Niulize chochote kuhusu biashara ya duka la rejareja

Je kama umempa mtu auze vitu ni njia gani rahis ya kumthibit awe makin asipoteze au kukopesha bidhaa bila kukumbuka?
Ukiajiri mtu kubali kuibiwa ila la muhimu hakikisha unapunguza kuibiwa.

Hakikisha Kila siku unakuwepo, unakuwa unajua bidhaa ipi imetoka ipi imepungua.

Usimpe access ya yeye kununua bidhaa ziliisha, hiyo ni kazi Yako.

Fanya ziara za mshtukizo mara Kwa mara.

JIPANGE KUKAA DUKANI MWENYEWE
 
nakazia

usimpe uhuru wakununua bidhaa nunua wewe mwenyewe
 
Inategemea malengo Yako ni nini.

Kama umeridhika na ukubwa na kipato unachotaka, kula Bata.

Kama unatamani liendelee kuwa kubwa unaingiza kwenye mzunguko.

Malengo yako ya Leo ndio yanaamua maisha Yako ya kesho.
Ahsante mummy lov u
 
Hakuna uchawi Wala ndumba nazingatia hzi mbinu
*nafungua mapema nachelewa kufunga
*sikopeshi hata kitu Cha Mia kukopesha nikumfukuza mteja
*kuwa msafi na kupanga vitu vizuri kuhakikisha duka linavutia
*usipende tongoza tongoza wake za watu na wasichana wa mtaani hapo utajitengenezea sifa mbaya
*kuwa na huduma nzuri kwa kila mtu
*hakikisha unakua na bidhaa ambazo zinakutambulisha kuwa dukani kwako pekee iyo bidhaa inapatikana
* tafuta machimbo ya Bei rahisi
duuu kwa iyo mtu akiwa anataka bidhaa ya 600 alaf ana 500 anasema 100 atakuletea baadaye hapo vip unampa au ??
 
Vingi alivyoongea mtoa mada vina ukweli. Bodhaa nyingi zina faida ya 12-30%. Vocha ndo zinakupa 5% faida.

Kama unauza shs 200K per day una uhakika wa faida ya 20K. Per month unakunja 600K.

Kama unafamilia jitahidi matumizi ya familia yasitoke kwenye biashara bila kulipia.
Mfano ukichukua kipande cha sabuni mafuta, sukari nk lipia.

Vinginevyo matumizi yako yakiwa yanatoka dukan hutoboi
 
Ndioooooo
 
Huu uzi umenikumbusha nilipofunga duka langu la mtaa na Madeni ninayowadai watu kama 120K hivii aiseee Biashara ya Duka ni ngumu sana hasa ukifanya uswahilini.. japo pakichangamka unapata hela shida mikopooo..!!
 
Kuna mwamba hapo ametumwagia chai ️ eti kaanza na laki 5 miezi sita tu duka limekuwa kubwa motivation speaker mnazingua sana
Mwenyewe nimemshtukia inawezekana hata hilo duka sio lake maana huo mzani tu wa kupimia sio chini ya laki 1 hzo shelf ukutani?
 
Back
Top Bottom