Kuna mtu huwa ananitumia Messages, mara ananisalimia, mara ananiambia forward kwa watu hamsini utabarikiwa, messages kibao zingine hazina kichwa wala miguu. Nikijaribu kuchunguza, kwa kweli hiyo namba ni ngeni, kwa maana kwamba kama vile sikupeana na mtu. Kila nikimpigia hapokei, nikikaa kidogo sms, ananiudhi! Siku moja nilimsms kumwuuliza wewe nani? Akanijibu una haraka ya nini, utanifahamu tu!
Nikaona niachane naye, maana huu ni wehu, nisubirie kumfahamu ili iweje hali ananisumbua na messages zake. Nikawa nimesave jina lake kwenye simu "Who?", halafu kila akituma sms nadelete bila kuisoma.
Sasa tulikuwa na mazungumzo sehemu ambapo niliamua kuweka simu yangu katika silence mode. Hata nilipoondoka hilo eneo la mazungumzo nilisahau kuondoa silence mode kwenye simu, nikawa natembea kwenda nyumbani. Kumbe huyo mtu ambaye hunitumia sms za ajabuajabu, akawa amenitumia picha WhatsApp ambayo kwa kweli siwezi kuielezea, imeambatana na ujumbe "karibu Apple, samahani lakini".
Kwa bahati mbaya nikiwa natembea huku simu ikiwa kwenye mfuko wa suruali, hiyo message ikawa imejituma kwenda kwa watu kadhaa akiwemo Boss wangu (ni mwanamke).
Sikujua kama yule mtu amenitumia picha ya namna hiyo, mpaka pale nilipofika nyumbani na kuangalia simu na kukutana na missed calls lukuki, za Boss zipo 21, na za watu wengine pia. Bahati nzuri message haikwenda kwa wazazi. Kulikuwa na missed call ya Boss hadi mida ya saa tano kasoro.
Sasa kuna mgongano ulishawahi kutokea kati ya mimi na Boss, ingawa nilimwomba msamaha, lakini alichukua muda kuamini kwamba ilikuwa ni bahati mbaya. Kwa kweli kwa hii picha sijui itakuwaje!
Wadau naombeni ushauri namna ya kujinasua maana naona hii issue yaweza kuwa nzito! Sijajibu chochote mpaka sasa, nafikiria labda nizime simu na kesho akiniuliza nimwambie simu nimeibiwa tangu jana mida ya jioni, lakini nashangaa kuna muda nilikuwa napiga inaita! Picha yenyewe nimeiattach.