Nitajieni vyuo vya kusomea u-nurse

Nitajieni vyuo vya kusomea u-nurse

Tripo9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Posts
4,366
Reaction score
3,561
Nina mtoto wa kaka yangu amemaliza form four anataka asomee awe nurse wa hospitali. Naomben mnitajie list ya vyuo na mahala vilipo ndani au nje ya Dar es salaam
 
Haydom Nursing School (diploma-3 years) iko ndani ya Haydom Lutheran Hospital katika wilaya ya Mbulu-Manyara
 
Inategemea na matokeo yake vyuo vipo vingi tu
 
Ilembula school of nursing-mbeya, eukernford-tanga, st.raphael-kibamba(dar) ,sengerema school of nursing
 
ANA DIV FOUR YA POINT 31. Ana D ya chemistry na D ya dini tu

Ili mtu asome nursing ni LAZIMA awe amefaulu physics, chemistry, biology na at least D ya mathematics. Sasa hawa watoto wenu wakishafeli ndio anaanza kufikiria nursing sijui kama atapata. Nursing ya siku hizi imebanwa, haijaachwa kama teaching iwe for FAILURES! Mpe pole na mwambie ajipange kwa kitu kingine. Pamoja na BRN bado kuna pass hizo! Loh!
 
hadi vya private vimebana mkuu?
 
hadi vya private vimebana mkuu?

Mkuu waraka walionao wa qualification ni mmoja. Wakishadahili huwa wanatakiwa kutuma wizarani majina ya wanafunzi na ufaulu WAP. Kama hana viwango husika hufanyi mtihani.
 
Mkuu waraka walionao wa qualification ni mmoja. Wakishadahili huwa wanatakiwa kutuma wizarani majina ya wanafunzi na ufaulu WAP. Kama hana viwango husika hufanyi mtihani.

duh, watoto wetu tutawepeleka wapi siye jamani
 
duh, watoto wetu tutawepeleka wapi siye jamani

Mkuu dawa ni kuwahimiza wasome na kufaulu. Nursing isiwe option kwa wale ambao hawana hata credit za kwenda advance. Watoto wanakosa hata C za arts!! Na wananchi ndio wanàkuwaga wa kwanza kulalamika kuhudumiwa na watumishi was afya wasiokuwa na kiwango. Ndugu zetu waliofeli tunaona option yao ni kwenda nursing...!!
 
ANA DIV FOUR YA POINT 31. Ana D ya chemistry na D ya dini tu
Tazama tovuti ya Haydom School of Nursing utaona maelekezo yote. Lakini kwa alama hizi andika maumivu. Wanahitaji awe amefaulu CHEM, PHY NA BIOLOGY kwa kiwango at least cha D. Tofauti na hapo hakuna kitu hapo hata kama Dini amepata A.
 
ANA DIV FOUR YA POINT 31. Ana D ya chemistry na D ya dini tu

imtu,kairuki na masana!!.lakini ana D mbili tena ya chemistry na dini tu..?!.hawawez kumpokea mpaka awe na atleast D 3 ambayo ni chem,biology & physics.! richa ya nursng kwa alama zake sijui atasoma nini na atasoma wapi,labda kampala university gongo la mboto ndo watampokea,na ataanza na foundation japo vyuo vingne ukiwa na D 3 ndo wanakupokea kuanza foundation. huyo labda arudie mtihani vinginevyo sijui.
 
Majanga shule zetu za kata
 
ANA DIV FOUR YA POINT 31. Ana D ya chemistry na D ya dini tu

Ilibidi awe na D nyingine ya Biology kuweza kupata nafasi . Maana wanasisitiza kuwa na pass ya masomo ya chemistry na biology
 
Back
Top Bottom