Nitumie viuatilifu gani kupalilia mahindi?

grand casual

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
255
155
Wakuu habar za jioni! nahitaji msaada wa dharura kwa wenye uzoefu. Naomba kujulishwa ni aina gani ya kiuatilifu naweza tumia kupalili mahindi ambacho kinaangamiza ndago na nyasi?, nilitumia 2,4 D haikusaidia kitu msaada tafadali
 
Tumia dawa inaitwa Stellar Star: Inapatikana kampuni ya Bytrade mikocheni njia ya cocacola, osifi ipo karibu na zilipokuwa ofisi za majembe.
 
2-4D inaua magugu au mimea yenye majani mapana (broad leaf weeds). Ni dawa inayochagua magugu (selective herbicide) kwa hiyo haiui mimea ya jamii ya nyasi. Kwa hiyo 2-4D inatumika kwenye mazao yanayopandwa karibu karibu mfano ngano, mpunga,nk kwa sababu huwezi kuepusha dawa kugusa mazao. Kwa hiyo dawa yenyewe inachagua iue mmea gani. Ndio maana nyasi na ndago zimeendelea kupeta baada ya kunyunyizia. Unaweza kutumia gramoxone (paraquat) au hata Stellar star. Stella star ni selective lakini inaokoa mahindi na miwa tu na kuua mimea mingine yote. Kuna dawa zingine zinazitumika baada ya kupanda kabla mimea haijaota mfano primagram.
 
Thank you Sana mkuu
 
tumia MAGUGUMA...ila kusiwe na maharage kwa shamba! au tumia NICOFURAN( km sijakosea spelling zake mkuu)..ni nzuri sana sana.inaua ndago na nyasi aina zote!
 
Back
Top Bottom