Nitajihusisha na financial markets maisha yangu yote

Mo Issa

Member
Jul 28, 2020
43
78
Hello wana JF

Ni matumaini yangu hamjambo na wenye afya tele na hata wale wagonjwa namuomba Mungu awaponye haraka.

Leo ningependa kuongelea hizi Financial Markets yaan Masoko ya Biashara za kifedha duniani. Imezoeleka na kusikika mara kadhaa hili neno pengine naamini unaelewa nini namaanisha hapa.

Kwa sasa dunia yetu imepiga hatua kubwa sana kiutandawazi kupelekea hata biashara nyingi kuja mitandaoni. Leo nitajikita katika zaid katika Biashara ya Forex kisha baadae nitaelezea Stocks Bonds na nyingine nyingi.

Nataka nielezee kidogo kuhusu Biashara ya forex kwa ambae ndo anaanza kujifunza, anatamani kujifunza au ambae amekata tamaa.

Biashara ya forex sio biashara ngeni kwa Tanzania, imekuwepo siku nyingi kidogo huko nyuma.. ni biashara ambayo inafanywa na Central banks mfano Bank of Tanzania (BoT), Commercial Banks, Governments, Hedge Funds na Makampuni makubwa, na Retail Traders (hawa ni wafanya biashara wadogo kwa maana wanakua na mitaji midogo)
Inahusisha kubadilishana pesa mtandaoni.. nitolee mfano. Ukiwa unaenda Kenya uko na Tsh 100k utafika mpakani ili kubadilisha Tsh yako kwenda Kshillings ili ikusaidie kufanya transactions huko Kenya. Kitendo cha kubalisha Tsh to Ksh tayari hiyo tunaita Foreign Exchange(Forex). Hapo anakuwepo ww uliye nunua na Aliye kuuzia.

Karne iliyopita foreign exchange(Forex) ilikua inafanyika Physically kama huo mfano wa Tsh na Ksh. Currently kwa sababu ya Technology kukua inaweza kufanyika online. Ambapo wanunuzi(Buyers) na wauzaji (Sellers) hukutana. Kitu ambacho kinafanyika ili wewe kuweza kufanya forex lazima upate mkutanishi.
Huyo mkutanishi (Broker) ndie anakukutanisha na buyers na Sellers kwenye soko la Forex. Brokers wapo wengi sana na wanapatikana mtandaoni. Kuna vigezo vya kumjua Forex broker ambae yupo legit yaani ambae sio scammer(mwizi) hili somo la siku nyingine. Haya tuendelee,,,

Tanzania ukilinganisha na nchi nyingne kama Kenya, South Africa, Namibia au Nigeria kwa hapa Africa bado Tanzania tupo nyuma kwa sababu ambazo nazielezea ndani ya sekunde mbili zijazo.

1. Hakuna elimu thabiti kujifunza na kuielewa Forex ni kitu gani. Forex ni biashara ambayo ni wide sana na inahitaji elimu kabla hujawekeza. Assume forex sio tu kubadilishana sarafu tu, unaweza trade commodities kama Gold, Mafuta (Oil), silver au Indecies kama Nasdaq au shares.
Mchezo unaotokea hapa Tanzania na watu kuiita biashara ya wizi ni hii hapa... Kwasababu ya uhitaji wa Elimu unakuta Kijana tu mdogo anaanza kujifunza kupitia YouTube au Google au forum yoyote... bila kujali ni muda gani ametumia kujifunza, anaweka pesa zake na kupata hasara. Hapa sasa ndo watu huamuwa kuiita majina kama utapeli na kadhalika pia nikichoona ni kuwa watu kwa kukosa elimu hushindwa kutofautisha kati ya Financial Markets hizi na Ponzi schemes(somo la siku nyingine hili, tutaona utofauti uliopo na pengine somo hili litawafanya watu kubadil mitazamo yao na kuwacha pia kufikiri biashara hizi ni kama betting).

Forex inahitaji discipline ya hali ya juu.. na kama huna itakufundisha. Ni industry ambayo ukiingia inakufundisha jinsi ya kuwa smart at age of 15 kama real man. Na hyo yote inatokana na kujifunza kila siku kuhusu pesa au investments. Sio biashara ya Kutajirika haraka kama ambavyo baadhi ya watu hudanganya watu wengine huko Instagram na ukiiendea kwa papara bila kujuwa unachokifanya utaumia kweli coz ni biashara ambayo ina risk kubwa pia hilo lazima ufahamu.

2. Kupenda pesa ya haraka. hii ni sababu ya pili kufanya wa-Tz wengi hua wanakimbia hii biashara. Forex inahitaji process na huwezi kuruka hata step moja.
Mfano : Ukiwa unaanza Forex trading ni lazima ujifunze/kufundishwa na mtu ambae katoboa tayari hujulikana kama Mentor ambae ndo atakae kupa muongozo katika biashara hii. Ukisha jifunza unaingia kufanya majaribio ya ulichojifunza kwenye Demo a/c ( ni account ambayo unapewa na Broker wako ikiwa na virtual money.. ni kwa ajili ya kujifunzia)

Nashauri utest ulichojifunza kwa muda usio zidi Miezi sita (6 months).. hapa ndo waTz tunakwama sasa.. unakuja siku mbili mtu kapiga msuli huko YouTube kesho kutwa anaanza kutrade real account.. bro usifanye hvo unakosea. Usiruke hatua utaumia vibaya mno.
Miezi sita umetrade ukatest ulichojifunza kama matokeo yako ni sawa. ( Hapa jipime kutumia myforexbook.com ukawa unatrack record zako)
Kisha sasa Fund account yako hapa nitaelezea vizur

Hutokea unajifunza forex ukiwa na hali ngumu ya maisha kwa maana.. pesa inakua ngumu. Nitakwambia trick ya kutumia. Nashauri kufund a/c pesa ambayo hata ikipotea isikuume au ikatengeneza emotions mbaya. Mfano kama unaweza afford kupata Dollar 100 basi fund hiyo.

Njia ya pili, kama huna pesa kabisa ila unaweza kupata hata tsh 20k.. ingia Google tafuta brokers ambao wanaweza kutoa account ya Cent. (Cent a/c inakua ni real kabisa lakini ukiweka dollar 1= inasoma $100 so kama uko na $5 = $500) hii itakusaidia kutest skills zako.

Trick hii ya kutumia cent a/c itakusaidia kuweza kutrade real money huku una-gain confidence ya soko same time unatest skills zako, same time unaearn Profits. Usinielewe vibaya.. kutumia cent a/c ni trick ya kutumia kama huna pesa kabisa.

Naomba niulize swali kama lipo kwa leo tuishie hapa.
IMG-20221027-WA0081.jpg
IMG_20221029_230611.jpg
IMG_20220623_190034_989.jpg
 
Hii bizinec haina 4mula kila unacho fanya humo ndani ni ku ' predict " kukisia/ kubashiri " soko lina muelekeo gani! Hakuna specific indicators wala strategies! Naweza nikakubaliana nayo kama kuna indicator inayotoa direction kwa zaidi ya 80% sijaona yaani nazo zina bashiri kama ww user unavyo bashiri! Ununue signal kwa gharama ambayo unaweza usiirudishe wakati pia hizo signal nazenyewe ni "densi100/100". Zesheni.

Hii kitu ingekua nzuri zaidi itengenezewe mtaala na kuwe kuna hata chuo kina toa kozi hii hata kwa level ya short course ili kila anaetaka ku shape ubongo wake aende.

Kinacho leta shida ni nature ya biashara yenyewe ukilinganisha na nature ya wa Tz wengi wamepitia kwenye ukata, na huku mitandaoni swala hili limerahisishwa na linaendeshwa kienyeji kiasi kwamba hata hao trusted wenyewe hua wanatafuta pakutokea, kufanya hii biznec kuonekana nayo ni DUBU lililo changamka na halina makelele kama lile dubu la bar.

Haya ndiyo wengi tumejifunza kwenye hyo kitu TUTOE TONGOTONGO
 
Ulichosema mkuu ni kweli kabisa kwa asilimia 90 wanaojinasibisha na biashara hii kwanza kabisa hawaijui hasaaa wanakurupukia. Lakin huwaaminisha watu kwenye hizo tango walizonazo wao hiki ndo kinawafanya hata waanaowaelekeza kufeli kufanya vizuri na hatimae kupata mahasara makubwa na kukata tamaa nitakwambia kitu.

Zipo njia nzuri za kujifunza na kwa hatua kadhaa itakayopelekea wewe kuijuwa vizuri biashara hiyo na utaifahamu vizuri ila itakuhitaji muda pia wakufanya mazoezi kadhaa...

Kinachowafelisha wengi wanaojifunza na ma-mentor wao ni kuwa kushikilia vitu/strategies ambazo hazifanyi kazi kwa sasa kwenye Market. upo wana base kwenye indicators,candlesticks pattern,chart patterns, trends na vitu kama hvyo wakat havifanyi tena kazi na badala ya kujuwa movements halisi za price,,,,so wengi wanaojiita mentors huwa hakuna walijuwalo zaidi hu-focus tu kwenye kupata pesa za kuwafundishia watu coz hata wao soko linawabamiza. Nikuhakikishie mkuu mentors wengi wana strugle kwenye market hivyo ili kuenjoy kwenye Forex na pengine pote pata mentor sahihi.
 
Kulikua na mentor experienced kama ontorio!!? Yule alizama kama Titanic na alikua trusted sana! Sshv hata hao mabroker ni wahuni watupu!? Suluhu ya hii kitu ingeanzishwa course maalum tu!
 
Kaka hakuna wa kuandaa mitaala kwa Tanzania yetu hii ila kwa nchi kama SA, Namibia na nchi nyingine nyingi za Ulaya zipo academy za mambo haya na mitaala ipo watu wanasoma hasaa. Ila kwa Tanzania hakuna ni wewe kujifunza kwa wanaolijuwa soko juu chini....

Umemtolea mfano Ontario hapo juu sitaki kutia neno kuhusu huyo mtu ila narudia tena 90% ya wanaojiita Fx traders na hizo Financial markets nyingine ni kuwa hawazijui hasaaa na hao ndo huleta dosari kwenye Industry hii na kuonekana ni ya kitapeli. Ikumbukwe kuwa hao 90% ya traders ndo hao wanaopiga makelele mitandaoni kwa kuwaonyesha magari,majengo ya kifahari pengine vyote vya kukodi za kupigia picha ili kuwahadaa Gurus never do that mkuu waganga njaa ndo hao so kama unataka jifunza achana na majina hasaa hao wanaojinasibisha na Uguru ila tafuta Maguruuu wazuri wanaolijuwa vizuri soko.
 
Tusaidie kitu kimoja mkuu! Course outline ya hii kitu means hii course yake itahusu masomo mangapi na mtiririko wa topics kwa kila somo! Material ya kusoma tutatafuta wenyewe! Liweke hapa hata pdf tukapambane nalo TUTAKUSHUKURU BAADAE
mocanu.gif
 
Sawa mkuu nitaaandaa hili soon.
Nashukuru sana pia, watashukuru sana wale walio umia bila kujua tutaingia class na matumaini makubwa na kama ww ni broker hatuto uza mechi haiwezekani utuletee keki alafu tukale kwingine! Ww ndio mentor wetu maswali yooote tuandalie majibu
 
Hivi nikitaka nijifunze ku trade Kwa njia rahis kabisa nianzie wapi mkuu, naomba muongozo
 
Tafuta mtu anaejuwa vizuri akuelekeze mkuu hakikisha anaijuwa vizuri coz wengi hawajui na ndo hufanya watu waone mambo ni magumu sana yasiowezekana kiasi cha kuwaza kuwa Forex ni utapeli. Ukimpata mentor atakupa A-Z nin ufanye wapi upite lipi la kushika na kufanyia kazi na lipi uachane nalo kiufupi awe vizuri coz lipo wimbi la Forex traders wasiojuwa chochote/ama kujuwa basics tu za mambo ambayo hayafanyi kazi sasa hivi hao ndo wengi wapo huko hufundisha so kuwa makini Forex utaiweza na utafanya vizuri... cha mwisho usiwaze utajiri wa kesho unapoingia bali weka nguvu nyingi kwenye kuijuwa kwanza ukiwa vizuri pesa utaiona.. mengine mentor utakayempata atakwambia mengi naamini.
 
Hii bizinec haina 4mula kila unacho fanya humo ndani ni ku ' predict " kukisia/ kubashiri " soko lina muelekeo gani! Hakuna specific indicators wala strategies! Naweza nikakubaliana nayo kama kuna indicator inayotoa direction kwa zaidi ya 80% sijaona yaani nazo zina bashiri kama ww user unavyo bashiri! Ununue signal kwa gharama ambayo unaweza usiirudishe wakati pia hizo signal nazenyewe ni "densi100/100". Zesheni.

Hii kitu ingekua nzuri zaidi itengenezewe mtaala na kuwe kuna hata chuo kina toa kozi hii hata kwa level ya short course ili kila anaetaka ku shape ubongo wake aende.

Kinacho leta shida ni nature ya biashara yenyewe ukilinganisha na nature ya wa Tz wengi wamepitia kwenye ukata, na huku mitandaoni swala hili limerahisishwa na linaendeshwa kienyeji kiasi kwamba hata hao trusted wenyewe hua wanatafuta pakutokea, kufanya hii biznec kuonekana nayo ni DUBU lililo changamka na halina makelele kama lile dubu la bar.

Haya ndiyo wengi tumejifunza kwenye hyo kitu TUTOE TONGOTONGO
kaka hujui nini unasema unalopoka tu! me ni trade japo sio wa mda mrefu kivilee ila nakwambia kuna trick zinafanya kazi kwa 90% sure, yani ukiingia trade 10 kama ulifanya analysis za uwakika ujue trade 9 zinakupa matokeo. Hili nimelithibitisha na ndo ninachokifanya sokoni. kitu kimoja unachotakiwa kujua kuwa mamenta wengi wa forex hawatoi siri zote yani menta anaweza kukupa trick ambayo hata yy anaitumia na kwa yeye anapata matokeo kwa 100% ila ww unapata 20% ni kwasabab hawafundishi kila kitu.
 
Kaka si kuwa hawatoi mamentor wengi hawaijui Forex ukichunguza zaid utakuta wengi wao pia wana strugle kupata profits hasaaaa.
 
Ila Forex wala sio issue ya kubahatisha vipo vitu vya kufata na utajuwa nini kinatokea hatua zote.. kila kitu utakifahamu na hakun supriz yyte utakayoiona kwenye Market kila kitu/price moves zote utazijuwa.
 
Back
Top Bottom