Conspiracy Theories hazikosekani hasa kwa watu maarufu kama MJ.Hiyo documentary niliiona youtube kuwa kauawa na Freemasons na DMX kuwindwa all in all hizo ni theorioes.MJ alikuwa kutoka uanamuziki wa kawaida hadi superstar mkubwa sana kwa ubunifu aliokuwa nao tangu Jackson 5 hadi kuwa solo na alijiunga na Motown records ambayo ilikuwa lebo ya weusi na akatingisha dunia nzima.Tungo zake zenye akili nyingi na ujumbe mzuri zitadumu mpaka dunia itakapoisha na sasa wanamuziki wa sasa hawafikii hata kidogo kiwango chake katika utunzi,kuvaa,kucheza,productions za audio na video,management,uwekezaji n.k.Bahati mbaya ni kwenye mahusiano The Wacko Jacko hakufanikiwa.Kuhusu ishu ya rangi MJ alikuwa haupendi weusi ukiachana na hizo sababu za ugonjwa wa Vitiligo.Alifanya show kubwa ya kuitangaza Pepsi miaka ya 80 ambapo aliungua moto kichwani.Pepsi walimlipa fidia kubwa na ikabidi awe anavaa mawigi maisha yake yote yaliyobakia.Alibadili pua yake na rangi pia kwani alikuwa analala kwenye kitanda maalum ambapo anaweka kichwa chake katika kifaa maalum.Alichongwa pua miaka ya 1989,1990 na mara nyingi tu.Alifanya operesheni nyingi tu kurekebisha kidevu,mashavu,paji la uso macho na hiyo ni sababu ya usuperstar kuwa mashabiki watamuonaje.Kama mastaa wengine kama MARYLIN MONROE alijikuta anaingia kwenye uteja wa dawa za usingizi mpaka zikamuua.Baada ya kukaa nje ya game kwa muda mrefu sana na albamu zake kutovunja rekodi kama za miaka ya 1980s ilimuuma sana na kumsumbua.Mapromota waliandaa shoo kubwa sana yenye thamani kubwa ya THIS IS IT iliyokuwa ifanyikie ukumbi wa O 2 jijini London.Waliweka matumaini makubwa ya kutengeneza pesa nyingi na pia kumrudisha MJ kwenye chati yake hivyo ilimpa msukumo mkubwa.Tafuta videos za show ya Rehearsals za This is it utaona mzee alivyokuwa anawapeleka vijana kwa viwango vyake vya 1980s na alikuwa hafanyi mzaha .Hiyo pole pole ilipelekea kwenye kifo chake kwani alizidisha utumiaji wa dawa za usingizi.Alikuwa akimlazimisha Daktari wake Murray mtaalam aliyebobea katika fani ya dawa hizo amuongezee dose na dose mpaka zikamuua.NIKIRUDI NTAANGAZIA NYIMBO NA ALBAMU ZAKE.