Uzuri sie hatuzodoani, tunasifiana tu ujinga
 
Kwa vle sijaelewa sana nadhani hainihusu sana[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom