Nitoke nje ya ndoa?

Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
948
1,000
Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa!

Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na Mungu wangu!

Nimesali sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je, nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25. Kwakweli sijitambui niko njia panda!

Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2 nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!

Sijielewi nahisi naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,

Nina uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!

Hapa najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani inatosha.

Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?
 

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
2,000
25 WAKIUME NA UMEOAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!????????? Damn!!!!!! YOU ARE PATHETIC INDEED!!!!!!!

Itakuwa alikubli umuoe KIMASLAHI sasa umemfika kooni, wamchefua nafsi. (Ngoja niishie hapa kukupa makavu maana na hizo stress hushindwi kujitundika na shuka! Mmhhhhhhhhhh!(Mguno wa kinafiki.)

Anyway hapo dawa we mrudishe kwao kwa muda, akisha test maisha bila wewe kidogo, MAYBE anaweza kjirudi na kukuheshi na kuacha tabia ya kukukoa mikwenzi.

NDOA ZA UTOTON ZINASUMBUA SANAAAAAAA! Thats why nangoja till i am at least 40 ndo nianze kuconsider kuingia.
 

tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,011
2,000
Kisa cha kuoa mapema nn.?? Pole wee..uliingia akili ikiwa haijakomaa c bure...wenzio wanaoa wakiwa 30 akili zishakomaaa
 

WISE BOY

JF-Expert Member
Dec 26, 2011
782
195
majaribu 2013 again, huishiwi hadithi za visa vya ndoa. Na mpaka unaingia kwenye ndoa "4 real" utakua umepata uzoefu wa kutosha
 
Last edited by a moderator:

Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
948
1,000
25 WAKIUME NA UMEOAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!????????? Damn!!!!!! YOU ARE PATHETIC INDEED!!!!!!!

Itakuwa alikubli umuoe KIMASLAHI sasa umemfika kooni, wamchefua nafsi. (Ngoja niishie hapa kukupa makavu maana na hizo stress hushindwi kujitundika na shuka! Mmhhhhhhhhhh!(Mguno wa kinafiki.)

Anyway hapo dawa we mrudishe kwao kwa muda, akisha test maisha bila wewe kidogo, MAYBE anaweza kjirudi na kukuheshi na kuacha tabia ya kukukoa mikwenzi.

NDOA ZA UTOTON ZINASUMBUA SANAAAAAAA! Thats why nangoja till i am at least 40 ndo nianze kuconsider kuingia.

Lara 1, shida siyo umri wala kumchefua ndugu yangu, mi sina masilahi amenipenda nikiwa sina kitu. Nina miaka michache lakini busara yangu kubwa saana, nimepewa uchungaji wa makanisa makubwa sana Dar nikakataa! Nadhani huyu mwanamke atakuwa jini maana anapata kila aina ya care, ukisema yale mambo yetu ndo kabisaaa hapa amefika! Nimesikia.pia aliachika tena miaka ya nyuma duh
 

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,504
2,000
pole sana ndugu, shirikisha ndugu wa pande zote
lakni sijajua hasa matatizo ya huyo mkeo mpaka mnashindwa kuelewana
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
umetibua wapi? Lazima kuwe na sababu zinazopelekea mkeo kufanya hvi. Kumuulza mwenyewe haitosh shrkisha na watu wengne
 

kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,608
2,000
mmmh pole maana,na hiyo safari bado ni ndefu,ki ukweli sometimes affair zinasaidia kuimarisha ndoa{ingawa sio kwa kila mtu}na sometimes zinaweza kuvuruga kabisa,zinasaidia kivipi,kama mke kweli ana matatizo na akija gundua una mtu mwengine,na ukimuelezea sababu ya yeye kufanya hivyo inampa funzo kuwa alaa hata kama hana kitu yupo ambae yupo tayari kuwa na relationship nae,mke atajishusha.ila kama huyo mke na yeye amekuchoka hiyo itampa sababu na yeye kufanya yake.ila mambo ya ndoa haya ni vizuri story uzisikie pande zote 2.
 

Ben Mugashe

JF-Expert Member
Oct 9, 2008
998
1,000
25 WAKIUME NA UMEOAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!????????? Damn!!!!!! YOU ARE PATHETIC INDEED!!!!!!!

Itakuwa alikubli umuoe KIMASLAHI sasa umemfika kooni, wamchefua nafsi. (Ngoja niishie hapa kukupa makavu maana na hizo stress hushindwi kujitundika na shuka! Mmhhhhhhhhhh!(Mguno wa kinafiki.)

Anyway hapo dawa we mrudishe kwao kwa muda, akisha test maisha bila wewe kidogo, MAYBE anaweza kjirudi na kukuheshi na kuacha tabia ya kukukoa mikwenzi.

NDOA ZA UTOTON ZINASUMBUA SANAAAAAAA! Thats why nangoja till i am at least 40 ndo nianze kuconsider kuingia.

Ahaha acha zako...kijana ameoa ww unamtisha..tatizo hivi vibinti vya facebook vinataka kula bata sana na vinajua ukiolewa kila weekend ni dinner na nyama choma, swali langu kwa kijana: ndoa yako ni ya dini gani? Kama za kwetu mKristo imekula kwako mdogo wangu huyo wako mpaka kifo kiwatenganishe, Na ww kubwa la maadui umezeeka sana kwa umri wako ulibidi uwe na mjukuuu ahahahhhahah
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
910
500
pole kwa yaliyo kupata hayo ni mapito tu..vip katika ndoa yenu umefanikiwa kupata mtoto???
cha msingi hapo mrudishe kwao.ili mpeane muda wakila mtu kujichunguza au kumchunguza mwenzake wapi alipo kosea.baada ya kujua tatizo tuliza akili yako na ujue yataisha kisha washilikishe wazee wenu iliwawape muongozo wa nini cha kufanya.usiwaze kabisa kutoka nje ya ndo maana ni hatali kwa afya.na uchumi kwa ujumla au utajikuta unaumia zaid ya hapo..
 

WISE BOY

JF-Expert Member
Dec 26, 2011
782
195
By WISE BOY<br />
<b><a href="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=129062" target="_blank">majaribu</a></b> 2013 again, huishiwi hadithi za visa vya ndoa. Na mpaka unaingia kwenye ndoa &quot;4 real&quot; utakua umepata uzoefu wa kutosha
<br />
<br />
Sasa mbona unadhani ni story nakuambia kitu cha kweli!
Mmh, we majaribu, huyu ni yule mliyeoana miaka mi4 iliyopota anayenuna bila sababu? Inamaana ulioa ukiwa na miaka 21? Acha visa bwana
 

Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
2,000
Mwanamke aliachika? Ulijua kilichomtoa kwa mumewe wa kwanza? Historia ya huyo mwanamke unayo?...btw...man umewahi eeeh? Halaf kingineee ukaacha na kazi kabisa? Halafu visa vyenyewe mbona huvielezei?unasema tu una matatizo ila naona kama hujafunguka ki-sawasawa
 

Ablessed

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
4,616
2,000
Kwa maelezo yako inaonyesha wewe ni muumini wa makanisa a kiroho. Nataka niamini kwamba wewe unaimani kubwa kwa Mungu na ndio maana unasema umesali weeeeee lkn mambo bado magumu. Nashindwa kuelewa kwanini mtu mwenye imani kwa muumba wake awe na mawazo ya kutoka nje ya ndoa. Yawezekana kweli mkeo ana matatizo lkn bado sio njia ya wewe kutamani kuanzisha mahusiano mapya. Bado jibu lako utalipata kwenye maombi ukiomba kwa moyo lazima kitaeleweka tuuuu kwani Mungu si mwanadamu hata aseme uongo.

Je umejaribu kuzungumza na mwenzako hayo yanayokukera na mkakosa muafaka. Kwa nionavyo mimi ni vema mkakaa na kujadili muskabali wa maisha yenu na kama mnaona mambo hayaendi basi mwaweza amua otherwise. Inawezekana mwenzako ana mtu au na yeye amekata tamaa alivyotegemea sivyo sasa hali hiyo imemchosha . Mkikaa kwa mazungumzo mtajua iwapo mtaamua kuwa wawazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom