Nitazipata wapi hizi hadithi zilizowahi kuvuma kwenye majarida?

Hadithi moja nilikuwa nafuatilia sana
KISIKI CHA MPINGO (huyu mzee ni noma sana). Hawa jamaa walikuwa wanajua kutunga sana.
Kuna ile timu ya bush stars ya Mapung'o. Uncle wangu alikuwa anapenda sana kusoma, namim nilikuwa navizia akimaliza kusomašŸ“°
 
Sijakuelewa

Huawezi kuelewa mkuu miaka ya 80s mabati yalikuwa yanaprintiwa ukinunua mabati unaweza kukuta limeprintiwa habari za gazeti la mfanyakazi au mzalengo au sani,watu waliozaliwa 60s,70s,80s wanaweza kujua.
 
Dah hicho kitabu cha pili pilipili nakitafuta sana jamani hakuna msaada naweza pata tafadhali toka kwako mkuu.
 
Dah hicho kitabu cha pili pilipili nakitafuta sana jamani hakuna msaada naweza pata tafadhali toka kwako mkuu.
Tatizo uaminifu mkuušŸ˜”šŸ˜”,.kuna member humu mpaka leo ana vitabu vyangu hajanirudishia tangu nimuazime,. tena ni vitabu aliniachia marehemu uncle wangu siwezi kuvisahau aisee ni vya mwandishi James Hadley Chase,.
 
mzee Kisiki mchawi kinoma, alikuwa anapambana sana na Bibi Chonjoluchonya


Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
samahani, mimi ni mmoja wa wapenzi mno wa riwaya hizi, mfano usiku wa balaa, msako wa hayawani, pesa zako zinanuka ,tutarudi na roho zetu n,k. nina mengi ya kukumbuka, nazipataje tafadhali
 
Inaitwa Anga za Wenyewe, chini ya mtaalam Fortunatus (4T) Ndilla.. sijui yuko wapi huyu mwamba ila heshima yake popote pale alipo! Alikuwa mchoraji smart sana, baadaye akaja Abdulrahman Dohu, naye alikuwa mtata ila si kama 4T Ndilla.
Nasikia alifariki, sijui ni kweli?
 
Anga za wenyewe hiyo
 
Blaza hicho Cha simu ya kifo hata ukiscan unitumie ntakushukuru milele, nilikisoma nikiwa Darasa la pili mwaka 1994 sijakisahau Bado nakumbuka Kuna Agnes na FAMBO
 
Mlinzi wa zamu, anga za wenyewe, Dunia iliyooza, Pablo zungu, mamdogo, nesi mtalamu. Acheni nyie nyuma raha
 
Bulicheka na mkewe Elizabeth.
Lila na fila.
Adili na nduguze
Mashimo ya mfalme suleyman humu yumo yule mwamba umsolopagaz mwana makumazhan
Yohana mjinga
Hadirhi za esopo
Mpiga firimbi wa Hamelin
Mwamba Abunuwas

Kikomo
Njama
Kufa na kupona
Hivi ni baadhi ya vitabu miaka ya 80 vilinihamasisha sana kujisomea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦