Nitatumia njia ipi ili arudi nyumban

Nitatumia njia ipi ili arudi nyumban

Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
13,286
Reaction score
13,460
Pole kwa majukumu ya kila siku wanaJF. Nimejitokeza kwenu kuomba ushaur! Nilikuwa na baba yangu mdogo alienda nje ya nchi kutafuta maisha akawa anaishi nchini Sierra leone amekaa huko kwa kipindi kirefu sana akafanikiwa kuwa na familia hukohuko japo hatukuwa na mawasiliano ya mara kwa mara. Mnamo mwaka 2009 akapatwa na umauti kutokana na vurugu za kisiasa nchin humo baada ya hapo familia yake yote ikawa imesambaratika na haijulikani kama wameshauwawa au wako wapi! Sasa kuna mtoto wake mmoja wa kiume alibahatika kuokolewa na akawekwa kwenye kambi ya wakimbizi nchi Senegal amekaa kambin humo toka 2009 mpaka sasa anaishi humo. Sasa mwezi wa 6 mwaka huu ndo tukapata taarifa kuwa mtoto wa marehem baba mdogo yupo kwenye kambi ya wakimbizi nchini Senegal nimejitahidi kutafuta mawasiliano nimepata namba ya sim na nawasiliana naye.....sasa naombeni ushauri nichukue hatua gan ili niweze kumrudisha Tanzania kwasababu analalamika sana anasema maisha ya kambin humo nisawa na Jela wananyanyaswa sana
 
nadhani ungeenda wizara ya mambo ya nje wanaweza kukusaidia
 
Samahani kaka naomba nikuulize maswali machache, huyo mtoto ni wa kike au wa kiume, pili ni yeye aliwatafuta au ni nyinyi mlimtafuta, umewahi kusikia utapeli wa wanaijeria kujifanya wapo makambini Senegal? Ukinijibu nitakusaidia kaka yangu kama huyo mtu ni Genuine!
 
Samahani kaka naomba nikuulize maswali machache, huyo mtoto ni wa kike au wa kiume, pili ni yeye aliwatafuta au ni nyinyi mlimtafuta, umewahi kusikia utapeli wa wanaijeria kujifanya wapo makambini Senegal? Ukinijibu nitakusaidia kaka yangu kama huyo mtu ni Genuine!

huyo mtoto ni wakiume yeye ndio alitutafuta kwasababu kipindi cha uhai wa babayake tulikuwa tunawasiliana japo mara chache tulikuwa tunawasiliana kwa email na simu lakn baada ya kifo chake mawasiliano yakakatika. Na huyo mtoto wake alitutafuta kwa email ndo tukapeana namba za sim
 
Usiwe umepata ile email ya kuomba msaada kurudi Tz, wengi wanatokea huko.
 
Back
Top Bottom