Nitawashangaa CHADEMA kushiriki chaguzi zinazokuja.

Gosheni

Senior Member
Oct 28, 2008
199
138
Ninania ya kuwasilisha kinacho nikereketa, japo sipo vizuri ila natumaini mtanielewa.

Tmeshuhudia namna chaguzi za 26nov zilivyoendeshwa na kufanyika pamoja na kisimamiwa.

Kwa namna nilivyoutathimini uchaguzi huu ni sawa na pambano la mabondia ulingoni, bondia mmoja kafungwa kamba mikono na miguu na kisha kufungwa kwenye nguzo, ili hali asimu wake akiwa mwenye afya tele na nguvu tele bila kufungwa na kitu chochote, wanapambanishwa.

CCM kwa kutumia kamba ambazo ni jeshi la polisi, refarii tume ya taifa, hawaa ndio walitumika ili kuhakikisha ushindi wa CCM. Kila mwenye akili timamu asingefurahia kuyaona yaliyotokea katika uchaguzi huu, ambapo watu wasio kuwa na hatia, wameuwawa, wengine kupewa ulemavu wa kudumu kwa kukatwa na mapanga, shoka na marungu bila kusahau mawe, na wengine wamewekwa mahabusu bila sababu yoyote. Yote haya ni kwa raia anayetimiza wajibu wake wa kikatiba.

Mara nyingi nimekuwa nikiwasikia viongozi wa upinzani wakiwahimiza wanachama wao kulinda kura baada ya kupiga. Hili neno la kulinda kwa majira haya si ya kuwatakia amani wanachama wetu, kwakuwa CCM wametoka kwenye kuiba kura mpaka kufikia hatua zaidi ya kupora, kwa bahati mbaya nimekosa neno lilozaidi ya kupora, hapa kinachotumika sio kuchukua kwa kificho, nikuchukuwa kwa uwazi na ukiwa king'ang'anizi mapanga yana kuhusu. Tumapo wataka wanachama walinde kura wakati huohuo viongozi wamejificha mbali sio sahihi.

Nimesoma maandiko ya Lema namna uchaguzi ulivyoendeshwa, akielezea alivyojificha kwenye gari ilihali mwanachama wake akipokea kipigo, nimesoma pia Mbunge Lijuakali kakimbia mahali pasipo julikana.

Uongozi wa awamu ya tano hautaki tena kushindana kwa hoja, wala hawataki upinzani kwa namna yoyote ile, wao upinzani ni uwadui, sio mawazo mbadala. Ndio sababu walitaka kumuuwa Lisu.

CHADEMA msishiriki chaguzi zinazo kuja bila kutueleza mtakabiliana vipi na hali iliyopo sasa. Mtuambie mtahakikisha vipi hamzurumiwi ushindi wenu bila ya kuweka maisha ya wanachama wenu rehani?

Sababu kwa nini msishiriki.....

1. Kujali maisha ya wanachama wenu, kwa kuzingatia kuwa kwenye uchaguzi huu baadhi ya wanachama wenu wa mefariki na wengine kupata ulimavu wa kudumu.

2. Msitunike kuhalalisha uovu wa CCM, kushiriki inahalalisha uchaguzi hata kama kanuni zimekuikwa.

3. Kuutangazia ulimwengu, mambo yanayoendelea Tanzania ya kuwa ni kinyume na haki za binadamu.
 
Wewe umwambieMbowe aache kugombea Hai ili aendelee na Cheo chake Kiongozi wa Upinzani Bungeni atakuelewa kweli?
 
Sio kushiriki tu...!mi naona kife kabisa ili kije chama kingine ambacho kitakua serious kupinga ufisadi ,Rushwa na kusimamia maadili mema kwa viongozi wake .CDM hii inapoteza kabisa matumani ya wapinzani wa kweli.CDM hii inatuacha njia panda kwenye vita ya ufisadi..
 
Back
Top Bottom