Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Ni wazi kwamba serikali ya awamu ya tano imejinasibu kuwa na nia moja yaani kuhakikisha kwamba taifa letu linaingia katika mabadiliko makubwa ya kutoka kuwa nchi ya malighafi pekee bali pia kuwa nchi ya viwanda. Kwa tafsiri fupi ni kwamba Tanzania ya Viwanda itakuwa na sifa zifuatazo:
1. Kupungua kwa tatizo la ajira.
Maendeleo ya viwanda yatapelekea kutengezwa kwa ajira nyingi miongoni mwa kundi kubwa la vijana wanaosota mitaani jambo ambalo kwa upande wa pili litapunguza upotofu wa maadili hususani ujambazi, wizi, urahibu wa madawa ya kulevya na ngono uzembe kwa maana vijana watakuwa busy mashambani, migodini, baharini na misituni kuzalisha malighafi kwa ajili ya viwanda huku wengine wakiwajibika viwandani pasi na kusahau watakaohusika na biashara ya bidhaa mbalimbali MADE IN TANZANIA.
2. Kuimarika kwa uchumi wa taifa
Uwepo wa viwanda utapelekea kukua kwa pato la ndani maana Tanzania itauza bidhaa ndani na nje ya nchi pamoja na kupunguza ununuaji wa bidhaa nje ya nchi jambo linalopelekea kupunguza matumizi ya fedha za kigeni na kupelekea kuimarika kwa shilingi ya Tanzania. Vile vile taasisi za kifedha na miundombinu ya kiuchumi kama vile barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege vitakuwa katika hali nzuri.
3. Kuboreshwa kwa huduma za kijamii
Hatimaye Watanzania watafurahia huduma bora za kijamii miaka michache ijayo ikiwa ni sehemu ya matunda ya viwanda. Kwa mantiki hiyo wananchi hawatakosa tena dawa maana viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza dawa tutakuwa navyo. Nani hajui kwamba tayari ARVs zinazalishwa nchini kupitia kiwanda cha Mhe. Madabida?
Ndiyo hivyo, wananchi tutapata maji safi, umeme, shule nzuri na hata magereza yetu yataboreshwa ili yaendane na thamani ya Mtanzania wa Mwl. Nyerere.
Pamoja na hayo yote ukijumlisha na nia ya Rais Magufuli, nitajie Waziri, Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya anayeonyesha ubunifu wenye viashiria vikubwa kwamba Tanzania ya viwanda yaja. Korea Kaskazini waliwahi kufanya special recruitment ya watoto na vijana wenye vipaji maalimu kwa ajili ya kuwatengenezea mazingira ya ubunifu, ugunduzi na utafiti juu ya nini wafanye ili kutengeneza njia ya industrialization kupitia mazingira yanayowazunguka.