Nitazipata wapi hizi hadithi zilizowahi kuvuma kwenye majarida?

Hadithi moja nilikuwa nafuatilia sana
KISIKI CHA MPINGO (huyu mzee ni noma sana). Hawa jamaa walikuwa wanajua kutunga sana.
Kuna ile timu ya bush stars ya Mapung'o. Uncle wangu alikuwa anapenda sana kusoma, namim nilikuwa navizia akimaliza kusoma📰
 
Sijakuelewa

Huawezi kuelewa mkuu miaka ya 80s mabati yalikuwa yanaprintiwa ukinunua mabati unaweza kukuta limeprintiwa habari za gazeti la mfanyakazi au mzalengo au sani,watu waliozaliwa 60s,70s,80s wanaweza kujua.
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
Dah hicho kitabu cha pili pilipili nakitafuta sana jamani hakuna msaada naweza pata tafadhali toka kwako mkuu.
 
Dah hicho kitabu cha pili pilipili nakitafuta sana jamani hakuna msaada naweza pata tafadhali toka kwako mkuu.
Tatizo uaminifu mkuu😔😔,.kuna member humu mpaka leo ana vitabu vyangu hajanirudishia tangu nimuazime,. tena ni vitabu aliniachia marehemu uncle wangu siwezi kuvisahau aisee ni vya mwandishi James Hadley Chase,.
 
Hadithi moja nilikuwa nafuatilia sana
KISIKI CHA MPINGO (huyu mzee ni noma sana). Hawa jamaa walikuwa wanajua kutunga sana.
Kuna ile timu ya bush stars ya Mapung'o. Uncle wangu alikuwa anapenda sana kusoma, namim nilikuwa navizia akimaliza kusoma
mzee Kisiki mchawi kinoma, alikuwa anapambana sana na Bibi Chonjoluchonya

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
samahani, mimi ni mmoja wa wapenzi mno wa riwaya hizi, mfano usiku wa balaa, msako wa hayawani, pesa zako zinanuka ,tutarudi na roho zetu n,k. nina mengi ya kukumbuka, nazipataje tafadhali
 
Inaitwa Anga za Wenyewe, chini ya mtaalam Fortunatus (4T) Ndilla.. sijui yuko wapi huyu mwamba ila heshima yake popote pale alipo! Alikuwa mchoraji smart sana, baadaye akaja Abdulrahman Dohu, naye alikuwa mtata ila si kama 4T Ndilla.
Nasikia alifariki, sijui ni kweli?
 
Kuna ile hadithi ilikuwa gazeti la bongo. George ni mpelelezi hatari. Kubwa la majamba likamtuma mrembo Vicky akajitongozeshe na kummaliza George. Vicky kamfananisha Raymond na George na kuzama penzini. Niliipenda sana.

Vitabu vingi Ulaya, hasa vya zamani vilianza kama series za magazetini.
Anga za wenyewe hiyo
 
Namshukuru mamangu ni mpenzi wa kusoma vitabu, magazeti, majarida n.k huwezi amini mpaka leo hii hivyo vitabu vipo ni mtu ukijisikia kujikumbusha unaenda kwenye library yake unachukua na kuburidika, mpaka magazeti ya jitambue na mshauri wako yapo mpaka leo hii na ukiyasoma bado yana ladha taam,.kwa hakika vya kale dhahabu.

Mfano vitabu vya marehemu H.H Katalambula na watunzi wengine mashuhuri ambavyo vipo hapa:
Lawalawa, pili pilipili, najisikia kuwa tena, simu ya kifo,msako wa hayawani, hofu, aisee ni vingi mnoo
Blaza hicho Cha simu ya kifo hata ukiscan unitumie ntakushukuru milele, nilikisoma nikiwa Darasa la pili mwaka 1994 sijakisahau Bado nakumbuka Kuna Agnes na FAMBO
 
Habarini wana jamvini?

Nilikuwa msomaji mzuri sana wa majarida ya mwezi kama Bongo, Sani na Tabasamu. Ndani ya haya majarida kulikuwa na riwaya nzuri sana za kusisimua kama MUSAKO WA HAYAWANI, MSAKO WAMR X (riwaya za Eddie Ganzel, na baadae Ray Ganzel ktk jarida la Bongo), DAMU NZITO ya Amri Bawji kwny jarida la Sani.

Na hata kwenye jarida la Tabasamu kulikuwa na mtunzi maarufu wa riwayaa ajulikanae kama Emmanuel P. Ndonde alikuwa akitunga hadithiza wapelelezi maarufuakina Micky Reuben na Dick Masamba (kama sijakosea).

Hizo ni baadhi ya hadithi nazozikumbuka, zipo nyingi tu zilizowahi kutungwa na kuchapishwa kwny majarida hayo..kuna baadhi ya hadithi za michoro chini ya wachoraji maarufu kama Fortunatus Ndilla (mtaalam), John Mohamed Kaduma(R.I.P), Aloyce Jacob, Daud Masasi n.k walitunga hadithi za michoro kama, Mlinzi wa zamu, Anga za wenyewe, Hofu ya vizito, hadithi za akina mzee ole, obi, linda n.k.

Hiyo ilikuwa ni miaka ya tisini katikati mpaka alfu mbili mwanzoni, magazeti haya yalikuwa maarufu sana. Nilikuwa mdogo kipindi hicho lkn nilikuwa navizia kwa majirani walionunua nami naazima.

Kwa kipindi cha hivi karibun nimekuwa nikipita k'koo kwa wauza vitabu, majarida na magezeti kubahatisha kama wanaweza kuwa na vitabu vya hadithi hizo. Nilibahatisha kupata kimoja tu cha MSAKO WA HAYAWANI.

Je hakuna utaratibu wowote wa kuwashauri watunzi au wamiliki wa hizi hadith wakachapisha kitabu kimoja kila hadithi na kuviuza?.. Maana hadithi hizi zilikuwa nzuri sana na zenye kufundisha.
Mlinzi wa zamu, anga za wenyewe, Dunia iliyooza, Pablo zungu, mamdogo, nesi mtalamu. Acheni nyie nyuma raha
 
Bulicheka na mkewe Elizabeth.
Lila na fila.
Adili na nduguze
Mashimo ya mfalme suleyman humu yumo yule mwamba umsolopagaz mwana makumazhan
Yohana mjinga
Hadirhi za esopo
Mpiga firimbi wa Hamelin
Mwamba Abunuwas
Kikomo
Njama
Kufa na kupona
Hivi ni baadhi ya vitabu miaka ya 80 vilinihamasisha sana kujisomea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom