Nitumie dawa gani mpenzi wangu aniache automatically?

Nitumie dawa gani mpenzi wangu aniache automatically?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,432
Nina mpenzi ambaye ananipenda sana (mi nazuga tu kwqmba nampenda, licha ya kwamba Zamani nilikuwa nampenda Sana). Kwa kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo upendo wake kwangu unavyozidi kuongezeka huku wa kwangu ukizidi kuyeyuka na kupoteza kabisa.

Binti wa watu kaacha dini yake kaja kwangu, alikuwa ni kada kindakindaki wa kile chama cha mashetani, kaachana nacho na Sasa hakitaki Tena, sio kwa Sera za chama ila kwasababu tu aufurahishe moyo wangu.

Kanitambulisha kwao, Mimi kwetu sitaki hata wamjue. Sasa nimechoka kufeki lavu andi laifu. Nifanyeje ili binti aniache automatically? Je nitumie dawa gani? Niogee chumvi ya mabonge ya Mshana Jr? Mbona nahisi Kama itaniongezea mivuto? Sitaki kumfanyia visa, nitakuwa nauumiza moyo wake.

Sitaki kumchana makavu, kabinti presha yake inashukaga Hadi anazimia siku tatu. Naombeni ushauri wajameni nifanyeje ili niachwe mie?
Nahitaji kuachwa, nahitaji kuachwaaaaaa, nahitaji kuachwaaaaaa (kwa sauti ya Nireeeteeeeni Gwajimaaaaaa)
 
Anza kupunguza mawasiliano,punguza mikutano nae taratibu sometime akikutafuta usipokee simu mjibu baadae sana!.. fanya Kama upo bize kindakindaki haswaa.. akikuita mjadili msikilize ila usitende atakavyo muwache na malalamiko yake!.. Kama hayo huyawezi ipo njia nyengine nyepesi!.. nitumie namba yake atakuacha yeye mwenyewe.. mkuu si anaomsambwanda au hana..??
 
We muombe ndogo asipokuacha ujue huyo ni wako huchomoki
Anza kupunguza mawasiliano,punguza mikutano nae taratibu sometime akikutafuta usipokee simu mjibu baadae sana!.. fanya Kama upo bize kindakindaki haswaa.. akikuita mjadili msikilize ila usitende atakavyo muwache na malalamiko yake!.. Kama hayo huyawezi ipo njia nyengine nyepesi!.. nitumie namba yake atakuacha yeye mwenyewe.. mkuu si anaomsambwanda au hana..??
KENZY, huko ndio kumuumiza moyo kwenyewe, sitaki aumie
 
Kweli maombi ya matajiri na masikini yako tofauti kabisa. Bill Gates anaomba Mungu ampe technology ya juu zaidi, sisi twaombea mapenzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom