Nitauvunja vunja moyo wake soon

Nitauvunja vunja moyo wake soon

kwanza kabisa niseme sikuwa na nia hii ila itabidi, siyo kosa lake tatizo ni mimi.

Huyu binti nilikutana nae mwezi may, mwaka huu, nilitokea kumtamani na kutamani kuwa nae hata kwa usiku mmoja tuu, nilifanikiwa kupata namba yake na kuanza mawasiliano.

Date ya kwanza ilienda vizuri na nilimrudisha anapokaaa salama baada ya kufurahi usiku kucha, kukaa nae na kuongea nae usiku huo nikatokea kumpenda, sikufanya nae mapenz aliniambia yupo period mapema na nilimkubalia.

Baada ya hapo kaja kwangu mara nyingi sana, tunapika na kula, na siku nyingine analala baada ya kumsikiliza story yake na malengo yangu nikaona kabisa hatupo njia moja...alikuwa ametoka kuachwa na mshkaji wake baada ya kimtoa usichana, alikuwa kwenye maumivu makali nikachukua jukumu la kumpa faraja kuhakikisha hata mitihan yake anafnya vizuri. ishu ni kwamba mtoto amenielewa na mipango yake yote ni mimi! Mimi mipango yangu ni mama mtoto ambaye natarajia kufunga nae ndoa mwezi december.

Nimefanikiwa kwa kiasi fulani kuishi double life, mke wangu mtarajiwa alishajua kuhusu huyu binti tukayamaliza, ila binti hajui chochote kuhusu kuwa na mke wala mpango wa ndoa. Last month nilimletea figisu tuachane akaniambia ntakuwa responsible kwa atakachokifanya hawezi kuishi, nikarud nyuma.

Msinitupie mawe wakuu, naombeni ushauri nini cha kufanya kwa sasa, namna gani nimuache asiumie, binafsi ninampenda pia yani ninawapenda wote yeye na mke mtarajiwa. Kuoa ni lazima nioe mwezi wa 12
huu uzinzi utakugharimu mda si mrefu,kwenye ndoa unayo enda kufunga.
mwambie dad wa watu ukweli usimpotezee muda na umuombe msamaha na ajue kabisa unaenda kufunga ndoa mwezi wa 12 ni kesho kutwa tu we bado unaangaika na wadad wengine uku nje huyo akutosherezi unae enda kumuoa?
ushawahi kujiuliza ingekuwa mwanaume mwingine anafanya hayo na moja kati ya hao wanawake angekuwa dada yako?
 
Mkuu kama unamtu mwingne unampenda na unatarajia kuoa,huyo mwingne mwambie tu ukweli umuache mkuu,ila jua tu kuwa itamuumiza

But mpe tu ukweli nw.
 
Kudadadeki sisi wengine tunatafuta wa kuoa kumbe nyinyi ndio mnatuzibia kila tukigonga mlango tunaambiwa una mtu
Wachukue wote pumbaafu
 
Mshika mawili moja humponyoka..ndio tatizo la kupenda wote hao...Focus kwa mmoja kwanza mkuu
 
Nitumie namba ya huyo dada inbox ili nikusaidïe. Maana ntamwambia jamaa uliyenaye ana mke ila anakuzingua tu.

Atakubali tu.
Fanya hivyo tafadhari
 
Una mke mtarajiwa alafu unapata short gun alaf unaipeleka home kwako!unatarajia nin?Bado haujakua mwanaume Wakuiongoza family ijayo!utaipa mateso sana!
 
Yaan wew unawapenda wote,alafu unaomba ushauri wa nn sasa mkuu,kuchepuka ni matokeo ya kuongezeka kwa kipato cha ziada ,naona uko na uwezo oa wote tu
 
Tatizo ulilitengeneza mwenyewe halafu limekuzidi mwenyewe. Peleka kwa Mange Kimambi
 
Peleka taarifa polisi. Akifa, afe bure....

Atapigwa Warning.
 
Back
Top Bottom