Nitamwekea pingamizi Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitamwekea pingamizi Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lukolo, Sep 7, 2010.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndugu wanaJF, nimeanza kuwasiliana na baadhi ya maadvocate kuona ni kwa vipi tunaweza kumwekea pingamizi Kikwete asigombee Urais kutokana na sababu zifuatazo:

  Sababu ya kwanza Inatokana na afya ya kimwili na kiakili ya mgombea huyu: Afya yake ni yenye mashaka makubwa kiasi cha kwamba inatia shaka kama ataweza kuwa kiongozi mzuri na makini katika muda wa miaka mitano ijayo.

  Afya ya mwili: Tuna kumbukumbu ya kuanguka jukwaani kwa zaidi ya mara tatu pasipo maelezo yoyote ya msingi yanayotolewa juu ya kuanguka kwake. Kwa kuwa ni nadra kwa binadamu yoyote asiye na maradhi ya kifafa kuanguka mbele za watu, na kwa kuwa Kikwete hana kifafa, naamini ya kwamba ana matatizo makubwa ambayo ni zaidi ya kifafa, na hivyo hataweza kusimamia majukumu makubwa ya kuiongoza nchi.

  Afya ya akili: Kutokana na ahadi mfululizo zinazotolewa na mgombea huyu kupitia CCM, kuna dalili za wazi kwamba hayupo katika hali yake ya kawaida ya kufikiri kabla ya kusema. Tangu aanze kampeni ameshaahidi kununua meli kadhaa, na kujenga viwanja viwili vya ndege vya kimataifa zaidi ya kile cha Dar es salaam ambacho kinatia aibu kukiita kiwanja cha kimataifa.

  Mgombea huyu:
  • ameshindwa kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi jijni dar es salaam katika muda ya miaka mitano aliyokuwa madarakani,
  • ameliua shirika la ndege Tanzania ATC.
  • Ameshindwa kuanzisha usafiri wa uhakika wa reli nchini,
  • ameshindwa kuimarisha miundombinu ya barabara vijijini na mijini ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kupunguza adha ya kusafirisha mazao hayo kwenda sokoni (Na kwa bahati mbaya au nzuri barabara ndiyo tegemeo kubwa zaidi la usafiri kwa watu wa hali ya chini),
  • ameshindwa kumalizia uwanja wa ndege wa kimataifa ulioanza kujengwa Songwe Mbeya wakati wa Mkapa,
  • ameshindwa kukamilisha mipango ya Mkapa ya kupanua uwanja wa ndege wa JK nyerere ambao mipango yake ilianzishwa na Mkapa tangu 1997,
  Cha ajabu anajadili kuhusu kuongeza viwanja vingine viwili vya ndege vya kimataifa na kununua meli. By the way, ndege ni usafiri wa kumsaidia nani? Watanzania tulio wengi hatuna uwezo wa kusafiri kwa ndege kutokana na uwezo wetu mdogo. Badala aimarishe miundombinu ya barabara na reli au kuongelea kuhusu kuimarisha miundombinu ya umeme ili aanzishe treni za umeme ambalo ndiyo tegemeo letu kubwa la usafiri anaongelea ndege ambazo zinatumiwa zaidi na mafisadi na wafanyabiashara wakubwa, na zaidi ya yote ndege hizo kimsingi hazipo, maana ndege za serikali alishazifisadi.

  Kwa ahadi kama hizi napata wasiwasi kwamba Mgombea uraisi huyu si mzima (ana tatizo la akili). Amesahau mengi aliyoshindwa kuyatekeleza wakati ambapo serikali ilikuwa na pesa za kutosha (kwa mfano kujenga reli kutoka Mtwara hadi mbeya) na sasa anaongelea utekelezaji wa ahadi nyingine ambapo nchi inaendeshwa kwa madeni. Ataweza vipi? Kwakuwa katiba inasema Rais mgonjwa wa kimwili au kiakili anapaswa kusimamishwa, basi naona ni vema akasimamishwa kabla hajaingia Ikulu na kutusababishia hasara hapo hali yake ya afya itakapozidi kuwa mbaya na kulazimika kufanya uchaguzi mwingine.

  Sababu ya pili ya kumpinga mgombea wa CCM ni kwa sababu ya udhalilishaji mkubwa uliofanywa na chama chake kupitia kwa katibu wake Mkuu Yusuf Makamba,na magazeti ya serikali dhidi ya mgombea wa CHADEMA juu ya ndoa yake na upadri. Kauli za Yusuf Makamba na kejeli za magazeti ya serikali dhidi ya Dr Slaa, yamemshushia utu na heshima yake mbele ya jamii jambo ambalo halikubaliki kisheria. Kwa kukiuka sheria hii ya usawa wa binadamu na utu wa mtu, hawastahili kuiongoza nchi.

  Nina tuhuma nyingine Lukuki dhidi ya mgombea huyu ambazo baadhi ya mawakili wanaendelea kuzipitia kuona kama zitaweza kutumiwa kama kigezo cha pingamizi hilo.
   
 2. E

  Edo JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kila la kheri
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Good luck
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Sababu ulizotoa ni za msingi, ila ukitaka pingamizi hili liwe na nguvu inabidi ulifanye kama la wananchi wenyewe si la kwako binafsi - wewe uwe pioneer utembee nchi nzima ili kupata wananchi wanaoliunga mkono pingamizi hili kabla ya kuliwakilisha mahakamani.

  Uliite "pigamizi la wananchi dhidi ya mgombea Urais wa chama cha mapinduzi" wazo langu.

  Good Luck - tupo pamoja mkubwa.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wow!! This sounds nice. Nafikiri wazo zuri sana. Kuna kila sababu ya kuliangalia upya katika mtazamo huu. Thanks
   
 6. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Interesting . . . . Ni sheria gani itatumika kumwekea Pingamizi?
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9, Sheria ya 1992 Na.4 ib …Na.20 ib.12, Sheria ya 1994 Na.34 ib.6

  Kuna wanasheria nimewaconsult bado wanayachambua kwa undani haya mambo. Na yakiwa na nguvu basi tutayapeleka kwa wananchi ili sauti ya umma iwepo (kwa mjibu wa ushauri wa Elnino) katika harakati za kumwekea pingamizi.
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  all the best mkuu :becky:
   
 9. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama inawezekana atatoka 2 kwa njia yoyote ile, adui muombee njaa 2
   
 10. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280


  Mambo yanawezekana kabisa, ila ndo hivyo sheria zinatuzingua saana, hao jamaa maadvocate wanatapa ulaji maana wakivalia njuga hilo suala, milioni 60 zipo jne nje kwa JK. Ila kama litakuwa suaala la wananchi then itakuwa poa zaidi.:A S-coffee:
   
 11. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Thank you, this is more interesting:

  Mkiona kuna hoja za kisheria chukueni supporters wote wa opposition ambao will support the move.

  Yule Bwana aliyempinga mahakamani kafikia wapi? (Not CHADEMA).
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  all the best mkuu, ukihitaji signature nipo......
   
 13. D

  Dopas JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Big Up sana. Umetoa sababu zenye uzito mkubwa kwa faida ya watanzania.

  Kwa vile muda unasogea haraka. Kwa maoni yangu wakati wa kampeni za CHADEMA, ukifika na upewe nafasi ya kuwaeleza wananchi hasa juu ya ugonjwa wa Akili wa JK ambao ndio ulioingiza nchi hii kwenye dimbwi la umaskini, kwani anayoyaahidi leo, kesho hayakumbuki na kuyaahidi mengine.

  Natumaini wananchi wengi wataona umuhimu na kumwekea JK na chama chake pingamizi la kuingia tena Ikulu kwa kuipigia kura Chadema. Hili linawezekana kuliko kupita kwa kina Augustino Ramadhani, na walio chini yake ambao hushika adabu kwa JK.
   
 14. b

  bobishimkali Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wanamwogopa mgombea wa CCM kikwete na wanajua kwamba hawawezi kumshinda kikwete katika uchaguzi wa 2010,hivyo wanataka ushindi wa mezani usiokuwa na ushindani kwa kumwekea pingamizi.Hizo ni dalili za kushindwa na kukata tamaa.CHADEMA wasubiri chaguzi nyingine za miaka ijayo watakapojipanga vizuri
   
 15. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Vita ni Vita Mura . . . . havina macho, havichagui Silaha . . . Ni piga nikupige!
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli mwaka huu vichaa wengi tutawaona hasa hapa jamvini!Hauko peke yako,mpo wengi tunasubiri uchaguzi upite tuwapeleke Mirembe kwa matibabu,hatuwezi kuwaacha mkitaabika kwa aibu mitaani huku mkipiga kelele ovyo kama mavuvuzela!
   
 17. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pingamizi hili linafaa litolewe tena na Dr Slaa kwani ndiye mwenye Locus standae ya kumuwekea mgombea wa kiti cha Uraisi.. Slaa anaweza kuweka pingamizi kwa vipengele vilivyotajwa na pia adai kwamba afya ya mgombea wa ccm ni ya mashaka.. hivyo itamlazimu Kikwete kuthibitisha afya yake kwamba yuko fit... Dr slaa inabidi aweke Pingamizi hili siku tano kabla ya uchaguzi ili kikwete aondolewe maana pingamizi litakuwa bado kutolewa majibu... vingivevyo itabidi uchaguzi uahirishwe...Kwani kama mgombea ana pingamizi, hawezi kupigiwa kura wakati pingamizi bado halijaamuriwa...
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha aa, karibu mkuu. Kama wewe hujaona kama hizo sababu ni za msingi basi wewe ndo wa kutangulia mirembe. Pole sana kwa homa, Mungu atakusaidia utapona kaka/dada
   
 19. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wazo zuri! Nafikiri kuna haja ya kushirikisha wapinzani wote. Maana suala la afya ya mgombea halimhusu Slaa peke yake. Itabidi kuangalia ni kwa vipi Lipumba na wapinzani wengine wataliunga mkono jambo hili. Naamini wale wa CHADEMA hawatakuwa na shida katika hili.
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Unategemea kutumia ushahidi gani, hasa kwa hayo mawili ya kwanza?
   
Loading...