Nitumie vyakula Gani baada ya kufanyiwa Upasuaji (oparesheni)

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,625
2,443
Ndugu zanguni habarini za Asubuhi ? Nimefanyiwa oparesheni ya kwenye utumbo wangu hivi napaswa kutumia vyakula gani ? Na ni vyakula vya aina gani sipaswi kutumia, Mie niliambiwa nisitumie MAHARAGE,UGALI ambao unga wake haujakobolewa, na vitu vigumu vigumu , je na hili zoezi inabidi niende nalo kwa muda gani? maana na nina wiki ya pili sasa na kuna baadhi ya vyakula naogopa kuvitumia nikihisi vitaniletea madhara.

Huwa sina tabia ya kula kula vitu napenda nile kwa muda.

Asubuhi Uji au Chai.

Mchana Chakula.

Na Usiku Mida ya Saa tatu Napata Chakula then nalala.

Karibu kwa mchango wenu.
 
Ungefafanua zaidi hiyo operesheni ilikuwa inarekebisha tatizo gani?

Ulipaswa kupewa ushauri juu ya lishe kabla na baada ya operesheni.

Wiki mbili ni chache sana kwenda tofauti na maagizo ya daktari.

Operesheni nyingi zinakuwa na siku za kurudi hospitali kuangali maendeleo ya mgonjwa....ukirudi unapaswa kuuliza maswali upate ufahamu juu ya vyakula na vinywaji unavyopaswa kutumia.

Ushauri wangu....jaribu kuwahi kula chakula cha usiku....saa tatu usiku naona umechelewa sana, labda kama unafanya kazi usiku.

Ugua Pole.
 
Pole...

Kwenye ulaji baada ya kutolewa kidole tumbo huwa kuna mabadiliko pale manzoni....
Baadae unaweza kuendelea na vyakula vyako vya kila siku.

Cha kuzingatia ni uponaji wa kidonda, kulingana na njia waliyotumia kuondoa kidole tumbo chako.

Zingatia vyakula laini , matunda , mboga na maji pia ili usikaukiwe.
 
Mi niling'oa tu jino huu mwezi wa 5 sasa nahisi kuna ka u sensitive fulani kwa mbali nikigusa na ulimi , wewe operation ina wiki mbili unakuja kuomba ushauri jf ? For real mkuu? Kama unaipenda afya yako basi fanya kuwauliza madktari husika , napendekeza hospitali uliyofanyiwa operation.
 
Mkuu kwa appendix mara nyingi wanatumia nyuzi ambazo ndani ya siku 7 mpaka 14 inakua Ishayeyuka mwilini ivoo ndani ya siku 7 mpaka 14 kula vyakula laini vyotee ambavo mpaka kufika mwisho wa utumbo mdogo (appendix) vinakua vilaini

Lakini kama hauwez hakikisha mlo wako una papai ndani yake wowote ule utapata Choo laini kabisa

Baada ya huo muda unaweza kula chochote
 
Mi niling'oa tu jino huu mwezi wa 5 sasa nahisi kuna ka u sensitive fulani kwa mbali nikigusa na ulimi , wewe operation ina wiki mbili unakuja kuomba ushauri jf ? For real mkuu? Kama unaipenda afya yako basi fanya kuwauliza madktari husika , napendekeza hospitali uliyofanyiwa operation.
Wakinikera sana niliwaambia vyakula gani etii vilaini , kila siku ndizi , uji, chai , sasa hivi vigumu km nyama nisile, kasamaki kakukaangwa nisile ? Wangenipa mtiririko wa vyakula ingependeza.
 
Mkuu kwa appendix mara nyingi wanatumia nyuzi ambazo ndani ya siku 7 mpaka 14 inakua Ishayeyuka mwilini ivoo ndani ya siku 7 mpaka 14 kula vyakula laini vyotee ambavo mpaka kufika mwisho wa utumbo mdogo (appendix) vinakua vilaini

Lakini kama hauwez hakikisha mlo wako una papai ndani yake wowote ule utapata Choo laini kabisa

Baada ya huo mda unaweza kula chochote
Ahsante kwa ushauri wako ,
 
Back
Top Bottom