Nitapata mke mwema Jf?

Nitapata mke mwema Jf?

BIREGU

Member
Joined
Feb 10, 2013
Posts
31
Reaction score
8
Nimekuwa na mpenzi wangu kisha kuwa wachumba kwa muda wa miaka 7 wakati tupo kwenye mchakato wa ndoa alifariki ghafla kwa ajari,niliskitika sana na ilinichukua muda kufikilia kuoa,sasa ni mwaka wa tatu tangu kifo chake.Roho kiasi imetulia natafuta mke mwema wa kuoa.
Awe mcha Mungu Mkristo
awe anajua kuchanganua mambo-msomi kiasi kuanzia diploma na kuendelea
Awe mpenda maendeleo.

mwenyenia hiyo aweza kujitokeza tuanze mchakato wa maisha ya pamoja kama tukiridhiana.
 
Da! Pole sana kwa jeraha ya moyo
Nakuombea baraka na bahati umpata wa kukufuta chozi
=
 
Mke mwema anatoka kwa bwana sio jf. Ila jf yaweza kuwa njia ya kukutanisha nae,,,akili kumkichwa. Mwenye masikio na asikie
 
nimesikia kabisa bila chenga........ila kuna kigezo kimoja hapo ndio kimeniangusha.........
 
Mke mwema anatoka kwa bwana sio jf. Ila jf yaweza kuwa njia ya kukutanisha nae,,,akili kumkichwa. Mwenye masikio na asikie

Mbona wake wema tupo hata hapa weye!!!!!!

BIREGU pole sana kwa kumpoteza mpendwa wako, nakuombea umpate mke na awe mwema!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mwenyezi Mungu akujalie , mwenye kheri na wewe, na akutimizie haja ya Moyo wako. Usiache kusali wakati unaendelea kutafuta.
 
kwani wa kwanza ulimpataje? maana unasema unahitaji mcha Mungu,mkristo nilifikiri ungetumia maelekezo ya kikristo neno lisemavyo "......mali na.......mtu hupewa na wazazi mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana"...."nitakutafutia msaidizi wa kufanana nawe" ni hiari yako kujitafutia mwenyewe au na member wa jf? au umuombe Bwana ambaye anakuwazia mema siku zote akupe mke atakayekufaa.
 
hapo kwenye RED ndo wanafanyaje? ni kwamba unamwomba tu Bwana akuletee nyumbani au unamwomba Bwana huku unatafuta akuonyeshe yupi ni bora kwako?
haya maandiko wakati mwingine tunayazungumza bila kuyaelewa.
All the best BIREGU, katika tafuta yako mwombe na Mungu akufunulie
 
Last edited by a moderator:
Nimekuwa na mpenzi wangu kisha kuwa wachumba kwa muda wa miaka 7 wakati tupo kwenye mchakato wa ndoa alifariki ghafla kwa ajari,niliskitika sana na ilinichukua muda kufikilia kuoa,sasa ni mwaka wa tatu tangu kifo chake.Roho kiasi imetulia natafuta mke mwema wa kuoa.
Awe mcha Mungu Mkristo
awe anajua kuchanganua mambo-msomi kiasi kuanzia diploma na kuendelea
Awe mpenda maendeleo.

mwenyenia hiyo aweza kujitokeza tuanze mchakato wa maisha ya pamoja kama tukiridhiana.

sina hakika kama utampata kwa haraka hivyo, kwa kuwa unaonekana una kawaida ya kuwachezea mabinti wa watu muda mrefu kiasi hicho. unawezaje mheshimiwa unakaa uchumba miaka saba na binti wa mtu?. hujaongea vizuri kuhusiana na ajali ya huyo binti-ikiwezekana alikufa akiwa anawaza alivyopotezewa muda na wewe, mawazo yakawa mengi akagongwa njiani.hata hivyo nakutakia mafanikio mema-umpate akupendae-usichukue miaka saba lakini
 
hapo kwenye RED ndo wanafanyaje? ni kwamba unamwomba tu Bwana akuletee nyumbani au unamwomba Bwana huku unatafuta akuonyeshe yupi ni bora kwako?
haya maandiko wakati mwingine tunayazungumza bila kuyaelewa.
All the best BIREGU, katika tafuta yako mwombe na Mungu akufunulie

FP,u made my day.....get like
 
Last edited by a moderator:
pole sana@mtoa mada!mungu yupo,na ni mwema atakutimizia haja za moyo wako
 
Mke mwema anatoka kwa bwana sio jf. Ila jf yaweza kuwa njia ya kukutanisha nae,,,akili kumkichwa. Mwenye masikio na asikie

Halafu wa JF ndio hao hao wa club, street, maofisini, church, misikitini na hata kwenye sebene hivyo usitegemee muujiza.
 
Kaa na uchanganue mambo kwa kina sana ili uweze pata mke mwema,
maana siku hizi walaghai ni wengi yaani wanakupenda kwasababu ya kitu fulani,
hivyo chukua muda na umchunguze utakaye mpata na sio kukurupuka tu, bila kufanya uchunguzi yakinifu.

Nakutakia mafanikio mema.
 
hapo kwenye RED ndo wanafanyaje? ni kwamba unamwomba tu Bwana akuletee nyumbani au unamwomba Bwana huku unatafuta akuonyeshe yupi ni bora kwako?
haya maandiko wakati mwingine tunayazungumza bila kuyaelewa.
All the best BIREGU, katika tafuta yako mwombe na Mungu akufunulie

Nimekupata vema FP nilichokiandika nakielewa ukimuomba Bwana yeye ndo atakuongoza namna ya kumpata mkeo au mmeo ndiyo unaweza funuliwa katika maono,unaweza kutana na mkaka/mdada ukasikia sauti ya Roho mt. akisema huyu ndo mkeo/mmeo,mnaweza kuwa marafiki wa kawaida bila kumega mkate baadaye Bwana anawathibitishia kuwa ninyinyi ni mke na mme,ila haya ni mambo ya ndani sana ya kiimani wengi wanaweza pinga kwa sababu mambo haya yanahitaji utakatifu na uongozi wa Roho mt. hayo tu kwa machache.kama mambo ya kiimani yamekupita kushoto pole ila jipe moyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom