Nitajie sehemu moja Tanzania ambapo umeme huwa haukatiki au ukikatika ni mara chache tu

Mahali fulan uswahili sana. Morogoro eneo la chamwino nilianzia maisha. Nilikaa pale miaka 4. Hakuna hata siku moja umeme uliwahi kukatika. Na mpaka Leo hii. Ni kwa sababu wananchi wa happy walipata umeme kwenye line inayoelekea kambi ya jeshi mzinga.
 
Umeme wa Sumbawanga kutoka Zambia ni Uhakika kwa 100%, ukikata ni dkk 10 unarudi jamaa wako vzuri na nguzo zao kuja Tanzania ni Kitako cha Zege, choma pori uwezavyo lkn nguzo haidhuriki.
 
Ni mkoa wa Kagera tu ambao umeme wake haukati hovyo hovyo labda sehemu ndogo tu ya Muleba mjini hao kila jmos hawana umeme na sababu hazijulikani utadhan wanatumia umeme wa upepo
 
Hii kuna watu itawashangaza ila hapa mtaani ninapoishi umeme ukikatika basi ujue Dar nzima haina umeme
 
Hebu tuambizane wakuu

Nitajie sehemu moja tz ambapo umeme huwa haukatiki au ukikatika ni mara chache tu?

Binafsi sijawah kushuhudia sehemu kama hiyo ambapo umeme huwa haukatikagi kabisa au unakatika kwa nadra tena ukikatika unakaa dk 5 tu unarudi

Ni sehemu gani ambapo huwa hakuna tatzo la umeme?
Nilibaharika kufanya kazi Njombe aisee watu wakule wanaraha sana umeme kila leo upo,, mpaka nikashangaa wao umeme wanautoa wapi..
 
Back
Top Bottom