Nitajiudhuru nikikosa ubingwa: Kondic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitajiudhuru nikikosa ubingwa: Kondic

Discussion in 'Sports' started by JoJiPoJi, Aug 10, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Na Sosthenes Nyoni  KOCHA wa Yanga Dusan Kondic amesema atakuwa tayari kujiudhuru kuifundisha timu hiyo endapo itashindwa kufuzu kwenye michuano ya Afrika mwakani.

  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Kondic alisema kutokana na kufanya usajili makini wa wachezaji wake msimu huu haoni sababu za kumfanya ashindwe kufuzu.

  "Nafikiri toka nimefika hapa msimu huu nimekuwa makini katika kusajili wachezaji wa kikosi changu sasa kama nitashindwa hata kufuzu tu kwa michuano ya Afrika itakuwa haina maana na ni wazi nitajiudhuru kuifundisha Yanga.

  Kondic alisema kwa ujumla ligi kuu msimu huu itakuwa ngumu kutokana na timu nyingi kuandaliwa vizuri lakini akasema umakini katika mipango unamsaidia kutimiza malengo yake.

  Akizungumzia maendeleo ya maandalizi ya kikosi chake alisema ameuomba uongozi umwandalie mechi moja ya kujipima nguvu kabla ya ligi kuanza huku akisema **** uwezekano wa kucheza na mtibwa Sugar Jumapili Agosti 16 ingawa viongozi wake bado hawajamthibitishia.

  "Nimeuomba uongozi uniandalie mchezo mmoja wa kujipima nguvu kabla ligi kuanza ,bado sijathibitishiwa lakini kuna uwezekanano wa kucheza na Mtibwa Jumapili,"alisema Kondic.

  Kuhusu hali za wachezaji, Kondic alisema majeruhi pekee katika kikosi chake ni Hamis Yusuph ambaye aligongana kichwa na mwenzake wakati wa mazoezi na kupasuka sehemu ya juu ya jicho.
  Alisema kwa sasa mazoezi yake ameyaelekeza zaidi katika kuwafundisha wachezaji mbinu mbalimbali za kiufundi pamoja na kuwaunganisha ili waweze kucheza kitimu zaidi.

  Source : Mwananchi
   
Loading...