Allan alikuwa ni character aliekuwa anatumiwa na mtunzi sir richard haggerd akiwa na wenzie kama henry Curtis,(inkubu )yaani tembo, pia umslopogaas, john good au bwana bougwan pia umbopa hao walikuwa washiriki wa allan katika vitabu tofauti sasa ungesema jina la kitabu kama mchangiaji hapo juu alivyojitahidi kukuelimisha pia napenda kusema tena ukipata kitabu unakuwa upo uzuri kuliko alieona picha coz matukio mengi yamefutwa au kupunguzwa katika picha.
Nahisi utakuwa ulisoma hadithi ya 'Allan quartamain na wenzake ".humo ndo utamkuta umslopogaaz na swaga zake za kizulu acha nikuonjeshe.
Maneno yako yote unayoyasema si ya kweli makumazahn sikuangamia kwa kupenda ukubwa na nguvu zaidi ila ni aibu juu yangu kusema ni uso mzuri wa mwanamke ndio ulioniangusha na sasa tutaona mambo kama tulioyaona zamani makumazahn? tulipowinda na kupigana katika nchi ya uzulu? ndio nitakuja! ikiwa kwa maisha !ama kwa mauti ni mamoja kwangu! mapigano yaanguke upesi na damu imwagike,nimepigana vita kwa miaka arobaini, nimekuwa mtu wa vita kuliko watu wa vita.