Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 31,139
- 88,800
Nissan wako serious sana kwenye issue ya EV na hybrids hivi karibuni. Kwa sisi wapenzi wa magari madogoa na economy, wametugusa sana na Nissan Note (hybrid) na Nissan Ariya (EV).
Sasa wametuletea all new Nissan Leaf 3rd gen, soon inaingia masokoni.
Wamefanya mapinduzi makubwa sana kuanzia architecture mpya, muonekano wa nje na ndani na charging systems.
Kwa kuanza na charging systems, Nissan wameachana na ile outdated system ya CHAdeMO na sasa wamekuja na system mpya ya J1772 kwa AC charging (ambazo zimesambaa sana na magari mengi yanatumia) na upande wa pili kuna port ya NACS kwaajili ya DC Fast Charging ambayo unaweza kutumia hadi charger za Tesla.
Pia Leaf kwasababu sahivi ina betri kubwa, unaweza kuconnect appliances za umeme moja kwa moja (V2L) ila iko limited to 3.5 kWh AC output. Kwa lugha nyepesi, ukienda camping na hili gari, unaweza pika wali kwa rice cooker (1kWh) bila shida.
Hapo kwenye battery, Leaf wameipa battery mbili 52 kWh (ili ndio dogo, zamani dogo lilikua 40 kWh) na 75 kWh (ili ndio kubwa, zamani kubwa ilikua 60 kWh) zote ni Lithium -ion na zote ni Liquid cooled. Hii ni bonge la step ukifananisha na air cooled za matoleo yaliyotangulia. Technology ya liquid cooling inasaidia sana kwenye battery management na inapelekea battery likae muda mrefu zaidi.
Range imeimprove kama zilivyo battery, sasa hivi zinaenda hadi kilometa 480 akwa single charger kutegemeana na trim.
Bei itakua kati ya $29,000 hadi $35,000 ambazo ni bei nzuri sana kwa features wanazozitoa.