"Nitakuja kumwona mwalimu wako" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Nitakuja kumwona mwalimu wako"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BRO LEE, Jan 7, 2012.

 1. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kisa hiki kilinitokea zaidi ya miaka 15 iliyopita.. Ungana nami..

  Wakati huo nilikuwa sekondari, mimi na mabinti tulikuwaa damudamu(kuongea, kusoma pamoja,utani nk), ni katika mazoea haya ilitokea binti mmoja akavutiwa na kampani yangu. Binti huyo alikuwa ni mpweke muda mwingi asiyependa kujichanganya hata na mabinti wengine, niliingiwa na udadisi wa kutaka kujua kisa ni nini kwa kuwa nilikuwa napenda sana kusoma maswala ya saikolojia katika magazeti nilihisi huenda nikawa na jambo la kumshauri.

  Tukaanza kutaniana na kuongea maswala mbali mbali lakini... binti alikuwa mgumu sana kufunguka. kadri nilivyozidi kuwa nae karibu ndipo nilipotambua hakutaka nijue historia yake.

  Baada ya kuzoeana binti akawa ananiwekea vimemo( wimbo au stika za kimapenzi) kwenye draw ya dawati, sikuwa najali sana kwa kuwa sikufikiria kuwa na GF(unaelewa maana yake kwa kibongo)'mupenzi". Mi niliendelea kumchukulia km rafiki zangu wengine.

  Zikanza kadi, kadi ya kwanza ilikuwa "GET WELL SOON" kwa kweli nilipata tabu kujua ujumbe wa kadi hiyo, kwa wakati huo nilikuwa na ka dictionary ka English/swahili kuanza kuunganisha neno moja moja ili kupata ujumbe ilikuwa kazi kwelikweli!!

  Kadi zikaendelea, maua na nyimbo zilizoandikwa kwenye zile karatasi za barua zenye "vikopa" picha za wapendanao nk. unafahamu slogan 'pata salamu jibu salam' nikaanza kutafuta kadi zinapatikana wapi. Duka la kadi lilikuwa posta( jina ckumbuki ila lilikuwa maarufu sana, wakati wa valentine's day lilikuwa linajaa acha kabisa).

  Tukaanza kutumia kadi na vijiua lakini nilikuwa najibu mapigo tuu, moyoni bado sioni km ni uhusiano wowote ulio makini. Kuna wakati nilipata tena wakati mguu kuelewa mwenzangu alimaanisha nini ktk mawasiliano, safari hii nilitumiwa kadi yenye picha mbali mbali zikiwa na maneno km ( you are ma ocean of love, valley of happiness...nk... that's why I LOVE U), kazi ilikuwa hapa; kwenye kadi hiyo alinakili wimbo wa " IT MUST HAVE BEEN LOVE...BUT IT'S OVER NOW", kwanza ckuwa naufahamu huo wimbo hivyo nilidhani ni ujumbe waka kaandika. Narudi nyumbani najiuliza nimemkosea nini?

  MKASA; Cku moja alinialika kwao, kwa kuwa ckuwa na nia ovu na nilimchukulia kama rafiki nikakubali. Nikaenda kwao muda wa mchana, nikawakuta "wazazi wake", nilikaribishwa nikapewa kinjwaji na baadae tulikula chakula cha mchana. Baada ya chakula binti alitumwa na mimi nikawekwa kitimoto na mdingi, nikatakiwa nijitambulishe na sababu za kwenda pale. Niliongea kwa kujiamini na kusisitiza bint alikuwa rafiki wa kawaida tu! Dingi hakuwa anaongea kwa ukali bali alinikuwa na mikwara mingi. Mwishowe akaniambia atanifuatilia shuleni kwa mwalimu wa darasa. Basi baadae binti alirudi nikaaga na kuondoka.

  Sikuwahi kumwambia binti kuhusu kilichojiri alipooondoka, lakini nilijitahidi kupata taarifa za binti huyo kupitia watu wengine na niligundua hakuwa na maelewano mazuri na wale walezi wake.Haikuchukua muda mrefu binti yule aliacha shule.
  Nilijifunza mpaka sasa huwa nachukua muda kumsoma mtu yeyote kabla ya kuwa nae karibu.

  Je mwana JF, unakumbuka kisa gani kilichokukuta wakati wa "FOOLISH AGE"
  ​
  ====Nitarejea na "BINTI WA MTANI===​
   
Loading...