Nitawezaje kuishi na mtu aliyeathirika

Mar 11, 2007
16
1
Naomba kufanunuliwa namna ya kuishi na mtu aliyeathirika na virusi vya ukimwi au mgonjwa wa ukimwi bila kuonyesha kumnyayapaa,mfano namna ya kufua nguo zake,kuchangia vyombo vya kuogea na vya kulia chakula nk.
 
Mie si mtaalamu wa fani hiyo, madaktari wako humu watachangia zaidi, lakini mie nina haya machache ya uzoefu wangu wa kimaisha (of course mengi nimeyasikia kwa hawa wataalamu wa afya pia).
1. Kwanza hakuna tatizo katika kuchangia naye vyombo vya chakula, unaweza tu kuviosha kama kawaida kama unavyoosha siku nyingine, wala hakuna ulazima wa kumtengea vyombo vyake mwenyewe. Isipokuwa kama ameshakuwa na hali mbaya ana vidonda mdomoni na vyombo anavitapikia, ni vema kuviloweka kwenye dawa kabla hujaviosha.
2. Kuhusu kuoga, inategemea hali ya mgonjwa. Kama ana vidonda vibichi mwilini, utashauriwa namna ya kumchanganyia maji ya dawa kwa ajili ya kumwogesha, lakini hakikisha unavaa golves mikononi unapomwogesha, maana usipofanya hivyo una hatari ya kudhurika. Kama unatumia body brush au dodoki kumsugua hakikisha unalitenga hilo mtu mwingine asitumie.
3. Hakikisha pia vitu kama mswaki wake havichaganyiki na vya wengine mtu mwingine asije akautumia kwa bahati mbaya, hasa kama mnaishi familia kubwa kwenye nyumba ndogo.
4. Nyembe zake anazonyolea hakikisha zinatupwa mahali ambako watoto hawawezi kuzipata wakachezea, labda kwenye choo cha shimo au shimo kubwa la taka ambako watoto hawafiki kuokota vitu vya kuchezea.
4. Vitu unavyotumia kumtibia kama vile vitambaa laini vya kufungia vidonda, pamba za kuoshea vidonda, gloves zilizotumika, hakikisha unavichoma moto kabisa hadi majivu vinapotoka mwilini mwake, maana watoto wanaweza kuviokota na kuchezea, matokeo yake wanaathirika.
5. Nguo zake, kama ni mkavu hana vidonda mwilini, waweza tu kuzifua pamoja na nyingine kama kawaida. Lakini kama ana vidonda, ama amefikia hatua mbaya anajiharishia, hakikisha nguo hizo umeziloweka kwenye dawa kama JIK kwa muda usiopungua masaa 3 kabla ya kuzifua, na ukiweza kupata ile mipira migumu ya kuvaa mikononi (huwa ni mirefu, wanatumia sana madobi), itakuwa salama zaidi kwako.

Kama ni mwathirika tu wa HIV ambaye hajaonesha dalili yoyote, hana vidonda wala hajiharishii, unaweza kuishi naye tu kawaida kama unavyoishi na wengine bila kulazimika kuchukua tahadhari hizo hapo juu, isipokuwa kwa mambo ya miswaki na vitu kama wembe na sindano. Kama ni mwenzio wa ndoa, basi hakikisha mnatumia kondomu siku zote na kwa kila tendo la ngono.

Hata kama mgonjwa ana vidonda, bado si hatari kukaa naye sebuleni au chumbani, kuzungumza naye, na kula pamoja, kwani huwezi kuambukizwa kwa njia hizo.

Hayo ndio yangu machache, huku pia kuna madaktari na wauguzi, hebu jitokezeni mumshauri mwenzetu.
 
Naomba kufanunuliwa namna ya kuishi na mtu aliyeathirika na virusi vya ukimwi au mgonjwa wa ukimwi bila kuonyesha kumnyayapaa,mfano namna ya kufua nguo zake,kuchangia vyombo vya kuogea na vya kulia chakula nk.

Naungana na Kithuku,
ila mimi nashauri, tahadhari zaidi si katika wagonjwa wa ukimwi tu ambao wameshajulikana, ila kwa wale ambao bado hatujui status zao. Kitu nilichokiona katika jamii ni kuwa mgonjwa yule yule ambaye aamekuwa akiugua mara kwa mara, akitibiwa hiki na kile, familia huwa haimbagui na wala ikamnyanyapaa, ila ikatokea akapimwa na kuwaconfirmed kuwa ana VVU (pamoja na kuwa alikuwa ashaonyesha dalili kitambo) mambo hubadilika, ndio wataanza safe precautions etc.Mimi binafsi,'bado' naogopa wagonjwa wa 'UKOMA' kuliko wenye 'UKIMWI'.
 
shukrani kwenu Kithuku na Kasana kwa msaada wenu nimepata mwanga.keep it up!

Kwa kuongezea. Ukimwi ni sexually transmitted diseases (STD). Na unaambukizwa kwa njia ya ngono au kupewa damu ya mtu aliyeathirika.

Hivyo kama huna mahusiano ya ngono na mwathrika hakuna sababu ya kuogopa.
 
Back
Top Bottom