Binafsi nina penda sana kufanya video za miziki, nimejipanga kimtindo nataka nichukue camera dslr moja nijikite zaidi sema nina swali unaposema motion graphics unamaanisha moving objects/ graphics?
Sijawahi itumia AE maana mimi ni begginner hivi hiyo AE inaweza kutumika ku edit videos pia au?
Karibu sana katika ulimwengu wa film/video production, uta enjoy zaidi kama siku zako za awali utachukulia kama hobby na siyo permanent career. Nasema hivyo kwa maana kwamba, watu wengi wanao wekeza katika hii industry kwa expectations za kutengeneza faida kubwa ya haraka, huishia kujilaumu pale matarajio yanapo chelewa.
Twende kwenye mada:
Ukiachia editing, motion graphics ni moja ya hatua muhimu sana katika post production ambapo mchanganyiko wa images, symbols, colours, fonts, objects hutumika kuongeza feelings and life katika film or video.
Kwa filamu ambayo iko well organized, team ya watu waliobobea katika compositing, inabidi ihusike tangu hatua ya mwanzo ya ku shoot ili zoezi la motion graphics liwe rahisi wakati wa post production.
Nikija kwenye swali lako la "motion graphics..moving objects/ graphics?".ni kweli,ili motion graphics ikamilike lazima kuwe na hali ya motion ya kitu kupitia animation.walibuni jina hilo ili kutofautisha na print media graphic design.
Tukija kwenye swali la AE kama inaweza ku edit.
Technically AE siyo program ya kufanyia editing kwa sababu haina baadhi ya tools ambazo zitakurahisishia utendakaji kazi.kwa mfano tool kama wembe (razor) haipo ndani AE.
Mfumo wake wa layer ni tofauti na editing program kama adobe premiere nk,kila layer inajitegemea,kwa maana hiyo hutaweza kuunga clip mbili katika layer moja na ku apply transion ie cross dissove.
Kwa upande wa audio,japo inaruhusu kui import audio na ina basic audio effects,interface yake haikupi nafasi kubwa ya kuweza kucheza na audio file,hauwezi ukafanya audio mixing au mastering kama AP (adobe premiere).
Nashukuru mkuu kwa mawazo hayo mimi napenda sana video making + editing nilianzaga na windows movie maker nilianza kuunganisha picha kuongezea miziki, na maneno maneno na baadae nikawa naandika kama love story hivi na majority walikua wanazikubali sana, sometimes in the future nataka nijizatiti kwenye matangazo na nataka nifanye kama career na iam very patient on this nataka nianze kuzi edit videos nazo zichukua kwenye simu kwa program ya final cut pro naamini una experience kubwa mfano nikijipa miezi 6 full fledge ya kujipiga nondo siwezi kua competent by january 2016 ? maaana nimeona gap kubwa sana kwenye haya mambo kwa Tanzania

Vp kwenye ku download adobe after effect, unanunua, ni bure au ni bure but unapewa trial period?
matumizi ya msingi ya AE ni kutengeneza digital visual effects, motion graphics na compositing.hiyo ni kutokana na muundo wake.ili kuyafanya hayo yote,files lazima ziwe katika mfumo wa picha za mwendo(film/video) ,picha mnato(still picture) au ziwe zinatoka katika program zinazo oana na AE na ''kuseviwa'' katika mfumo uliokubliwa na adobe.mfano photoshop files PSD,maya scene files,cinema4D files,quicktime files nk.Mimi swali langu matumiz ya adobe after effect,unatumika kwenye kutengeneza nini zaidi,je video pekeyake?
uliza swali wapi panakutatiza kuhusu Adobe Premiere Pro.nipo online.
kuna posts tayari nilisha eleza kazi ya AE.zitafute mkuu.Kazi yake ni nini labda unifafanulie, na mfano wa movie ambayo hizo effects ziko applied