NITAKUJA KUMHOJI SIRO

fakhbros

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
338
550
Kamanda Saimon Siro hakuwahi kuwa mwinjiristi..

Kamanda Saimon Siro hakuwahi kuwa diwani au mwenyekiti wa Kijiji..

Siro akiwa amezaliwa Katika nyumba yenye maadili ya mungu siku chache katika maisha ya utoto wake alipitia katika mafunzo ya kipaimala kabla ya Kupokea Sakrament iliyotoa nafasi ya ubatizo..

Siro mtiifu mbele za mungu Alie geuka kulitumikia hekalu la Shetani baada ya kuihangaikia dunia kwa miaka mingi na mwisho wa Safari yake akapokea tuzo ya utukufu wa mikono ya Rahabu Kahaba wa kuzimu...

Kiapo chake kilitengenezwa kwa gharama na matukio Kutoka Kazi mzumbe Kule Kibiti

Nilitamani kweli kuliko wimbo wa NEY usemao alisema /alisema mwalimu Yule siku zile za uhai wa nyota Kila Jambo lilimfanya kumtukuza yeye

Nakuona Sai ukiyaacha Magwanda na Salute ukiungana na wenza ulio wafitini

Kweli cheo ni dhamana sawa na ugoni kwa mke wa mtu..

Umetumika ukajisahau kwa mvinyo Mo Enegy.

Ni huyu huyu ambae idadi Kubwa ya watanzania wengependa kumuona akilisemea Taifa kuhusu Ismail wa Taifa hili alietoweka katika mikono ya Mungu..

Mtakatifu Siro kwa upako wake amerihutubia Taifa pasina Aibu na kuwaridhisha tu kuwa Yule mpendwa wao amepaa mbinguni kama Nabii Eria na Si muda ataweza kurejea akiwa salama nakuwaonyesha mikono isiyo na kovu Wala arama..

Japo mtakatifu Sai hakuwahi kuishi kwa karama lakini moyo wake umejaa elimu ya Ubashiri wa Mambo yasiyo jibika kirahisi mbele ya halaiki..

Sai Amezionyesha Ishara kwa Mafarisayo ili watumie karama zao kufumbua Mambo yaliofichika...

Ni hekima tu iwezayo kumfanya mwenye kiu kuondoa haja yk
Ikiwa kivuri kinaweza kulitikisa jiwe kuu Basi haja ya mapambano itaweza kutufanya kuamini Kila Lilo ndani ya mioyo yetu..
 
Back
Top Bottom