Mi naomba unijuze jinsi ya kupika kachori
Naomba unielekeze kupika BIRIANI
MahitajiMie nataka kuelewa namna ya kupika sambusa za nyama.
Halafu kwa nini kila ninapopika huwa naugnua sana bana.
Au mikono yangu ina matege.??
MahitajiNAOMBA NIELEKEZE JINSI YA KUPIKA TAMBI NZURI ZA RANGI NA HARUFU NZURI.
Thank youMahitaji:
Viazi ,Kitunguu saumu(galic) na Tangawizi iliosagwa,Chumvi,Pilipili ya kusaga kutegemea na unavyoipenda,Ndimu,Mafuta ya kupikia,Unga wa dengu au Ngano Kiasi.
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Chemsha viazi mpaka viiive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.
2. Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini(viponde kabla ya kupoa)
3. Saga vitunguu saumu na tangawizi kisha changanya na viazi .
4. Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.
5. Tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray.
6. Vuruga unga wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.
7. Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.
8. Chovya madonge kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia)
9. Wacha kachori zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.
10. Weka Kachori kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa na chatne na juice au chai.
My dear, tambi hizi zinaitwa pasta.Mahitaji
Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)Mafuta (vegetable oil)Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai)Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai)Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai)Maji kiasi
Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.