1) Mabango ya biashara kila mahali, mirangi rangi tu isiyokuwa na mvuto wowote ule na wakati mwingine huhatarisha hata usalama wa watumiaji barabara
2) Uvunjaji wa sheria za barabarani kila mahala na kila wakati. Watu wanatanua bila sababu ya msingi, waajiriwa wa majeshi ya ulinzi, polisi, kampuni binafsi za ulinzi kujiona wako juu ya sheria za barabarani, kero za misafara ya viongozi, watu kuegesha vyombo vyao vya usafiri kila mahala hata kwenye kona, pikipiki za BAJAJ- Uendeshaji wao na maegesho yao yasiyo rasmi, watu kutoheshimu makutano ya barabara na mizunguko (kipu lefti) hususan pale kwenye makutano ya Mwenge na Sam Nujoma, kutokuheshimu taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu, watu kujivukia vukia hovyo tu barabarani, matuta kwenye dual carriage way na interstate highways, n.k